Lodge na Guest House nzuri Mwanza

jembelamkono

JF-Expert Member
Nov 19, 2015
2,733
2,011
Wakuu naombwa kujuzwa lodge au guest house nzuri kwa maeneo ya Mwanza mjini.
Isiwe mbali sana na mjini au iwe inafikika kirahisi kwa maana ya kutoka au kuelekea mjini.
Ni vyema kama ningejulishwa na bei na huduma husika.
Wasalaam.
 
kuna lodge inaitwa lesa garden ipo malimbe huto juta kufika bei yake ni kuanzia 30 mpaka 50 na utapata msosi wa uhakika. au kuna nyingine inaitwa samanene nayo ipo malimbe nayo hutojuta
 
Ipo moja mdau katikati town tsh 15000 self inaitwa Hotel Intercity.Ipo mtaa wa kaluta karibu nastend ya zamani ya Tanganyika.Namba hii mdau 0688092160,paka pazuri.Mi nikitimba rockcity ndio mahali pangu hapo.
 
kuna lodge inaitwa lesa garden ipo malimbe huto juta kufika bei yake ni kuanzia 30 mpaka 50 na utapata msosi wa uhakika. au kuna nyingine inaitwa samanene nayo ipo malimbe nayo hutojuta
Mkuu kutoka mjini kwenda malimbe kwa tax ni kama kiasi gani?au mwendo wa muda gani?
 
Mkuu haujaweka bajeti yako lakini ngoja nikusaidie. Pale kona ya Bwiru kuna MS Hotel ni pazuri. Iko barabarani na jirani kuna Diamond Pub ambapo pako decent sana kwa kupotezea muda. Bei za room zao ni 25,000/= (namba zao ni 0766013809 na 0762478500), Jirani kuna Hotel Kingdom iliyo mtaa wa Ghana (40,000), Pale Nera kuna Oliver Hotel (30,000/=), Mtaa wa Kaluta kuna Holmand Hotel (sikumbuki vizuri nadhani rate ni 35,000/= au 40,000/= na ni pazuri sana. Namba zao ni 0754542277, 0682163739), Planet lodge ipo Ghana na bei zao ni 30,000/=. Pale Nyegezi karibu kabisa na stand ya mabasi kuna Cosmopolitan Hotel bei zao ni around 30,000 bahati mbaya contacts ziko mbali kidogo. Mtaa wa Rufiji kuna The Pigeon Hotel (0753095087) na pale mjini kuna Gold Crest iliyo jirani na New Mwanza hotel. Rate zao hao Gold Crest ni around 120,000/= per night. Kazi kwako mkuu.
 
Ipo moja mdau katikati town tsh 15000 self inaitwa Hotel Intercity.Ipo mtaa wa kaluta karibu nastend ya zamani ya Tanganyika.Namba hii mdau 0688092160,paka pazuri.Mi nikitimba rockcity ndio mahali pangu hapo.
Ninaingia Mwanza kesho ni kweli hii lodge nzuri na ipo karibu na City Center.Maana kuna kusanyiko pale MWANZA CC HALL.

Sent from my HUAWEI Y330-U11 using JamiiForums mobile app
 
Duh! huu uzi unanihusu kabisa, mi naulizia mitaa ya Nyegezi, bajeti yangu ni sh 20000 mpaka 25000, nikipata na contact ntashukuru sana

Kuna moja inaitwa Pentagon karibu na ilipokuwa ofisi ya Scandinavia Bus, nadhani rates zao ni 25 - 30 Kilos, ipo nyingine mtaa huohuo inaitwa Isami kama sijakosea sana nilifika siku nyingi kidogo ni nzuri sana, generally speaking Lodge nyingi za Mwanza wapo juu sana katika ukarimu na huduma kwa ujumla
 
Kuna Victoria Annox ipo karibu na kiwanja cha furahisha bei 25000 tu unapta huduma ya kuliwa bure tea ya asubuhi ni self service, chakula jioni ni buffet type masamaki au kuku wa kutosha huduma ya chakula ni 6000 tu lakini msosi wa nguvu hutajutia hela yako pia ipo karibu na villa park hapo kajionee burdan mwenyewe nk
 
Uwaombe radhi wenye hotel kwa kuwaharibia biashara yao. Unamaanisha nini unaposema kwamba mteja anapata huduma ya KULIWA BURE?
 
Nyegezi naona cosmopolitani wako vizuri zaidi ila sema mara nyingine kuna kuwa na walevi hadi usiku mwingi hapo Inakuwa mbaya sema huduma zao ni za kichangamfu sana na ulinzi wa hali nzuri
 
Duh! huu uzi unanihusu kabisa, mi naulizia mitaa ya Nyegezi, bajeti yangu ni sh 20000 mpaka 25000, nikipata na contact ntashukuru sana

nenda kumalija hapo karibu na ofisi za dar lux vyumba ni kuanzi 12000 ambacho siyo selfu na 15000 kwa 20000 ambavyo ni self ila ni bila chai ya asubuhi
 
Back
Top Bottom