live updates.SIMBA VS RUVU SHOOTING

Mkuu vipi? Mnyama mwakani ni mechi za "mchangani", na professionals wazuri wote tunakomba! Hawawezi kucheza mechi za "mchangani" miaka miwili. Itabidi mnyama abadili fani! Achana na mpira, endeleza kilimo. Si tayari mna shamba Bunju?

Ligi Bado Mbichi Chochote Kinaweza Kutokea Tuna Matumaini Bado
 
Ligi Bado Mbichi Chochote Kinaweza Kutokea Tuna Matumaini Bado

Mkuu, hayo ni mambo ya utani! Ila kazi mnayo. Angalia mechi zilizosalia zilivyokaa, za ugenini na nyumbani. Simba inabidi mjipange myakabili hayo matatizo yenu soberly. Kinachowaponza ni kufikiria fitna, mara oh tuwape sapoti Azam Yanga asichukue ubingwa. Hayo ni mambo ya kizamani sana, hayawasaidia hata kidogo. Mtamsaidia Azam ataishia kuchukua nafasi ya pili, nyie mtabakia mchangani. Wachezaji bora wataondoka tu. Kwa nini waendelee kukosa mechi za kimataifa misimu kadhaa mfululizo? Umenipata mtani? Tuition ya bure hiyo!!
 
Masao Bwire amezungumza kwa machungu amekubali kipigo cha leo huku akidai kuwa kipigo cha Yanga ni cha aina yake kinachowanyong'onyesha kila wakikikumbuka, loo, Yanga noma. Amewaomba mashabiki wao wasikate tamaa.
 

Asante kwa historia ndefu, sasa zungumzia ung'oaji viti huku mkijua hakuna wa kupigwa faini kwani klabu yenu ilikuwa haichezi. Badala ya kufurahia ushindi wa timu ya Tanzania mkakasirika hadi kung'oa viti. TFF imekula kwao.
 
Asante kwa historia ndefu, sasa zungumzia ung'oaji viti huku mkijua hakuna wa kupigwa faini kwani klabu yenu ilikuwa haichezi. Badala ya kufurahia ushindi wa timu ya Tanzania mkakasirika hadi kung'oa viti. TFF imekula kwao.
Mkuu hata suala la kung'oa viti halijaanza siku ya Kagera, kuna siku ilikuwa ni mechi ya Simba sijui na timu gani viti viling'olewa pia tena kote kote, washabiki wa upande wa kulia na wale wa upande wa kushoto, Jana pia viti vilianza kung'olewa mapema kabla hata Yanga hawajapata goli na picha zinazoonekana zinaonyesha mashabiki waliovaa nguo nyekundu na wengine wamevaa nguo za rangi ya kijani wameshikilia viti sasa mimi sijui hao ni mashabiki wa timu gani.

Lakini kwa ujumla suala la kung'oa viti ni kukosa ustaarabu, ni sawa na wanafunzi wanapoamua kuharibu mali za shule mimi naona ni utovu wa nidhamu na kukosa heshima, hii tabia inabidi ilaaniwe kwa nguvu zote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…