Livingstone Lusinde, Mbunge mwongo asiye na haya!

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,252
8,003
Huyu mbunge anajaribu kusimama bungeni eti anadai kua kuna wabunge wa UKAWA walioko nje ya bunge,wanakutana kwenye chai huku wakimtuma yeye ati awasemee bungeni! Hivi huyu mbunge anaweza kumsemea nani? Kuna mbunge gani ndani ya UKAWA anaweza kujitoa akili amtume mtu kama Lusinde amsemee bungeni? Kwa kipi labda? Maana tangu aingie bungeni yeye anajua kuongelea matusi tu.


Kwanini Lusinde haoni haya kusema maneno mengi kwa kukaukiwa mate mdomoni sijue kua yeye siku zote hupuuzwa? Angesema hata jina la mbunge mmoja basi athibitishe kweli kua hua anatumwa! Mtu mzima kutokwa mishipa kuongelea kitu usichothibitisha ni unafki na uongo uliokubuhu.


Mtu kama Lusinde hata shule hana ni darasa la saba pure kama yule wa Geita vijijini watasema nini sasa bungeni? Eti hawa nao ni watunga sheria maskini! Hiki ni kishibitisho kua muhimili wa bunge unazidi kukosa hadhi yake ya kipekee kwa kuingiliwa na baadhi ya watu mizigo.
 
Natani hii comment yangu iwe ya mwisho, kumuongelea Lusinde hapa ni kupoteza muda na kujiweka kwenye level yake ya ukilaza........
 
Kumuanzishia Lusinde au yule dogo wa Ulanga, Sugu, Kubenea au Musukuma thread ni kukosa kazi... Mkapa kawaweka sehemu yao very well today
 
Alikuwa anatafuta kick tu kupitia Ukawa, maana hakuna mbunge hata mmoja kupitia Ukawa anaweza kumsemea mule bungeni, kwani uwezo huo wa kujenga hoja tofauti na udaku, unafiki, na kila aina ya upuuzi hana
 
wakati utaongea wenyewe,wakati ni zaidi ya maneno ya lusinde wakati ndio utatoa mjumuisho wa wanayofikiria wabunge wa ukawa kwa sasa kwa kitendo wanachofanya kama ni cha kushinikizwa na mbowe au ni maamuzi yao kutoka mioyoni................
 
Ccm wamemtuma, Mbowe kachukua taa zake.Ccm hawaoni tena pa kusoma na cha kusoma.
 
Neno KILAZA naona limetumika humu pia.Hili neno limetokana na neno gani...je ni kiswahili sanifu....je ni tusi .....Nisaidieni
 
Mbona Mbowe hana shule anaongoza kundi lile lote? Acha kuona upande mmoja. Sugu, Lema, na mababie wote.
Mtu kama Lusinde hata shule hana ni darasa la saba pure kama yule wa Geita vijijini watasema nini sasa bungeni? Eti hawa nao ni watunga sheria maskini! Hiki ni kishibitisho kua muhimili wa bunge unazidi kukosa hadhi yake ya kipekee kwa kuingiliwa na baadhi ya watu mizigo.
 
Bora Hawa wanatoa hoja zenye mshiko huyo lusinde hamkuti lema Hata kidogo. Ni hoja gan nzito ameshawah kutoa bungen .
Hakuna hoja kwa mtu asiye na elimu. Ni Tanzania tu ndo tumebaki tunachagua watu kujaza viti vya bunge. Wenzetu wanaleta watu wenye uelewa na falsafa tofauti.

Mtu anaongea maneno 10 matano ni kejeli huyo si mbunge.
 
Hii mibunge mingine mzigo tu kwa taifa huyu anasema katumwa na wabunge wa ukawa eti awasemee huko bungeni sijui ni lini walimpigia kura hajui badala ya kutumwa na wananchi wake eti katumwa na ukawa na posho anachukua na kujisifu kafanya kazi ya kuishauri serikali huu nao ni ufisadi wa kodi za watanzania ni bora wangelipwa kutokana na uzito wa hoja zao na sio mtu anachangia uharo alafu anaenda kuchukua posho
 
Back
Top Bottom