Mkuu! Fahamu kuwa kiasi cha 75000 ni kununua lita karibu 40 za diesel. Kwa wastani magari makubwa (kulingana na tonnage) husafiri km hadi 6 kwa lita. Hapo ni kwa mwendo wa 80km/hr na kwenye barabara isiyo na milima akitumia gea ndogo. Kwa hivyo utaona kuwa km 6/ltr ni mwendo wa km240 endapo kanunua lita 40! Depending wapi anaekwenda na ukubwa wa gari, kwa siku utamaliza lita hizo. Mfano, kawaida magari mengi reserve yake ni litre 10-15 hasa makubwa. Kwa hiyo endapo tank ni tupu, ina maana dereva anakuwa na litre 25 tu za kufanyia kazi! Hizi zita-cover km 150 tu