Kwa hali ilivo Anza kuzoe maumivu utakua muhanga muda wote wa maisha yako hauwezi kujiamini!! Kuanza upya si ujinga! Bora Angekua rafiki ila ndugu kabisa utakosa Amani'
dah pole kijana ukajua umepata kumbe umepatikana!! But kaa nae ujaribu kumueleza ukweli na ana msimamamo gani kwako maana unaweza ukasema anakupenda kumbe anaempenda zaidi ni uncle
Bwana mtaraji kuoa kama unampenda mchumba wako mwelezee ukweli na endelea na mipango yenu ya kuoana. Mimi imani yangu ni kuwa kila mtu ana PAST yake; sio wote tulioa/kuolewa tumekutana bila kuwa na mahusiano sehemu nyingine. Kwani hawa wake/waumme zetu hawana ex wao??? Na hiyo bado haijazuia watu kuoana.
Mkiamua kuoana mwambie na uncle wako AACHE MAWAZO YAKE YA KUENDELEA na uhusiano na huyo mdada kwakuwa sasa ni MCHUMBA WAKO!!!!
ni kweli kabisa af kikianza kuwa dhahabu kwa uncle huku kwa mhusika kinafifia guess what...................kujilipua,kulipuliwa,tindikali,kukatana makoromeo,makorodani,kuchinjana ndivyo vitakavyo husika kwa wakati huo,huyu kaka bora amteme tu huyu demu maana huko mbele ni majanga zaidi ya majanga
Kwanza nampongeza huyu dada ni mwaminifu na muwazi sana ila sidhani kama ndoa yako itakuwa na HESHMA mbele ya nduguzo jamaa hata marafiki pale mahusiano waliyokuwa nayo mpenzi wako na uncle wako yatakapobainika!
Cha kufanya ni kumuita uncle wako ukiwa na bibie humfahamishe huyo ndiyo mkeo na upime mwenyewe kwa mda kama atamuheshimu na kukaa mbali naye, na je nduguzo watalichukuliaje kama watafahamu!! maana unaweza kumchukua dada wa watu baadae akafanyiwa vurugu na NDUGUZO.