Lowasa mbuzi wa kafara kashfa ya Richmond

Kuchasoni Kuchawangu

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
604
340
Ni wazi kabisa ufisadi wa Lowasa juu ya Richmond haujathibitishwa na mahakama yeyote hapa Tanzania na hata nje ya nchi. Mara nyingi amekuwa akituhumiwa kuhusika na kashfa ya Richmond na yeye kukataa kuwa hakuhusika, na hili halina ubishi kwani hata CCM hawana ushahidi wa moja kwa moja juu ya ushiriki wake kwenye kashfa hiyo ndo maana walishindwa kumchukulia hatua kama kamati teule ya Mwakyembe ilivyoagiza. Hata ilipokuja Vua Gamba CCM haikuwa na ujasiri wa kumvua. Mara nyingi Lowasa amekuwa akimwonya Kikwete kwa mafumbo kama "Ukimwaga ugali nitamwaga mboga, Hatujakutana barabarani nk"
Inawezekana kabisa Lowasa aliamua kuulinda urais wa Kikwete usianguke, kwani kwa kutambua hilo Kikwete 2010 alikwenda kumnadi Lowasa na kusema ni mtu safi. Na Lowasa akadhani wapo pamoja maana hawakukutana barabani. Kwa haya aliyofanyiwa Lowasa hana sababu sasa ya kutomwaga mboga ili ukweli aliobaki nao moyoni kwa miaka saba ujulikane na Ukawa wampokee bila hofu ya kashfa ya Richmond tena. Lowasa hana sababu ya kuogopa sasa kwani aliowalinda na kuvaa fedheha wamemgeuka ni vema naye ageuke sasa bado ana nafasi kubwa kwenye madaraka ya nchi hii akiamua kusema ukweli watanzania wakaujua. NIMEFADHAISHWA SANA, NIMEONEWA SANA NAACHIA NGAZI YA CCM.
Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom