Pistol
Senior Member
- Oct 13, 2015
- 194
- 86
Waziri Mkuu wa zamani na mgombea Urais na mjumbe wa Kamti Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais mstaafu wa Kenya Kalonzo Musyoka pamoja na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Peter Mathuki.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Falme za Kiarabu kwenye mji wa Dubai.
Makamu huyo mstaafu wa Rais wa Kenya pia ameshawahi kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha ODM Kenya na kuambulia nafasi ya 3 katika uchaguzi wa mwaka 2007.
Kalonzo Musyoka ameshatangaza nia ya kugombea urais chini ya mwamvuli wa CORD, katika muungano wa CORD Raila ndio anatajwa kuweza kupeperusha bendera ya CORD, japokuwa atapata upinzani mkali ndani ya muungano huo.
Kama inavyojulikana Raila Odinga ni swahiba wa Magufuli na Mbunge mmoja huko Kenya amemtuhumu Rais Magufuli kuwa anahusika na vurugu na maandamano ya upinzani nchini Kenya, maarufu kama #AntiIEBC. Maina Kamanda: Tanzania's Magufuli and South Sudan's Kiir funding Raila to distabilize Kenya
Je, kwa mtazamo wako mwana Jukwaa kuna nyuma ya pazia gani zinaendelea kati ya Magufuli na Odinga na kwa upande mwingine Lowassa na Kalonzo Musyoka?
Huyo Mbunge mwingine wa Afrika Mashariki aliyepo hapo kwenye picha kwenye picha hapo juu, Tanzania elections as seen in the light of EAC, anakaririwa akisema haya kwenye kipindi cha uchaguzi; "The current mood in Tanzania is that people want change. Most of the youth want their country to play a major role in the EAC," Mr Mathuki said. He added: "However, they are most concerned with what is in the EAC that they can benefit from, especially trade, employment and other integration activities." Mathuki said Lowassa seems to represent the views of most youths. "The young people are strong participants in this general election. They are very keen on the EAC integration process," he said.
Je, hawa madon wawili wa siasa za Bongo Lowassa na Magufuli mapambano yao yamehamia kumuweka mtu wao Kenya atakayewasapoti??
Tiririkeniii......