Lodilofa na majibu yake....

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
kila nikikumbuka vituko vya lodilofa huwa nacheka...kimojawapo ni hiki hapa...akiwa ndani ya kigari chake alisimamishwa na traffic wa kike...maongezi yalikuwa hivi....
TRAFFIC; Washa indicator..
LODILOFA; Lete kona
T: washa taa
L; lete giza
T; Mbona unanichezea hivyo?
L: Hata sijakushika unasema nakuchezea, nikikushika si utasema nimekubaka? Lodilofa aliwasha kigari chake na kumuachia vumbi traffic,..je majibu gani unayakumbuka ya huyu jamaa?
 
jarida la sani enzi zile kabla ya kuanza kutoka kama gazeti lilikua bomba sana.
 
Me nakumbuka hki...
Mzee tambi alienda kumtembelea lodilofa...
Tambi: aah..! Mzee mwenzangu nmekuja kukutembelea bwana..
Lodilofa: kwenda zako huko unanitembelea mimi ni miguu yako?
 
kila nikikumbuka vituko vya lodilofa huwa nacheka...kimojawapo ni hiki hapa...akiwa ndani ya kigari chake alisimamishwa na traffic wa kike...maongezi yalikuwa hivi....
TRAFFIC; Washa indicator..
LODILOFA; Lete kona
T: washa taa
L; lete giza
T; Mbona unanichezea hivyo?
L: Hata sijakushika unasema nakuchezea, nikikushika si utasema nimekubaka? Lodilofa aliwasha kigari chake na kumuachia vumbi traffic,..je majibu gani unayakumbuka ya huyu jamaa?

ngoja kidogo...................inapakia.........
 
Lord lofa alikwenda hospital. Dr. Akamuuliza: unaendesha? Akajibu ndiyo, naendesha kile kigari kidogo
 
Jamaa>naomba lift
Lodilofa>mimi sina lift ningekuwa nayo ningekupa
Jamaa>sina maana hiyo yaani naomba nipande gari yako..
Lodilofa>pumbaf...umeona gari yangu ni mahindi au maharage mpaka upande shambani..!?HUKU AKIWASHA GARI NA KUONDOKA SPEED AKIMUACHIA JAMAA VUMBI.
nilikuwa namkubali sana Ndondocha wa tabasamu kama kuna anayekumbuka kituko chake akitoe jamani.
 
hahahhhah jamani msinikumbushe vile vibonzo vya zamani nilikua naipenda sana Sunche na Kapeto. siku hizi hv hamnaga hizo???????
 
Jamaa>naomba lift
Lodilofa>mimi sina lift ningekuwa nayo ningekupa
Jamaa>sina maana hiyo yaani naomba nipande gari yako..
Lodilofa>pumbaf...umeona gari yangu ni mahindi au maharage mpaka upande shambani..!?HUKU AKIWASHA GARI NA KUONDOKA SPEED AKIMUACHIA JAMAA VUMBI.
nilikuwa namkubali sana Ndondocha wa tabasamu kama kuna anayekumbuka kituko chake akitoe jamani.

Kituko cha ndondocha kwenye mazishi.
Msemaji: Poleni sana ndugu wafiwa, sasa kama ilivyo kwa utamaduni wetu mtu akifa lazima apatikane mtu wa kumsindikiza (Akimaanisha azikwe pamoja na marehemu)
Waombolezaji: Ndio..
Ndondocha: Kweli kabisaaa, lazima tudumishe mila, sasa tutampataje huyo mtu?
Msemaji: Wanandugu watapiga kura.
Waombolezaji: Uamuzi wa busara. (Wakapiga kura)
Msemaji: Nashukuru sana, tumeshampata msindikizaji, mtu aliyepigiwa kura nyingi ni Ndugu Ndondocha, hivyo tunaomba usogee karibu na kaburi hapa ili tumalize haraka.
Ndondocha: (Huku akiwa na hasira..) Jamani basi naombeni mniruhusu nikaage familia yangu, nipeni dakika 15 tu tena na ulinzi kama hamniamini.
Waombolezaji: Sawaaa
Ndondocha kaenda nyumbani akakusanya jeshi lake (Mwanae KIOKOTE na mbwa kama laki mbili hivi pamoja na Anko wake KAISI jamaa anapiga vichwa balaa)
Kilichotokea nafikiri msomaji unaweza malizia..

I miss NDONDOCHA
 
Kuna vituko 2 navikumbka,kimoja ni cha Lodilofa na Kingine madenge.Nianze na cha Madenge.Baba yake kamuuliza "Madenge 2x2ni ngapi"Madenge kajibu ni 4,Baba yake akamsifia sana na akamuuliza,"Haya mwanangu,umepataje hiyo4"? Madenge kajibu,"Mwaego baba nilikuwa nakudanganya"! Kingine Lodilofa kahudhuria mechi ya mpira wa miguu kwa mara ya kwanza Akatoka uwanjani mbio na kigari chake mara akarudi kwa jazba ikwa amejaza mipira 22 katika gari na kuimwaga uwanjani huku akifoka,"Acheni ulofa wenu hapa,watu22 mnagombea mpira mmoja tu! Haya sasa kila mtu acheze wake!"
 
Thanks bana kwa kukumbushia enzi izo walau unatufariji na hali ngumu ya maisha inayosababishwa na hawa magamba na mafisadi wao
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom