Live Updates: Kuandama kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
A salaam Alaykum Warahmatullahi Ta'alah Wabarakaatuh..

Leo ni mwezi 29 Shaaban, kama ilivyo mbingu zitafunguka na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kuonekana. Ni matarajio kuwa hapa JamiiForums ni sehemu mojawapo ya kuhabarishana kuhusu taarifa za kuandama kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Kwahivyo popote pale ulipo ukisikia au kuuona mwezi mwandamo ni vema tukajulishana kupitia hapa. Muhimu na lenye kuzingatia ni kuwa na taarifa sahihi.

Nawatakia kila la heri wale wote kwa watakaojaaliwa na wanaojiandaa kwa ajili ya mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhan, Mwenyezi Mungu asikilize dua zetu na kututimizia yote ambayo tumenuia katika mfungo huu, Insha'Allah.

Wabillah Tawfiq

Ramadhan Kareem .
Ramadhan Mubaarak.
Ramadhan Maqubur.
 
Noted

================
UPDATES -16/05/2018.

Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa Mbingu na Ardhi(Nchi) kwa kutujalia tena Afya bora na hatimaye tunaenda kuanza Ibada tukufu ya Mfungo wa Mwezi wa Ramadan.

Wapo wengi walitamani kujumuika katika hii Ibada lakini kwa Mapenzi yake Muumba hawajafanikiwa.

Allah tujalie Afya njema ili tuweze kutekeleza tena Ibada hii muhimu kwa mara nyingine tena
 
Back
Top Bottom