Livingston Lusinde amkejeli Zitto

Livingston Lusinde amkejeli Zitto

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,579
Reaction score
161,431
11081325_10202757683221927_5066445753323452524_n.jpg
 
Wana CCM wanajua kucheza na mindset za watu kwelikweli.Siku zote hizo Huyu Lusinde hakujua kama ACT ni chama cha Zitto.? Anapotoka CDM hajui kuwa angeelekea chama gani..

By the way,anajifanya eti hajui Zitto atapata wapi pesa za kuendesha chama. Duuu...kweli Tz safari ya demokrasia isiyo na sarakasi kama hizi tunayo.
 
Mbunge wa Mtera-CCM,Livingstone Lusinde aka Kibajaji amemkejeli mwanachama mpya wa ACT-Tanzania,Zitto Kabwe kwa kumuambia kuwa amepotea. Lusinde amesema kuwa kitendo cha Zitto kuhamia ACT badala ya CCM ni kupotea kisiasa na kufuata umaskini.

Lusinde amemtaka Zitto kujiandaa kuiendesha ACT kwa pesa zake. Pia,amemkejeli kwa kumuuliza kwanini amehamia usiku-alikuwa anaroga? Lusinde aliwahi kumshukuru Zitto kwa kuiachia CCM Jimbo la Kigoma Kaskazini.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Katika wabunge ccm waliobugi ni lusinde, jamaa mweupe kabisa mbona deo sanga si msomi lakini ana akili na kafanya makubwa makambako , huyu lusinde hakuna alichofanya Mtera, Tutampigia kampeni LE MUTUZ alichukue hilo jimbo, Lusinde ana mambo ya kitoto sana
 
Kwa hiyo hoja za Lusinde kwa sasa mnaziona zina maana.

Kila siku mlikuwa mnasema hana hoja, leo kwa vile ameongea hoja inayokoleza matamanio yenu, kwa sasa anaheshimika.

Naona kwa sasa mnakosa mpaka usingizi hapo Ufipa.

Shughulikeni na maisha yenu ya kisiasa hapo Ufipa.

Maisha na Siasa za Zitto mwachieni Zitto.
 
Andika vya maana kijana

MTT
 
Sasa angetaka amsifie ZZK kuhamia ACT? He is quite right, CCM na ACT ni Vitu viwili tofauti.
 
Kwa hiyo hoja za Lusinde kwa sasa mnaziona zina maana.

Kila siku mlikuwa mnasema hana hoja, leo kwa vile ameongea hoja inayokoleza matamanio yenu, kwa sasa anaheshimika.

Naona kwa sasa mnakosa mpaka usingizi hapo Ufipa.

Shughulikeni na maisha yenu ya kisiasa hapo Ufipa.

Maisha na Siasa za Zitto mwachieni Zitto.

ZZK anawasumbua sana CDM maana kila kitu ZZK
 
katika wabunge ccm waliobugi ni lusinde, jamaa mweupe kabisa mbona deo sanga si msomi lakini ana akili na kafanya makubwa makambako , huyu lusinde hakuna alichofanya mtera, tutampigia kampeni le mutuz alichukue hilo jimbo, lusinde ana mambo ya kitoto sana

hizo ndio sampuli za wabunge wenu....na huo mbadala inadhihirisha uwezo wako wa kufikiri ulipofikia..
 
lusinde huwa anapenda kumwambia zitto ukweli
 
Kwa hiyo hoja za Lusinde kwa sasa mnaziona zina maana.

Kila siku mlikuwa mnasema hana hoja, leo kwa vile ameongea hoja inayokoleza matamanio yenu, kwa sasa anaheshimika.

Naona kwa sasa mnakosa mpaka usingizi hapo Ufipa.

Shughulikeni na maisha yenu ya kisiasa hapo Ufipa.

Maisha na Siasa za Zitto mwachieni Zitto.

Wewe nadhani umeandika ukiwa usingizini. Tazama umekuwa wa pili kuchangia hii thread, sasa umemjibu nani? Maana sioni hoja iliyokutangulia ikisema Lusinde ni wa maana. Mbaya zaidi unasema masuala ya ufipa, ulikuwa ukimjibu nani? tafakari kijana kabla ya kufanya jambo lolote sivyo unadhihirisha ukilaza wako.
 
Ndo utajua wanasiasa wanawaza nini vichwani mwao.

Siasa Ni ujasiliamali tu kama ujasiliamali mwingine, watu wanawaza kupiga pesa tu.

Kutegemea eti chama fulani kinapigania ustawi wa raia ni kujipumbaza tu.
 
Lusinde ampa ukweli Zitto watu wanadhani kujenga chama cha siasa ni kazi rahisi sana Zitto ameenda kujimaliza kisiasa huko ACT.
 
Katika wabunge ccm waliobugi ni lusinde, jamaa mweupe kabisa mbona deo sanga si msomi lakini ana akili na kafanya makubwa makambako , huyu lusinde hakuna alichofanya Mtera, Tutampigia kampeni LE MUTUZ alichukue hilo jimbo, Lusinde ana mambo ya kitoto sana
LE MUTUZ labda akagombee ubunge chalinze huko mtera wananchi wameshachoka kuongozwa na mbunge wa ccm .hilo ni jimbo la chadema wala CCM msihangaike.
 
Kwa hiyo hoja za Lusinde kwa sasa mnaziona zina maana. Kila siku mlikuwa mnasema hana hoja, leo kwa vile ameongea hoja inayokoleza matamanio yenu, kwa sasa anaheshimika.
Kwa hiyo wewe leo unaona hoja za Lusinde hazina maana? Kila siku ulikuwa unasema ana hoja nzuri, leo kwa vile kaongea hoja inayopingana na matamanio yako, kwa sasa unamdharau?
 
Wahenga walisema "Aliyezoea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi" hatumshangai huyu mbumbumbu Kwani kama ni umaridadi wa kusema hata kasuku huwa anaongea.
 
Lusinde sio chizi ila nimegundua kua anayoyafanya hua anafanya kwa makusudi. Kibajaj amemsih vzr sana Zzk
 
Back
Top Bottom