Lowassa afuata upako kwa 'Nabii' wa Nigeria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lowassa afuata upako kwa 'Nabii' wa Nigeria

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngao One, Jun 11, 2011.

 1. N

  Ngao One Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 33
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu mwaka 2008 kwa kashfa kubwa ya ufisadi ya Richmond, Edward Lowassa, ametuma ujumbe wa watu wawili waende Nijeria kukutana na Pastor TemitopeBalogun Joshua a.k.a. Prophet T.B. Joshua ambaye 'alimtabiria' Mbunge Beatrice Shellukindo kuwa Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

  Wajumbe hao wa Lowassa ni mtoto wake Frederick Lowassa na mshauri wake mkuu wa masuala ya vyombo vya habari, Absalom Kibanda, ambaye ni mhariri wa gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe.

  Frederick na Kibanda wako safarini Nijeria kwenda kuchukua 'upako' ili wamletee Lowassa asafishe nyota na kuepuka na dhoruba kubwa ya kisiasa katika kipindi hiki kigumu ambacho wajumbe wa NEC ya CCM wamedhamiria kuwafukuza mafisadi kwenye chama, akiwemo Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz.

  Wajumbe hawa wa Lowassa wanatarajiwa kukutana na TB Joshua siku ya Jumapili Juni 12, 2011, ambayo mchungaji huyo atakuwa anasherehekea birthday yake na atawapa "dawa" wamletee Lowassa Tanzania ili asafishe nyota yake.

  Ikumbukwe kuwa 'nabii' huyu wa Nijeria aliwahi kumwambia Mbunge wa CCM, Beatrice Shellukindo, kuwa anatabiri Lowassa atakuwa Rais ajaye wa Tanzania.

  Beatrice, ambaye mume wake William Shellukindo, aling'olewa ubunge kwenye jimbo la Bumbuli na kina Lowassa-Rostam-Chenge na kisha wakamuweka January Makamba, sasa amehamia kwenye kambi ya kumpigia debe Lowassa awe Rais pamoja tuhuma kubwa za ufisadi dhidi yake, ikiwemo kujilimbikizia sana mali, ufisadi wa Richmond, kununua hekaru la sh bilioni 1 London na mengine mengi.

  Siri ya Edward Lowassa nje | Gazeti la MwanaHalisi

  Eti huyu fisadi kweli anadhani atakuwa Rais wa Tanzania?
   
 2. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umetumwa na samweli sitta wewe punguwani
   
 3. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  Hao wameenda kuchukua waganga wa kienyeji wanajifanya wanaenda kwa TB Joshua kama geresha tu. Wamefuata waganga wa kienyeji huko.
   
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nawewe ni great thinker?
   
 5. W

  Warofo Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wewe unapakatwa kweli na Lowassa. Kila mara ujitokeza kumtetea bwana wako kwa pesa chache unazopewa. Kazi unayo kijana
   
 6. W

  Warofo Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 75
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno, maana Lowassa anatafuta Urais by any means necessary
   
 7. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280

  huyo tb joshua anahusiana vipi na mambo ya lowassa?kwani huyo joshu ni mganga wa kienyeji au ni nini?
   
 8. Nico1

  Nico1 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 60
  Hivi kweli hata kama angefuata upako wapi Mungu si mnafiki hata kidogo kama wapiga ramuli.
  hHi nchi ikiongozwa na mtu kama huyu tumekwisha na wala Watanzania hatujasahau bado tunauguza
  vidonda.
   
 9. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,768
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280


  nimecheka sana uliposema "ramuli"
   
 10. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 738
  Trophy Points: 280
  Mnataka kumchafua mtumishi wa Mungu kwa kumuunganisha na huyu fisadi nyangumi...
   
 11. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi kweli mimi na msimamo wangu itokee eti namkubali Lowassa kwa sababu tu kaenda kwa nabii au mpiga ramli! Atishikaye huyo mwendawazimu na pia lazima mfuasi wa hizo imani. Lowassa lazima ajibu hii hoja lasivo akubali kuwa bado anazipokea na kushabikia kashfa.
   
 12. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowasa ni mwizi mkubwa , ni sawa na shetan. Hawezi kusafishwa.
  Lowasa , rostamu chenge ni pembe tatu za shetani
   
 13. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  yaani fisadi katili namna hii ndo awe rais? basi nchi kwishney kabisa
   
 14. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Maswali na majibu ya humu yananifanya nicheke tu! bwahahahah hahaaaa haaaa!:behindsofa:
   
 15. G

  GunzInTheAir JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: May 25, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa naanza kuamini kuna baadhi ya watu wanaendesha maisha yao kwa kumuongelea Lowassa.
   
 16. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 0
  Mtumishi wa Mungu nani TBJ? USANII!
   
 17. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Kuna dhambi isosafishika kwa mujibu wa dini mloletewaNa wazungu na waarabu?
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Watu mbona mna jazba namna hiyo?? Huyo Lowasa hasafishiki.
   
 19. a

  alpha5 JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  ha ha hii kali
   
 20. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Sisi wateule tunatazama mchezo huu kwa umakini mkubwa! Lengo letu ni kupata kiongozi bora kwa wananchi wake, hayo makundi yatakufa kifo cha kadhia.
   
Loading...