LIVE updates: Taifa Stars vs Bafana Bafana

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
TIMU ya soka ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, leo inakutana na kipimo kingine wakati itakapoivaa Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni.

Licha ya kuwa Bafana Bafana haitakuwa na nyota wake mbalimbali wanaocheza Ulaya, akiwamo Steven Peenar, Bafana Bafana pia itawakosa wachezaji wa Orlando Pirates akiwamo mshambuliaji Thlou Segoleta na kiungo Andile Jali, ambao watakuwa na kibarua cha kuichezea klabu yao katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la Nedbank leo.

Nyota pekee wa Bafana Bafana anayecheza Ulaya atakayekuwamo leo ni Bernard Parker ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Uturuki, ambapo ligi kuu nchini humo imeshamalizika na mchezaji huyo kurejea nyumbani kwa mapumziko.

Mchezo huo ni kipimo kizuri kwa timu zote, ambapo Bafana Bafana na Stars zote zina mechi ngumu ugenini za mchujo kusaka tiketi za fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) zitakazofanyika mwakani Equatorial Guinea na Gabon.

Haya tena mliopo uwanjani tupeni updates na je TV gani inaonyesha live mechi hii?
 
kwanini kuna sehemu mbili za Stars vs Bafanabafana? Ingekuwa poa kabla mtu ajaanzisha thread asome kuona kama aipo, ni rahisi sana , inatakiwa kusoma post za leo( new posts) kama aiko ndo uanzishe.
 
Mechi inaonyeshwa live Stars TV mkombozi wetu sijui hii TBC1 kAzi yake nini inashindwa kuonyesha matukio ya kitaifa kama game hii ya leo??
 
Hivi kama unataka kupata update za hapa hapa kwenye hii forum unafanyeje? Mana mie siku zote uwa natumia refresh button ya website, je kuna njia cheap zaidi ya hiyo?
 
Leo Stars ikishinda nitakuwa na confidence kuwa hata C.A.F wataishinda kwao, vinginevyo wasiwasi juu yao itakuwa mkubwa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom