Lowasa; Serikali iwawezeshe wanawake kiuchumi

  • Thread starter ANC-KWA ZULU NATAL
  • Start date

A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
325
Likes
0
Points
0
Age
48
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
325 0 0
Lowassa: Serikali iwawezeshe wanawake kiuchumi

Dodoma. Mbunge wa Monduli (CCM), Edward Lowassa, amesema kuna haja kwa taifa kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuzingatia mchango wao mkubwa katika maendeleo na ustawi wa familia.
Lowassa aliyasema hayo juzi alipokuwa akizindua Jumuiya ya Akiba, Mikopo na Maendeleo ya Dodoma (Jamimado) katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, mjini Dodoma.

Jamimado ni Muungano wa Vikundi vya Wanawake Wajasiriamali mkoani Dodoma, wakiwamo wafanyakazi wa ngazi za chini katika sekta za umma na wafanyabiashara wadogo.

Alisema ni lazima Serikali ithamini jitihada za wanawake hasa walioko katika vikundi vya Kuweka Akiba na Kukopa kwa kuwa wanawake wakipata nguvu za kiuchumi wanazielekeza nguvu hizo katika familia na kusababisha jamii ipige hatua za kimaendeleo.

“Nathamini sana Saccos za kinamama, maana ukimwezesha mama umemwezesha baba na watoto, yaani familia nzima, ukiwekeza kwa kinamama umewekeza mahali sahihi,” alisema.

Lowassa alitoa mchango wa Sh10 milioni kama sehemu ya hamasa kwa jumuiya hiyo na kuwataka kuandaa harambee kwa lengo la kukusanya sh500 milioni.

Lowasa alisema ingawa amekuwa akihudhuria harambee, lakini hana fedha kama inavyoaminiwa na baadhi ya watu na kwamba alichonazo ni nguvu ya kushawishi watu. “Mimi sina pesa ila nina ushawishi mkubwa kwa watu…. mkiandaa harambee, mkaniletea watu wa kutosha, mtaona nguvu na ushawishi wangu…ninawahakikishia mtazipata hizo shilingi milioni 500,” alisema
 
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
325
Likes
0
Points
0
Age
48
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
325 0 0
Source; MWANANCHI
 
T

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Messages
15,337
Likes
339
Points
180
Age
28
T

thatha

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2011
15,337 339 180
Haya bwana tumeona.
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
15,045
Likes
5,770
Points
280
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
15,045 5,770 280
wanawake wengi hawana elimu -- wengi wao wamebakia kuwa ni wahudumu wa baa, na wengine wasiotaka kazi wapo kona bar na mabarabarani - mmeua elimu ya shule za msingi, mmeua ufundi na elimu ya kujitegemea ngazi ya shule za msingi na secondary, mmeua michezo mashuleni, mkajenga shule za secondary lukuki bila walimu na vifaa za kufundishia, mkaamua maksudi kuwanyima mishahara mizuri walimu sasa matokeo yake niyo haya, unaanzia wapi kumsaidia huyu msichana / Mwanamke? hata elimu ya ujasiriamali ni tatizo kwake
 
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
325
Likes
0
Points
0
Age
48
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
325 0 0
nazan wakiwezeshwa kwa kuanzsha vkund vya kibiashara kwa mikopo isiyo na rba itakuwa vzuri...serkali kaz kwenu
 
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2013
Messages
325
Likes
0
Points
0
Age
48
A

ANC-KWA ZULU NATAL

JF-Expert Member
Joined Jun 5, 2013
325 0 0
nazan wakiwezeshwa kwa kuanzsha vkund vya kibiashara kwa mikopo isiyo na rba itakuwa vzuri...serkali kaz kwenu
 

Forum statistics

Threads 1,274,333
Members 490,676
Posts 30,508,619