Lowassa afafanua kutoonekana kwake misibani

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
223
303
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu kutoonekana kwake kwenye misiba ya viongozi wawili wa zamani serikalini, Samuel Sitta na Joseph Mungai.

Sitta, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, alifariki dunia Novemba 7, akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa tezi dume na siku iliyofuata alifariki Mungai, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

Gumzo kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa ni kutoonekana kwa Lowassa, ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Lowassa aliliambia gazeti hili jana kuwa, kilichomkwamisha kufika kwenye misiba hiyo ni kuwa safarini Afrika Kusini alikokwenda kumuangalia mdogo wake, Bahati Lowassa aliyekuwa mgonjwa.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyu ndio mleta mabadiliko wa Nyumbu ambae hata homa ya mdogo wake tu anampeleka Africa kusini!!!!!!!

Chadema wanayohubiri na wanayotenda ni tofauti kabisa

"Ujinga hauondoki kwa kumchukia mwenye akili, umasikini hauondoki kwa kumchukia tajiri, kuhesabu dhambi za mwenzio hakukufanyi wewe kuwa mtakatifu," -
Peter Msigwa/Mbunge-Iringa Mjin
 
Huyu ndio mleta mabadiliko wa Nyumbu ambae hata homa ya mdogo wake tu anampeleka Africa kusini!!!!!!!

Chadema wanayohubiri na wanayotenda ni tofauti kabisa
Zile milioni thrity something zilizookolewa kwa safari ya Mwanza tungeambiwa zimeelekezwa wapi tungepiga makofi
 
Kwa nini watu wanahoji sana kutoonekana kwake wakati Mwinyi, Msuya, Salim na wengine wazamani hawajaonekana? Hii ndiyo inadhihirisha kuwa Lowassa yuko mioyoni mwa watu wote hasa zaidi ccm
 
Huyu ndio mleta mabadiliko wa Nyumbu ambae hata homa ya mdogo wake tu anampeleka Africa kusini!!!!!!!

Chadema wanayohubiri na wanayotenda ni tofauti kabisa
Alienda kumuangalia sio alimpeleka,wewe jamaa sijawahi kuona unaleta hoja ya msingi kwenye post.

Note:sina chama maana kwa akili yako finyu utaleta ujinga.
 
13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom