Love story

Manun'guniko

Senior Member
Jul 23, 2014
155
59
Habari zenu....nawaleteeni LOVE STORY...ni miriamu binti mzuri mpole na ambae amelelewa ktk mazingira ya kimaskini lkn n mwenye tabia nzur na mwenye kuridhika na maisha yake hajawahi kupenda ila amependwa na wanaume wengi ambao naweza kusema hawana malengo na yeye ila kumtamani kwa uzur wake binti aliyajua yote ndo maana alwakataa wanaume wote ...ktk kufanya biashara za kuuza matunda barabaran anakutana na brayan mwanaume ambaye alimkosakosa na gar lake anashuka na kumsaidia kuokota matunda yaliyodondoka ndipo nyuso zao zinakutana na brayan anabaini uzur alionao miriamu brayan anamsaidia lkn anakuja kugundua mguuni kwa miriamu kuna mikwaruzokwaruzo ndipo anamwambia twende hospital tukachek kama mwil wako uko sawa miriamu anamwambia niko sawa usijal endelea tu na safar zako,miriamu anainuka kwa kuchechemea na kuanza kuondoka lkn brayan anamfwata nyuma na kumsihi angarau apande kwenye gari ampeleke nyumbani baada ya brayan kumlazimisha sana miriamu anakubal kupelekwa kwao...brayan anashangazwa sana na sehemu ambayo miriamu alikuwa anaishi n nyumba ambayo haikuwa na tegemeo la kesho kuikuta imesimama...miriamu baada ya kufikishwa alimwambia kwa sura ya upole asante kisha akaingia ndani brayan aliwasha gar lake na kuondoka huku akiwa na shauku kubwa ya kumjua yule msichana ambae hata jina lake halikuwa alijui,wazazi wa miriamu walimshukuru mungu baada ya miriamu kuwaadithia yote yaliyomkuta
kesho yake hasubui alishangaa kusikia hodi inapigwa na alipoenda kufungua alikutana macho kwa macho na mwanaume alyemsaidia jana brayan kabla ya miriamu ajasema chochote brayan almwambia nimekuja kukuona na pia sikukuuliza jina lako nani miriamu alimwambia jina halina maana sana na kama umekuja kuniona nimeamka vyema nashukuru mungu ila ningependa kama usingekuja tena hapa wakat miriamu anamwambia hivyo brayan saut ikasikika tokea ndani ikiita miriamu miamu miriamu ilikuwa ni saut ya mama yake brayan kusikia vile alitabasamu alafu akamwambia na mimi jina langu ni brayan alafu akaondoka miriamu anae akajikuta nae ametabasamu kwa tukio lile mama yake alipotoka nje akakuta gari linaishia mama yake akamuuliza n nani yule miriamu akamwambia ni mwanaume ambae niliwahadithia jana amekuja kuona ninaendelejae mama akujaji sana
Siku zilivozid kwenda ndivo brayan alvozid kumtembelea miriamu,miriamu ilibid akubaliane na hali hiyo na mwisho wakajikuta wamekuwa marafiki wakubwa,wazazi wa miriamu hawakukubaliana na urafiki wao ku tokana na brayan kutoka ktk familia ya kitajil tofaut na wao maisha yao kuwa ya kimaskin sana miriamu alijaribu kufuata wazazi wake walivotaka lkn brayan hakukata tamaa na hal ilibadilika pale alipomwambia nakupenda miriamu kubal uwe msichana wangu ili siku moja tuwe mme na mke haikuwa rahis kwa miriamu kukubaliana na hilo japo moyön alikuwa tayar ameshampenda
brayan aliwabembeleza Wazaz wa miriamu sana na wakat huo alikuwa ameshawatarifu wazaz wake ambao walikuwa nje ya nchi kwamba kuna msichana anampenda na wazazi wake walimuhaidi mwez ujao wangekuja kumwona huyo msichana:jaman ee mi nimechoka see u next time
 
LOVE STORY-2
baada ya wazaz wa brayan kumuhaidi kwamba watakuja mwezi ujao na baada ya brayan kumbembeleza miriamu atimae miriamu anafunguka na kumwambia brayan ni kiasi gan anampenda japo tatizo lilikuwa bado kwa wazaz wa miriamu lkn brayan hilo halikumzuia furaha yake alifurah sana baada ya kukubaliwa na msichana wa ndoto zake.Miriamu alijitahidi sana kuwabembeleza wazazi wampe baraka zao ili mahusiano yake na brayan yawe ya furaha zaid kwasababu anaamin mapenz ya kwel hayaangalii utajiri wa mtu wala umaskin wa mtu hatimae wazaz wa miriamu wanakubaliana na mahusiano na wanawapa baraka zao kilichokuwa kimebaki ni miriamu kutambulishwa kwa wazaz wa brayan ambao wanakuja hivi karibuni.
Mapenzi yao yalikuwa ya furaha sana na brayan alimuhaidi miriamu kwamba hatokuja kumuacha kwa hali yoyote labda kifo ndicho kinaweza kuwatenganisha...siku zilienda na hatimae wazaz wa brayan walitua nchini kwa hamu kubwa ya kumuona brayan pamoja na msichana wake,brayan aliwapokea uwanja wa ndege lkn hakuwa amefwatana na miriamu kwasababu alitaka kuwasuprise wazazi wake wazaz walifurah kumuona mwanae kwa mara nyingne tena baada ya wazaz kufka nyumban brayan aliwaeleza jinsi gani anampenda miriamu na yupo tayar kumuoa siku chache zijazo maneno ya brayan na furaha aliyokuwa nayo usoni ndio ilivyozid kuwapa hamasa wazaz wa brayan kumuona huyo msichana...kesho yake hasubui brayan alienda ofisin kwao na baada ya kutoka alienda moja kwa moja nyumban kwa miriamu tayar kwa kumchukua kipenz chake kwa chakula cha jion lkn lengo kuu ni utambulisho kwa wazaz wake,miriamu alifurah pia alivaa gaun lake refu alilonunuliwa na mpenz wake, brayan alifika bila kuchelewa na kumchukua mpenz wake na akiwaacha wazaz wa miriamu wakifurah kwa ile hatua waliyofikia...walifika nyumban na kuwakuta wazaz wakiwa wanawasubir kwa hamu kubwa ndipo nyuso zao zilipokutana na msichana mrembo na mpole brayan alimtambulisha kwa wazazi na wazaz walifurah sana kumjua miriamu na ndipo wakakaribishana chakula na wote wakaket na wakaanza kula lkn ktk mazungumzo baba wa brayan akamuuliza unasoma au unafanya kaz gan miriamu bila hofu akamjibu sikubahatika kusoma kutokana na wazazi wangu kuwa masikin na sifanyi kazi yoyote nafanya biashara ndogondogo mama wa brayan kusikia vile akainuka kwa hasira na kumwambia brayan mtu gani huyu umetuletea ! Mi nilidhani ni msomi mwenzako kumbe ni msichana wa mitaani unatushushia hadhi ktk familia yetu miriamu kusikia vile machozi yalianza kumtoka hakuamini kama mapenzi yanaingliana na elimu kabla brayan hajafanya chochote miriamu aliinuka na kukimbia kutoka nje..."itaendelea"
 
Back
Top Bottom