Lowassa Afunguka Mazito Kuhusu Wanachama Wanaofukuzwa CCM

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amewapa neno wanachama wa CCM wanaotaka kufukuzwa ndani ya chama hicho wakituhumiwa kumuunga mkono.

Akiongea hivi karibuni katika kikao cha Baraza Kuu la chama hicho kilichofanyika jijini Mwanza, Lowassa aliwasihi watu hao kujiondoa CCM na kujiunga na Chadema kwani kuna maisha mazuri zaidi ndani ya chama hicho kikuu cha upinzania.

“Lakini hivi karibuni kuna utaratibu wa kuwafukuza kwenye chama watu ambao waliniunga mkono. Wanafukuzwa wanaambiwa ‘ondokeni mfuateni Lowassa’.

"Nasikia kuna mipango mikubwa zaidi baada ya mwezi wa sita atakapokabidhiwa Rais Magufuli… kuna mipango mikubwa zaidi ya kuwaondoa kwenye chama,” alisema Lowassa.

“Sasa mimi nawaambia kwa niaba yetu. There is life outside CCM, nawaambia tena kwa ajili yenu, waje Chadema kuna maisha mazuri tu hapa. Wasibaki huko wananyanyaswa, wanabezwa wanafanya nini… waje tushirikiane tufanye kazi,” aliongeza.

Lowassa ambaye ni Waziri Mkuu Mstaafu alieleza kuwa CCM hivi sasa wanaumia kwa sababu kuondoka kwake na kujiunga na Chadema kuliiongezea nguvu kambi hiyo ya upinzani na kupunguza ruzuku kwa kiasi kikubwa kwa chama hicho tawala.
 
Ushauri mzuri sana huo, huu ndio wakati wa kukijenga na kukiimarisha chama kwa kuongeza wanachama wengi zaidi
 
kwa kumbukumbu sahihi ni KWAMBA LOWASSA HAJAWAHI KUSTAAFU UWAZIRI MKUU bali ALIJIUZULU au KUFUKUZWA NA BUNGE KWA KASHFA YA RICHMOND. USIPOTOSHE HAPA WEWE BINTI
 
Uchaguzi wa 2015 umenifunza kuwa Rais wa Nchi ni Powerfull hata kama Wafanyabiashara wote wataungana dhidi yake.
 
Back
Top Bottom