Lowasa aukana urais


Mkuu mbona umeeelezea vizuri kuliko hata mimi!! Yani ndio nilichotaka kusema. Marekebisho madogo tu, naona umezidisha chumvi kusema tunamwona malaika. Hakuna malaika, tunajua ni fisadi lakini pia ni kichwa he is an intelligent man. Kuna viongozi CCM hata danguro huwezi kuwapa waendeshe lakini lowasa unampa kampuni yako huku ukijua pamoja kuwa utaibiwa lakini faida utaiona na kampuni haitakufa sababu ni mtu mwenye PRIDE na ni mwenye chongo kati ya vipofu!
 
Unaposema Watanzania wengi wanamkubali, una ushahidi?? Maana hata hapa JF tukipiga kura sidhani kama tunaweza kupata hayo matokeo unayoyakadiria!! Hizo pesa za marafiki zake anazozigawa hovyo hovyo ndizo zitampeleka choonini 2015!!
Nilikuwa nahesabu kura kwa sample ya watanzania waliochangia uzi huu tu,naona jamaa amepita! Lakini bado najiuliza endapo jamaa alikuwa ameonewa kuhusu dili la kifisadi la Richmond ambalo bila shaka limeigharimu sana serikali yetu na lilisababisha kibarua cha jamaa(uwaziri mkuu) kiote nyasi.
Pia kwamba inakuaje mtu aliyeliingiza taifa kwenye matatizo makubwa katika cheo cha ngazi za chini(Waziri mkuu) apewe ukuu wa nchi; unaonaje?
 

Umeongea vizuri.lakini umekosea mkyembe na magufuli hawafai.hawa hawafikiri taratibu.watasababisha vita.Anatakiwa Raisi mwenye uwezo wa kufikiri na kutafakari siyo yule anayereact react kwa kutumia media.Kikwete namkubali sana anavyohandle mambo bila papara hata ingekuww issue kubwa namana gani.nimemkubali issue ya kagame na Joyce banda. Angekuwa mwakyembe au magufuli migogoro hii miwili ingekuwa mikubwa sana. Hata migiro hana sifa ya Uraisi ila ubunge anafaa.Huyu Slaa anafaa ila naye anatakiwa apate washauri wazuri sana.
 
Kufikiria kuwa Lowasa atakuwa ni rais ajae wa JMT ni kukosa fikra kwasbb 2015 urais wa JMT ni zamu yetu Wazanzibari. Vinginevyo, ikiwa kwamba ndo mnampenda sana na ni lazima akuongozeni basi mfikirieni kwa urais wa Tanganyika. Angalau serekali tatu zitakundoleeni kiu yenu ya kutaka kutawaliwa na E.Lowasa.
Ombeni sana dua rasimu ya katiba ipite ikiridhia serekali tatu.
 

Ndugu yangu, akili za wadanganyika ni kama za walevi wa gongo…utakumbuka ni juzi tu kodi ya laini za simu (simcard tax) imehamishwa halafu wakadanganywa kwamba eti kodi IMEFUTWA wakakubali na kuanza kukenua mimeno kama mazuzu…kimsingi kodi haijafutwa ila imehamishwa kutoka mkono wa kushoto na kuwekwa mkono wa kulia wa mtu huyo huyo (mvujajasho). Mtu hawezi kukuhamishia mzigo kutoka kichwani akauweka mgongoni na kukudanganya kwamba ameutua halafu wewe ukakubali kama zuzu!

Serikali yahamisha kodi ya simu - Kitaifa - mwananchi.co.tz


Upungufu na uzezeta wa akili za wapiga kura wa Tanzania ndio uliotufikisha hapa. Utadhani watanganyika wanavuta bangi. Wanalalamika kuhusu ufisadi lakini ikifika kipindi cha uchaguzi wanakubali kuhongwa fulana, ubwabwa na gongo, wanatoa kura za kishindo kwa mafisadi. Nchi hii imeishalaaniwa kitambo. Tukiwa na wapiga kura wenye akili za kuku na wenye njaa kama hawa sidhani kama tutafika.



 
haya sasa, bei ya umeme imepanda kwa 67% lakini mkumbuke kwamba huyo fisadi mnayemuunga mkono ndiye aliyetufikisha hapa kupitia ufisadi wake wa Richmond LLC. Msiwe wagumu wa kuelewa na wepesi wa kusahau.
 

Nani wa kumpeleka kwa pilato wakati ni wale wale,yaani kesi ya nyani unampelekea ngedere si watasaidiana tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…