Kasie
Platinum Member
- Dec 29, 2013
- 22,801
- 43,177
Good Afternoon ladies and gentlemen,
It is my pleasure to great you this morning and I feel like sharing this with you whats fills my heart, sorry to those who will see this as nonsense but to Kasie it is excitement, am glowing, am happy, may be because am single thats why this scene makes me glow and feel joyous all the night to this noon.
Haya wacha twende kazi maana hapo nilikuwa kama mnywaji wa maji ya dhahabu aka mlevi wakishapata chupa 3 basi lugha inabadilika na anaanza kuzungumza kiingereza hata kama hajasoma. Sasa mie nikiwa joyous basi najikuta tuu lugha ni za kiingereza yaani hata smile ya kiinglish................ this is Kasie.
Jana siku ya Nyerere day ikiwa ni siku ya mapumziko Bi. Mkubwa alikujanitembelea bagamoyo (kwa mara ya kwanza nimeongelea habari ya bimkubwa) Bi. Mkubwa alidondoka bafuni na akavunjika mkono wa kushoto, sasa matibabu ya Tanga Muheza hayakumpa nafuu ikaonekana hali inakuwa mbaya ikabidi familia tufanye mpango aje apate matibabu Muhimbili maana umri wake umesonga na ni mnene haswaa sasa wasiwasi ukaja kwenye kuunga mifupa asije pata ulemavu wa uzeeni. Mwanzo wa wiki hii akaripoti muhimbili na akapata appointment ya kufanyiwa operation wiki ijayo. Kule Tanga baada ya kupiga x-ray daktari akasema arudi nyumbani hadi uvimbe uishe kasha arudi hospitali wamfunge POP ili mkono uunge na alisema mifupa imevunjika. Mwezi ukaisha uvimbe haupungui ndo hapo tukaona bora aje Dar kwa matibabu zaidi.
Juzi alinipigia simu kuwa anaomba siku ya mapumziko ya Nyerere Day aje Bagamoyo tuongee mie nikamwambia poa njoo tustorishe. Saa tatu asubuhi dereva kamfikisha home nikamwambia wewe rudi mie ntamrusidha, nikamwambia binkubwa leo sina upako wa kupika twende ztu mahali tukakae tuhudumiwe, akakubali. Tukaenda moja ya hoteli za Badamoyo ina garden iliyotuliaaa na haina wateja wengi. Tukakaa hapo na kuanza kustorisha hapa na pale maongezi lukuki tukanywa chai, mchana tukala hapo hapo na vinywaji vikaendelea.
Kwenye mishale ya saa 11 jioni hivi akapita kaka mmoja hivi from nowhere . Akafika mahali tulipokuwa tumekaa na bimkubwa akamsalimia mama kwa heshima zote kisha akamwambia pole mama utapona tuu ukipata matibabu sahihi, na hapo itachukua kama miezi mitatu kupona, utatakiwa kuwa unaufanyia mazoezi mkono kwa kuzungusha bega na wrist (maana alikuwa amevaa lile lifuko ili kuupa support mkono usiwe na movement sana na kusaidia uvimbe kupungua.) Akaendelea kuongea mama usijali utapona tuu pole sana hapo inabidi upate matibabu mazuri you should get good treatment mama maana na mimi mama yangu alipata tatizo la kuteguka mkono na umri wake ni kama wewe na sasa hivi yuko safi kabisa. Muda wote huo anaongea hayo tunamtazama tuu na kumsikiliza akaona kama hatumuelewi mi nikamwambia kuwa mama hajateguka mkono umevunjika akasema hapo atafanyiwa operation na watamuwekea vyuma, mie nikamwambia anawekewa vyuma kama zile antenna akasema hapana anawekewa vyuma kwa ndani vinashikilia mifupa hiyo miwili sasa hapo akaanza kuongelea na terminology za kidaktari tukawa tunamsikiliza na kumuitikia tuu hata sielewi. Akasema mimi nina ujuzi wa matatizo hayo ya maifupa na mimi niishapata ajali ya gari nikavunjika mguu nilifanyiwa operation na nimewekewa vyuma todate niko vizuri sema nilifanyiwa operation London. Mama wewe usiogope hapo wakikuwekea vyuma utapona vizuri tuu you should be in good hands for better treatment
Akahisi hatumuamini akasogea karibu na kiti changu na kunishika mkono bila kujielewa akapandisha mkono wa shati lake kisha akanishikisha mkono wangu juu ya wrist na chini ya bega idogo amewekewa nuts kushikilia mifupa. He made me go through his arm and I was like just puzzled sielewi ni nini kinaendelea.
Kawaida yangu watu wananiambiaga huwa ninaringa sana so mtu ambaye simjui simsalimii na ikitokea salamu basi itaishia hapo siendelezi maongezi au mtu akinilazimisha kuongea najikausha kama simsikii au simuoni ila kwa jana was tofauti. Huyu kaka kwa mtazamo wa haraka haraka si handsome ila sauti, the way he speaks, the way he moves without barriers ilinifanya nimtazame kwa jicho la tofauti. Kumbuka hatujui na wala hatumjui .
Ikaendelea akasema wacha niwape mtu pale Muhimbili atawasaidia na mtapata huduma nzuri na huyu dokta kikawaida kumpata sio rahisi maana anafoleni sana na ni expert wa mambo ya mifupa. Akatoka kwenda kuchukua simu aliporudi akampigia huyo dokta na akaweka loud speaker. Akamwambia dokta nina rafiki yangu wa karibu nilisoma nae uingereza (akimaanisha mimi) mama yake amevunjika mkono na umri wake ni mkubwa hivo naomba msaada wako wafike hapo Muhimbili umsaidie mama apate matibabu mazuri, is it ok nikimpa namba yako akifika hapo akupigie, yule dokta akajibu sawa wape akasisitiza chukua hii namba umpigie huyu dokta you are in good hands na utaniambia mama akimaliza operation atarudi Tanga akiwa health and happy huku kabeba ndoo ya lita 10 ya mafuta mkononi.
Mimi naishi UK naelewa umuhimu wa matibabu hasa kwa watu wazima na ntafurahi mama akipata matibabu sahihi. OK ngoja niwaache, haya mama mbaki salama akampa mkono mama akanigeukia mimi na kuniambia bye.
Tukabaki na mama tunatizamana hatuelewi je huyu ni malaika? Ni mtu tuu amekuja? Ni daktari kweli? Why aje kwetu na aoneshe msaada wakati hatujui, ni kawaida yake kusaidia watu au imetokea kwetu tuu? Mama amefurahi maana alikuwa anaogopa kukatwa mkono.
Baada ya kumrudisha mama home nikarudi zangu Bagamoyo, whole night was thinking about this Doctor, his good name is Zurich hadi sasa I hear his voice in my brain.
Zurich wherever you are Kasie admires you.
NB: Ikikushinda kusoma pole endelea na nyingine, ikikuboa pole ipotezee, ikikuudhi msamehe Kasie buree maana she is the way she is.
Good day good peoples.
Kasie.