kama ingekua ni mipango ya lowassa isingekuja kidizain hii.maana inawalenga wagonjwa tu.
kweli ruhumbuka alisema mengi ila hili la loliondo wala halijatabiliwa na mwanafalsafa. ni nyakati tu kama zilivyokua za nuhu,luthu na hata kipindi cha farao.
Kama ikiwa huyo Mzee wa Umasaaini huko Lolindo ni Mganga wa EL na kuwa kila atakaye kunywa hayo maji yake 2015 huta mwambia lolote juu ya EL, basi tumeliwa tena tuhesabu 2025.
Napata mashaka makubwa juu ya taarifa zake, napata shida kwanini wizara ya afya haitoi tamko lolote. Kwanini wizara ya afya wasipereke wataalam wao na wagonjwa ili kupata sample za wagonjwa waliopona kwa ajili ya kutoa taarifa elekezi? kwanini serikali imelala!
Niliwai kusoma kitabu cha Prof.Gabriel Ruhumbuka; Janga kuu la Wazawa, ambaye hajakisoma akitafute, ni riwaya ilitumika sana katika Vyuo vikuu mbali mbali Amerika na nadhani pia ni miongoni mwa vitabu teule Tanzania. Mambo yote yanayofanyika hapa Tanzania mengi yake Ruhumbuka alikwisha yaona katika riwaya. mtunzi anaongelea Ushirikina na madhara yake akitumia Tanzania kama jukwaa la kufikisha ujumbe, utakuta mauhaji kwa imani za kishirikina kama yale ya Albino yalikwisha andikwa na huyu mwana falsafa wa kitanzania, alikuwa UDSM 1970 hadi 1985 kabla ya kuamia USA.
Siyo kwamba napinga kuwa huyo mzee hana dawa, hapana na uliza kwanini serikali haitoi tamko elekezi kutoka wizara husika ya Afya? ilitujue watu wetu wanaomiminika huko Loliondo kupewa maji wapo salama!
Hili swala linavyotolewa maelezo si la kiimani tena, maana ukisha kuvuka kuponyesha kwa maombi ukaanza kutoa dozi iwe ya maji au vidonge tayari hiyo siyo Kuponyesha kwa imani ni kuponyesha kwa tiba asilia, kwa kweli hapo siyo imani peke yake.
Hisije ikawa kama 1995 kila aliyewai kupita na basi Chalinze hata kama alikuwa mwanao na Mkeo hawakuwa wanashikika wakisikia jina la Kikwete; ulikuwa ukiwahoji Uwezo wa Kikwete wanataka kukupiga, mimi nilikuwa nampinga kidogo nipigwe risasi na rafiki wa karibu sana. Baadaye yalioyoongelewa Mungu ndio anajua, leo hadi wakina Yahya wanatangaza agharani kuwa wanamlinda raisi kwa ushirikina, leo Ikulu imejaa waganga kutoka Tanga na matunguli, UWT haipangi ulinzi wa Rais tena, inapangwa na Waganga na wachawi.
Kumbukeni ya Kibwetele na ya Makanisa yalioibuka kama uyoga na baade kushiriki biashara ya unga hasa mikoa ya Mbeya, Iringa na Dar es Salaam.
hahaaaaaaaaa haiwahitokea.
Vipi na wanaochekacheka kama huyu wanatibiwa? Maana anachekacheka kama leader flani hapa nchini. Loh!!
Mkuu Umenena vyema. Tatizo ni kwamba Serikali yetu imekaa kishabiki shabiki kwenye kila jambo. Usishangae ukienda Ofisini kwa Waziri husika ukaambiwa kuwa naye amefuata dawa Loliondo. Isitoshe nimesikia kuwa kuna hata wakubwa wa Serikali wanaenda huko. Nao wanafuata dawa eti!! Binafsi nimekuwa najiuliza swali kama lako, kwa nini Serikali, kupitia wizara ya AFya isifuatilie na kisha kuweka utaratibu mzuri wa watu kupata hiyo huduma na wakati huo huo kufanya mpango wa kuepusha tabu wanazozipata wagonjwa wanaoenda Loliondo? Manake kwa jinsi nilivyouona msururu unaoelekea kule ni dhairi kuwa kunakuwepo na scrambling kubwa sana ili kuweza "Kupata dawa".
Kwa mfano, kama wangeweza kufuatilia na kufanya uchunguzi kama ulivyoshauri, wakiridhishwa na matokeo yake wanaweza kumleta huyo mganga Arusha mjini na akajengewa mazingira ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na akihitaji kuzifuata dawa zake basi anapewa usafiri maalum kwenda Porini na kurudi Arusha ambako ingewawia rahisi na salama "wateja" wake kumpata.
Anyway, Serikali yetu ina mapungufu mengi sana yanayochangiwa na uzembe,, hii ni sehemu ndogo tu ya mapungufu yao....