Live! Updates: Brazil vs Spain - Confederations Cup 2013 Final - Leo Jumapili, 30/06/2013

Live! Updates: Brazil vs Spain - Confederations Cup 2013 Final - Leo Jumapili, 30/06/2013

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
=
FIFA_CONFEDERATION_CUP_BRAZIL_2013.jpg

=
Patashika : Kombe la Mabara litaitikisa Dunia leo, timu ya Brazil na Hispania, wanakutana katika mchezo wa fainali ya kombe la mabara.

Brazil imetua kwenye michuano hiyo kwa tiketi ya wenyeji wakati Hispania ipo hapo kwa sababu ni Mabingwa wa Dunia.

"ni mechi ngumu dhidi ya timu ngumu, na ni mechi ya dunia, inazikutanisha timu zote zina rekodi nzuri na wachezaji wazuri"

"Leo ni ufundi tu, hakuna kingine"

RATIBA
MECHI YA KWANZA
KUTAFUTA MSHINDI WA TATU
[Salvador][
SAA 1 USIKU]
Uruguay v Italy
uruguay-vs-italy.png

Mechi ya FAINALI
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
Brazil v Spain
brazil-vs-spain.png
 
BJORN KUIPERS, Refa kutoka Holland, ndie atakaechezesha Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara itakayochezwa leo Jumapili, 30 Juni' 2013, Usiku Uwanja wa Maracana huko Rio De Janeiro kati ya Wenyeji Brazil na Mabingwa wa Dunia Spain.Hii ni Fainali ya pili kubwa Mwaka huu kwa Refa Kuipers, mwenye Miaka 40, kwani pia alichezesha Fainali ya UEFA EUROPA LIGI Mwezi Mei kati ya Chelsea na Benfica.Katika Mechi ya utangulizi ya kusaka Mshindi wa Tatu wa Kombe la Mabara kati ya Italy na Uruguay Refa atakuwa ni kutoka Nchi ya Algeria Djamel Haimoud mwenye Miaka 42.
Refa Haimoud ndie aliteuliwa Refa Bora Afrika Mwezi Desemba 2012 katika Tuzo za CAF.Kwenye Mashindano haya ya Kombe la Mabara Haimoud alichezesha Mechi ya Kundi B Spain ilipoitwanga Haiti.===RATIBA YA LEO YA KOMBE LA MABARAJumapili Juni 30 MSHINDI WA TATU[Salvador][SAA 1 USIKU]Uruguay v Italy FAINALI [Rio De Janeiro][SAA 7 USIKU]Brazil v Spain
 
Presha yapanda Hispania na Brazil
LEO Jumapili Dunia itashuhudia fainali kabambe ya Kombe la Mabara kati ya Hispania na Brazil.
Huku presha za nchi hizo zikiwa juu, kocha wa Hispania, Vicente del Bosque, amesema anachotaka kuona ni wachezaji wake wanapata ubingwa huku akisisitiza hawezi kuvumilia kusikiliza maelezo kuwa wamechoshwa na mechi nyingi mfululizo.
Hispania ambayo ni mabingwa wa Kombe la Dunia, wamefika fainali baada ya kuitandika Italia kwa penalti 7-6 huko Fortaleza juzi Alhamisi.
Sasa Kocha Del Bosque anaamini wachezaji wake wamepumua kwa siku mbili kabla ya kutua kwenye mechi ya fainali.
Wachezaji wa Hispania wamekuwa wakilalamikia joto kali la Brazil na kudai kuwa jambo hilo ndio linafanya wasifunge mabao mengi.
Lakini Del Bosque amesema anaamini mechi ya fainali dhidi ya Brazil kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro itakuwa ya mafanikio.
Kocha huyo amewaambia wachezaji wake wanapaswa kujituma kwenye Uwanja wa Maracana ambapo ilipigwa mechi ya nusu fainali kati ya Brazil na Uruguay na wenyeji walishinda kwa mabao 2-1. "Sitaki kusikia sababu wala visingizio vya aina yoyote," alisema Del Bosque ambaye aliiongoza Hispania kupata ubingwa wa dunia mwaka 2010 na ubingwa wa Ulaya miaka miwili baadaye.
"Ninafahamu wapinzani wetu wamekuwa na muda mrefu wa kupumzika kwa kuwa walicheza nusu fainali Jumatano, lakini na sisi tuna saa 72 za kuvuta pumzi," alisema.
Kwa upande mwingine, kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, amesema timu yake kwa sasa ni nzuri na ana uhakika atawanyoa mabingwa hao wa dunia.
Kocha huyo ambaye ameanza kazi ya kuinoa Brazil miezi saba iliyopita, anaona mwanga mpya kwenye timu yake iliyotwaa ubingwa wa Dunia miaka 11 iliyopita huko Japan.
Brazil imefika fainali baada ya kuzifunga Japan, Mexico, Italia na Uruguay.
SC: M_spoti
 
Kwa hapa kwetu ni kesho kwani si unaanza 7 usiku which 01.00 Am,au nakosea wadau.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Natabiri NEYMAR kuwa mchezaji bora...na BRAZIL kushinda 2-1 dhidi ya mahasimu wake HISPANIA
 
Kwa hapa kwetu ni kesho kwani si unaanza 7 usiku which 01.00 Am,au nakosea wadau.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

RATIBA YA LEO YA KOMBE LA MABARA
Jumapili Juni 30

MSHINDI WA TATU
[Salvador][
SAA 1 USIKU]
Uruguay v Italy

Mechi ya FAINALI
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
Brazil v Spain
 
Mwakani world cup tutapata shida sana saa 7! mechi duh.
 
Hii mechi inachezwa usiku sana,itabidi nilale kwanza ili baadaye niamke.
 
game itakuwa ngumu kwani watataka kombe libaki brazil just waiting hiyo kesho saa saba..
 
Mechi za usiku hivi yakubidi uwe mchawi ndio uziangalie. Halafu ukizingatia kuwa kesho ni Jumatatu siku ya kazi.
Ndio maana mie naombea maandamano yaendelee mpaka wahamishe kombe la dunia lifanyike Uingereza ili tufaidi game bila kusinzia. Wananchi wa Brazil Endeleeni kuandamana na kuleta vurugu mtusaidie sisi wapenzi wa Soka.
 
watu wengine mambwiga kweri keri....nimeona live nikajua mechi imeanza.....
 
Presha yapanda Hispania na Brazil
LEO Jumapili Dunia itashuhudia fainali kabambe ya Kombe la Mabara kati ya Hispania na Brazil.
Huku presha za nchi hizo zikiwa juu, kocha wa Hispania, Vicente del Bosque, amesema anachotaka kuona ni wachezaji wake wanapata ubingwa huku akisisitiza hawezi kuvumilia kusikiliza maelezo kuwa wamechoshwa na mechi nyingi mfululizo.
Hispania ambayo ni mabingwa wa Kombe la Dunia, wamefika fainali baada ya kuitandika Italia kwa penalti 7-6 huko Fortaleza juzi Alhamisi.
Sasa Kocha Del Bosque anaamini wachezaji wake wamepumua kwa siku mbili kabla ya kutua kwenye mechi ya fainali.
Wachezaji wa Hispania wamekuwa wakilalamikia joto kali la Brazil na kudai kuwa jambo hilo ndio linafanya wasifunge mabao mengi.
Lakini Del Bosque amesema anaamini mechi ya fainali dhidi ya Brazil kwenye Uwanja wa Maracana jijini Rio de Janeiro itakuwa ya mafanikio.
Kocha huyo amewaambia wachezaji wake wanapaswa kujituma kwenye Uwanja wa Maracana ambapo ilipigwa mechi ya nusu fainali kati ya Brazil na Uruguay na wenyeji walishinda kwa mabao 2-1. “Sitaki kusikia sababu wala visingizio vya aina yoyote,” alisema Del Bosque ambaye aliiongoza Hispania kupata ubingwa wa dunia mwaka 2010 na ubingwa wa Ulaya miaka miwili baadaye.
“Ninafahamu wapinzani wetu wamekuwa na muda mrefu wa kupumzika kwa kuwa walicheza nusu fainali Jumatano, lakini na sisi tuna saa 72 za kuvuta pumzi,” alisema.
Kwa upande mwingine, kocha wa Brazil, Luiz Felipe Scolari, amesema timu yake kwa sasa ni nzuri na ana uhakika atawanyoa mabingwa hao wa dunia.
Kocha huyo ambaye ameanza kazi ya kuinoa Brazil miezi saba iliyopita, anaona mwanga mpya kwenye timu yake iliyotwaa ubingwa wa Dunia miaka 11 iliyopita huko Japan.
Brazil imefika fainali baada ya kuzifunga Japan, Mexico, Italia na Uruguay.
SC: M_spoti

halafu wakishinda spain wajitie hata kama kuna joto kali wao nacheza tu..
 
Kiukweli huo muda wa fainali ni kikwazo sana na ujio wa Obama huu bongo ndo kabisaa hakuna kutembea uck
 
Back
Top Bottom