mimi nilijifunza kiingereza toka nikiwa bado mdogo, lakini bahati yangu nzuri kiingereza changu kilikuwa sio cha ubishoo, bombast, kilikuwa hasa katika ufundi wa kutumia maneno ya kawaida na kujenga picha. katika uzungumzaji wangu wa lugha nyingi tu, iwe ni kabila yangu, kiswahili, kiingereza au hata kabila tu lingine, huwa napata burudani sana nikikutana na mtu anaongea lugha FASAHA. anachagua maneno hayo hayo lakini jinsi anavyoyatumia, anajenga maana mbalimbali na kutoa ujumbe wa aina mbalimbali: kutilia mkazo, utani, mahaba mazito, kutuliza, kuhuzunisha, kuliwaza, kufafanua jambo, n.k.
Nilipoona title hii: "lovers of English language..." nilipata hamu ya kuona kuna kitu gani, kumbe kilichozungumzwa sio hasa kwa ajili ya lovers of English language, maana niseme tu kwamba lugha hapo imebakwa. wala sifikiri kwamba kuna haja ya kuchukia kiingereza, au kifaransa. Na pia haikuzuii kujifunza lugha yako ya kabila, lugha ya kiswahili au lugha nyingine yoyote.
kujua lugha yoyote ni kupata silaha unayoweza kuitumia kwa faida yako. kujua lugha kwa ufasaha ni silaha kali zaidi. watu huguswa zaidi na mpangilio wa maneno, sauti, na vitu kama hivyo, na huweza kuhamasisha watu na pia kutumika kama kaulimbiu kwa vizazi na vizazi. fikiria maneno kama "I have a dream..."; au vile watu kama kina Mtikila wanavyoweza kutumia maneno kwa ufundi, na hata kuunda maneno kama "gabacholi" na likafikisha ujumbe kwa uhakika ziadi.
hata ukichunguza watu kama kina Obama, moja ya mafanikio yake ni jinsi anavyoweza kuhamasisha watu wanaomsikiliza, wakamwona anafaa kutokana na jinsi anavyoweza kufikisha ujumbe wake kwa uhakika. Hakuna bombast hapo. hata ulaya, marekani, si kawaida kukuta mtu anafoka bombast. hiyo ni yetu siye wadandiaji, malimbukeni.
Napendekeza hata vita dhidi ya ufisadi, ipiganwe kwa kutumia lugha pia, kwa ustadi, katika kufikisha ujumbe na kuhamasisha watu.