Love or Lust: Ijue tofauti ya kupenda na kutamani

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,360
2,000
Ni vigumu sana kutenganisha hisia za kupenda au kutamani. Mara nyingi jinsia, zote wanaume na wanawake, huwa wanashindwa kutenganisha hisia hizi pale macho yao yanapogongana na kuziamsha hisia hizi kwa wakati mmoja pasipo kutarajia, hasa macho yanapoona kile tunachofikiri kinavutia.
love and lust.PNG
Hisia za kupenda au kutamani zote mbili zinaweza kuwafikisha watu wawili katika ndoa na kuishi kwa furaha maisha yao yote au kuishi kwa huzuni na majuto maisha yao yote. Hisia hizi mbili zenye nguvu ya ajabu hutupeleka kufanya maamuzi mazuri au ya hovyo kabisa na wakati mwingine kuharibu kabisa mwelekeo wa maisha ya mtu husika.

Kupenda ni nini?
Kila mtu anaweza kuja na tafsiri yake, infact kupenda kuna maana pana sana na kuna kupenda kwa namna nyingi, mimi nitazungumzia zaidi kupendana kati ya Mwanaume na Mwanamke. Kupenda ni kujali na kuwa tayari kujitoa kwa ajili ya mwenzako na kuwa tayari kuvumilia na kukubali hali yoyote ile. Upendo huvumilia, hustahimili, hujali, haujivuni, hauhusudu, hautafuti sababu, hutoa zaidi kuliko kupokea, hautafuti mambo yake yenyewe, huwa na huruma, hurekebisha pasipo hasira na zaidi ya yote upendo haushindwi.


Upendo hujengeka taratibu sana hautokei ghafla tu, ni kama mbegu ya mti ikipandwa huchukua muda mrefu tangu kuota na kuwa mti mpaka kuzaa matunda. Upendo kama mti, mizizi yake huenda chini sana, hata ukikatwa unaweza kuchipua tena na kuendelea kukua. Mti hukaa pale pale unapooteshwa na huwa hauwezi kuhama na kwenda sehemu nyingine, pale pale ulipo huikubali ile ardhi na kuipa kivuli na matunda, huvumilia wakati wa jua na wakati wa mvua vile vile. Wakati wa baridi na wakati wa joto wenyewe utaendelea kuwepo tu.

Kutamani ni nini?
Kutamani ni hisia kali sana ya kuhitaji kitu anayoipata mtu mara tu baada ya kukiona kitu kinachomvutia, na kutaka kukimiliki au kukitumia pasipo kujali lolote kwa wakati huo. Jinsia zote mbili huwa na hisia za tamaa, kutamani kunatokea baada ya kuona na kuwa na hisia ya kutaka kuwa na yule uliyemwona bila ya kujali yeye ni nani. Kutamani hutokea haraka sana tena kwa ghafla, tena kutamani huja na hisia kali sana na wengi huwa wanajidanganya na kusema kutamani eti ni “love at first sight!..ukweli ni kwamba ukimwona mtu kwa mara ya kwanza na kupata hisia za kumuhitaji, hiyo siyo Love at first sight bali inapaswa kuwa ni “Lust at first sight”. Hakunaga love at first sight.


Niifananishe tamaa na nini? Tamaa ni kama uyoga, huota haraka sana tena hauna mizizi mirefu kwenda chini, wala hauna matawi wala hauwezi kuleta kivuli wala kuzaa matunda. Jua likiwaka sana uyoga hunyauka na kufa. Uyoga unapenda sana maji, unyevunyevu na kivuli, kamwe hauwezi kuvumilia ukame. Uyoga ukikatwa hauwezi tena kuchipua, bali hujifia haraka sana. Uyoga unaota leo, tena kwa haraka na baada ya wiki moja au mwezi mmoja unajifia wenyewe.

Wengi hujiuliza; hivi nitajuaje kama ananipenda au ananitamani? Zifuatazo ni ishara ama matendo ya mtu anayependa au anayetamani, kuna tofauti na ukitulia utaijua tofauti hiyo;

1-Mwenye kukupenda: atataka kumfahamu yule anayempenda kwa undani sana na kumjua vyema, na kujenga naye urafiki wa karibu sana na sio kutaka kusex naye mara tu baada ya kufahamiana. Atatumia muda mwingi ili kukujua na kuvumilia wala hatakuwa na haraka ya kulala na wewe.
1-Mwenye kukutamani: kitu cha kwanza atakachotaka kutoka kwako baada ya kufahamiana kijuu juu ni kutaka ku-sex na wewe, atakuwa tayari kufanya kila awezalo aifikie tu nguo yako ya ndani, atakuwa tayari kukuonesha ni jinsi gani anakiu na mwili wako. Atataka kusex na wewe kwanza kisha ndiyo muwe marafiki wa karibu, ukikataa ku-sex basi atakuchukia sana.


2- Mwenye upendo wa dhati: mtakuwa mkiongelea naye mambo ya maana ya future, namna ya kuyakabili maisha na changamoto zake na siyo kuwaongelea celebrities muda wote au kufanya jokes muda wote. Atazungumzuia maisha kwa ujumla na siyo kuusifia uzuri wako au muonekano wako wa nje kila wakati.
2-Mwenye kukutamani: maongezi yake yatahusu sana muonekano wako wa nje, uzuri wako, mara zote atakusifia uzuri wako, atasifia sana mavazi yako, ataongelea habari za udaku, na jokes nyingi ili tu ucheke naye na kufurahi naye, hawezi kuongea na wewe mambo serious ya maisha. Kama ni mwanamke atasifia sana vitu vyako, gari, saa, viatu, simu au hata shati ulilovaa.


3- Mwenye kukupenda: anakuwa tayari kusema ukweli bila kuogopa chochote kile, hawezi kukudanganya ili tu akupate, atasema kweli, na hawezi kuji-pretend kuwa mtu ambaye siye, mwenye upendo uongo au pesa siyo silaha yake sababu anafahamu kuwa hata akikudanganya ipo siku utagundua maana yeye anakuwa na malengo ya muda mrefu na wewe, hivyo hawezi kukudanganya wala kukuhonga pesa.
3-Mwenye kukutamani: yupo tayari kusema uongo, atatumia pesa na uongo kama ikibidi, wala hatajali kusema uongo ili mradi tu akupate, anatumia uongo na pesa sababu hana malengo ya muda mrefu na wewe. Hata kama utakuja kugundua uongo wake hapo baadaye wala hatajali, sababu yeye lengo lake lilikuwa ni kukupata kwa muda ule. Mara nyingi hata huwezi kugundua ule uongo, maana baada ya kukupata hatadumu muda mrefu na wewe.


4- Mwenye kukupenda: anakuwa na hamu ya kuwajua na kukutana na wazazi au ndugu zako. Kama ni mwanaume anakuwa huru kukukaribisha nyumbani kwake, na kama ni mwanamke anakuwa huru kukutambulisha kwa marafiki zake na ndugu zake.(ingawa hichi wakati mwingine siyo kigezo cha upendo wa kweli).
4- Mwenye kukutamani: anakuwa hana haja sana wala hamu ya kuwajuwa wazazi wako au kukutana nao. Kama ni mwanaume utamwona anakuwa mzito sana kukukaribisha nyumbani kwake, mara zote atataka mkutane sehemu za starehe, au kwenye hoteli au lodge. Na kama ni mwanamke amekutamani tu, basi utamwona ana furahia sana mnapokuwa kwenye sehemu za starehe na hotelini kuliko nyumbani.


5-Mwenye Kukupenda: kwa dhati yupo tayari kuvumilia bila ya kufanya sex mpaka mfunge ndoa, atakuheshimu na kuujali mwili wako, ataheshimu hisia zako na hawezi kukulazimisha mfanye sex. Na hivyo hivyo kwa Mwanamke, hawezi kujirahisi kwako ili tu ufanyenaye sex.
5-Mwenye kukutamani: hawezi kuwa na wewe bila kufanya sex, kwake yeye sex ndilo jambo la kwanza na kisha mambo mengine yatafuata baadaye. Tena kama ni mwanamke amekutamani utaona jinsi atakavyojirahisi kwako ili tu akupe sex kwanza, wala hatajali lolote lile. Kwa mwanamke aliyekutamani, kwake yeye sex ndiyo silaha yake kubwa, na kwa mwanaume pesa na uongo ndiyo silaha yake kubwa.


6-Mwenye kukupenda: anakuwa yupo huru kukusahihisha hata kukukosoa bila ya kujali kuziumiza hisia zako. Ukikosea hawezi kukusifia bali atakukaripia kwa upole na uvumilivu pasipo kuwa na hasira wala haweki kinyongo, visasi na chuki moyoni. Siku zote atakuambia ukweli wako kwa faida yenu wote wawili.
6-Mwenye kukutamani: hana uhuru wa kukusahihisha wala kukukosoa unapokosea sababu ataogopa kuziumiza hisia zako. Ukikosea utasikia anakusifia na kukujaza ujinga na kisha atayaweka moyoni mwake, atasubiri siku akiwa na hasira ndipo atakapoyatoa yote.


Mara zote penye upendo wa dhati mwisho wake huwa mzuri tena ni wenye furaha na uvumilivu na kuheshimiana kwa dhati. Waliofunga ndoa baada ya kupendana kwa dhati huishi maisha ya furaha na amani. Upendo wa dhati hudumu siku zote na kamwe hutasikia habari za michepuko wala nyumba ndogo.

Penzi la tamaa mwisho wake ni kilio na majonzi. Wale waliofunga ndoa baada ya kutamaniana mara nyingi sana ndoa zao huvunjika na kama zisipovunjika basi hupitia mitafaruku chungu mzima na kuishia kuishi maisha ya huzuni na kukosa furaha. Kwenye ndoa kama hizi ndipo utasikia habari za michepuko, nyumba ndogo na watoto wasio wa baba husika. Penzi la tamaa siku zote huyeyuka kama mshumaa!

Kuna watu wengine wamekutana tu kwenye daladala, wanagonganisha macho na kutamaniana moyoni; wanajidanganya ni upendo, yanayotokea baadaye ni majuto. Kuna wengine wamekutana kwenye ndege, wanaishia kutamaniana na wengine hata kufunga ndoa na kuzaa watoto, baada ya muda lile "penzi la tamaa" linaisha, kinachofuatia ni kuachana. Kuna wengine wanakutana kanisani, misikitini, night club, popote pale, lakini mwisho wa siku kama ilikuwa ni nguvu ya tamaa, basi ni lazima mtasambaratika tu.

Katika kujuta, utamsikia mtu anasema.., “lakini tulipendana sana siku za mwanzo, sijui ni shetani gani aliingia kwenye penzi letu”... Iko hivi; ukiona hivyo fahamu kwamba ninyi hamkupendana bali mlitamaniana tu, mkajidanganya kuwa mnapendana. Na sifa moja kuu ya penzi la tamaa huwa linaisha na kuhamia kwingine. Bali wapendanao kwa dhati hata siku moja hawatengani, upendo wao huwa hauhamii kwingine, sifa kubwa ya upendo wa dhati ni kudumu ndani yenu maisha yenu yote.

Hizo ni baadhi tu ya ishara za kupenda au kutamani zinavyokuwa. Kuna mengi sana katika kutamani na kupenda hivyo na wewe unaweza ukaandika yale uyajuayo. Swali ni Je! Umependwa au Umetamaniwa?.....Ulipendwa au Ulitamaniwa? Jibu unalo mwenyewe.
 

Son of Gamba

JF-Expert Member
Oct 26, 2012
3,360
2,000
Most ov women are victims for falling in lust to love!, based on man's money and assets.....
Nakubaliana na wewe, lakini pia wanaume huwa wanatamani bila hata ya kuwa na pesa, na hapo uongo mwingi sana hutumika ili kumpata yule anayetamaniwa.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
57,901
2,000
1 Wakorintho 13
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
 

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
3,163
2,000
U
1 Wakorintho 13
4 Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
5 haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
6 haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
7 huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
8 Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
Umejibu vyema...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom