Lowasa ampongeza JK, Tanzania kufanya vizuri kimataifa

ukuta2013

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
275
98
LOWASSA AMPONGEZA RAIS DK JAKAYA KIKWETE



Mhe.Edward Lowassa
Na Swahili TV


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania MheshimiwaEdward Lowassa, amemsifia RaisJakaya Kikwete kuwa ameweza kuifanya Tanzania kupata heshimakatika ulingo wa kimataifa, aliyasema hayo wakati akihojiwa na Swahili TV jijini Washington DC.

Alisema kitendo cha Rais wa Marekani Bwana Barack Obama kuja nchini na

viongozi mbalimbali wa mataifa makubwakumeonyesha Rais Kikweteanakubalika.


"Ni hivi karibunitu Rais Xi Jinping wa China, Rais Obama na Rais mstaafu wa Marekani George W.Bush walikuwa nchini Tanzania, hii inaonyesha kuwa Tanzania iko juu katika medani za kimataifa” alisema Mheshimiwa Lowassa.



Mheshimiwa Lowassa ambaye yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi, aliongeza kwa kusema, Rais Kikwete anastahili pongezi sana kwa hilo kwani sio rahisi kwa viongozi wa mataifa makubwa kutembelea nchi zingine labda kama mko juu sana katika medani za kimataifa.



Pia alisema Rais Kikwete amekuwa akihusishwa na utatuzi au ushauri wa kutatua matatizo mbalimbali ya nchi zingine na pia ameanza kuishirikisha Tanzania katika usimamizi wa amani katika nchi mbalimbali.

Tanzania iliweka historia hivi karibuni kwa maraisi wawili wa Marekani kukutana katika nchi moja kwa wakati mmoja, Rais Barack Obama na George W.Bush walikutana jijini Dar es Salaam mwezi huu.
 
Huu ni uwendawazimu kabisa,hivi kwa akili fupi,ujio wa marais wa mataifa ya nje wanadhani ni kwa manufaa ya Watanzania au manufaa ya nchi zao?eti E.L nae anataka kutuongoza!what a clap!
 
Huu ni uwendawazimu kabisa,hivi kwa akili fupi,ujio wa marais wa mataifa ya nje wanadhani ni kwa manufaa ya Watanzania au manufaa ya nchi zao?eti E.L nae anataka kutuongoza!what a clap!
Kwa vile akiri yako fupi huwezi kuona umhimu wake.
 
Kwani Rais wa China hajawahi kwenda Sudan ambayo record Yao ni mbaya kwenye Haki za Binaadamu?. AMA kweli ukiwa na kichwa cha kifisadi na ukazidi ugamba unakuwa kichwani tope tupu
 
Malimwengu,naamini Savimbi naye angekuwa hai basi angefika Tanzania
 
Kumsifia mtu hutokana na moyo wa mtu jinsi gani ameridhika na jambo fulani ambalo mwenzake kafanya maoni ya lowasa kumpongeza jk ni kuongeza nakshi kwenye sifa za jk zilizotukuka.
 
Mmmmh unafkiri kwanini mzee pale juu picha ya kwanza amenuna?anajua kuwa kuna tatizo naona nywele nyeupe anaanza kumsogelea jamaa ili kuangalia upepo kama atawekwa kwenye majina ya wagombea duh ama kazi kwelikweli
 
Kwa vile akiri yako fupi huwezi kuona umhimu wake.

Kwa uhandishi wako huu tu,mimi na wewe nani mwenye akili fupi?hauna hoja wewe siwezi kupoteza muda wangu ku argue na mtu aliye na umaskini mbaya kuliko umaskini wote(umaskini wa mawazo na u.j.i.n.g.a) eti mkubwa mzima una type with a confidence...kwa vile "AKIRI" yako! Go back to school son,sipoteze muda wangu na mtu kama wewe,tayari uko kwenye ignore list yangu
 
Sasa vichaa wakisifiana mbona hamna la ajabu?
settle down my fellow country man! Huyu raisi kikwete ni shujaa sana na ametuletea heshima ya kujulikana kimataifa kuliko kiongozi yeyote aliyetawala nchi hii. MImi sasa hivi nipo nje ya nchi na nimeshuhudia kwa kiasi gani nchi yetu ilikuwa haijulikani kabisaa ulimwenguni. Tena nakuhakikishia hata sauth africa walio wengi hawaijui Tanzania ipo wapi.

mwandishi wa habari maarufu wa Daily news alikwenda studdy tour south africa, na alipokuwa anjitambulisha kwa rafiki yake msauzi, alishtuka baada ya msauzi kumwambia tanzania ipo wapi au ipo ndani ya Kenya! HUyu mwandishi wa habari aliitoa hiyo article gazetini na ilishtua walio wengi!

Ushahidi mwingine ni kuwa mwaka 1980 Tanzania ilianzisha safari za ndege kwenda London, Yaani Tanznaia iliadhirika sana , kwa sababu ilikuwa haipati abiria. Ilikuwa inaenda London na abiria mmoja na kurudi patupu. kwa sababu abiria hawaijui nchi yetu ipo wapi!

wewe kubali au usikubali, nani anaipenda nchi ya Korea kaskazini hapa ulimwenguni? sasa heshima kiama hiyo ndiyo tulikuwa nayo sisi kipindi chote cha utawala wa kikomunisti(ujamaa na kujitegemea). Tanzania mwaka 1973 ilipiga marufuku mbio za mashindano ya magari maarufu kwa east african rally simply kuwakomoa Ulaya na marekani! mashindano hayo yamehamia senegal, tazama senegal inavyo vuma duniani!Mashindano haya yalijulikana duniani kote na na dunia ilidrawa aatention katika mashindano haya. Sasa raisi Kikwete kafanya kazi kubwa sana kurudisha heshima yetu aliyotuachia mkoloni.

Hongera sana Kikwete!
 
Ustaadh Abdallah.jpg
Ustaadh Abdallah?
 
Sifa za kukejeli na za kipuuzi,wananchi tunaishi maisha ya kuunga unga kama nini,halafu Ustadh Abdalah anasifia waliokuja kuibia taifa letu,Jk na Lowasa chungu kimoja....Richmond=Dowans=mafisadi=udini.
 
Hivi alipotaka avuliwe kofia moja kati ya zile mbili haya hakuyaona ? Hatudanganyiki .
 
Back
Top Bottom