Yahya, bado ninatatizwa na huu upungufu mkubwa wa wapiga kura wakati wa zoezi la upigaji kura. Nashauri tume ifanye utaratibu wa kupitia upya daftari nchini ili kubaini kama kweli hawa watu walijiandikisha kweli au kuna jambo lolote lisilo la kawaida. Kwa nini tatizo halikuwa kubwa sana Mwaka 2005, na kadiri chaguzi zinavyoendelea ndivyo idadi ya wapiga kura inazidi kupungua. Why? Binafsi naona elimu ya wapiga kura inatolewa zaidi sasa kuliko ilivyokuwa hapo nyuma kwa nini watu wasijotokeze zaidi pia?