nimekuelewa na umeeleza vizuri, ninachokisema mimi ni double standards za hawa waleta lockdown. Pamoja na Lockdown jamaa waliendelea kufanya kazi na kutuuzia bidhaa zao, mpaka sasa nchi zetu za Africa hatuna tunachouza huko kwao zaidi ya madini. Tungeweka lockdown si tungetawaliwa zaidi? na hili la kuuza chanjo kwa faida kubwa nalo ni njia ya kutudidimiza, kwasababu shughuli haziendi kutokana na ugonjwa lakini mtu anataka umpe sehemu ya bajeti yako ili akupe chanjo.
Ngoja nichangie kwa kutoa mfano huu ambao ninautumia kama 'illustration'. Unatoka kwenye kitabu kinachoitwa 'The Bird's Song' by Anthony de Mello (SJ). Kicha cha habari ni 'THE DISABLED FOX'. Stori inaenda hivi: A fable of the Arab mystic Sadi: A man walking through the forest saw a fox that had lost its legs and wondered how it lived. Then he saw a tiger come with game in its mouth. The tiger had his fill and left the rest for the fox. The next day too God sent, the tiger to feed the fox.
The man began to wonder at God’s greatness and thought. “I too shall lie in a corner trusting the Lord to give me all I need.” He did this for a month, and was almost at death’s door when he heard a voice that said, “O you who are on the path of error, open your eyes to the truth! Imitate the tiger not the fox.” On the street I saw a naked child, hungry and shivering in the cold. I became angry and said to God, “Why do you allow this? Why don’t you do something?” God did not reply. That night he said, quite sudden-ly, “I certainly did something. I made you.” Ukisoma stori hii kwa makini na ukilinganisha na ambavyo mataifa yetu ya Afrika yalivyo utagundua kwamba 'almost always' sisi tumekuwa 'fox' kama hadithi hii inavyosema.
Hatufanyi lolote na tunasubiri mataifa mengine yatufanyie na yakifanya kwa jinsi tusivyopenda tunayalalamikia. Miaka nenda rudi viongozi wetu wamekuwa wakisafiri nchi mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali. Ukiondoa mbinu za kivita (ambavyo kwa mtazamo wangu ndilo eneo pekee tunalojifunza na kuja kufanya huku kwetu) maeneo mengine naweza kusema hatujaweza kujifunza na kufanya kitu kinachoonekana kama sisi. Kwenye dunia ya sasa binadamu wote tumekuwa kama wanyama wawindaji - nguvu, mbinu za kuwinda na mbio tulizonazo - ndivyo vitakavyotuokoa kutoliwa na wanyama wengine. Otherwise, tutabaki watu wa kulalamika. Angalia hata hapa kwetu - kama kuna magari mengi kwenda Gongo la Mboto, ukisafiri kutoka Tazara utaenda kwa Sh400. Kama kuna magari machache, kuna daladala zitapakia kwa Sh1,000, bajaji 1,500 au Sh2,000 na pikipiki Sh3,000.
Nadhani unakumbuka kanuni ya 'supply' na 'demand'. Kwa kifupi, wakati wa shida ndiyo pia wakati wafanyabiashara wanapata faida zaidi na huwezi kuwalaumu kwa sababu kama shida hakuna hata wao wanauza kwa bei ya kutupa. Uzalishaji wa nyanya au vitunguu ukiwa mwingi utanunua kwa bei ya kutupa, lakini zikiadimika itabidi ujikune kichwa. Makampuni yanayotengeneza dawa pia yanafuata kanuni hii ya 'supply' na 'demand' . Solution ni nini? Tusiwe kama 'fox', tumwige 'tiger' kwenye stori. Tuwekeze kwenye utafiti na matokeo yake yafanyiwe kazi na mamlaka husika na taratibu taratibu na sisi tutakuwa na mchango mkubwa kwa dunia na tutakuwa na uwezo mkubwa wa bargain' kibiashara kwa sababu na sisi tunajua tutawashika wanaotupandishia bei au wanaotuuzia bidhaa feki.