Tatizo tulilonalo watanzania ni kwamba hatuna sera yoyote ya kupambana na mfumuko wa bei. Hivyo tunajiendea hovyo hovyo tu tofauti na nchi nyingine. Chombo kikuu serikalini cha kupambana na inflation ni benki kuu ambayo maelezo yote inapewa kutoka wizara ya fedha.
Tatizo tulilonalo watanzania ni kwamba tunapenda sana bidhaa za nje kuliko za nyumbani, bic ya kuandikia, chaki za kuandikia na madaftari vyote hutoka nje ya nchi na vikifika nyumbani bei yake huwa juu sana kulingana na ushuru wa forodha na kodi kadhaa baadaye. Nakubali bidhaa zetu za ndani wakati mwingine hazina ubora wowote wa kushindana na bidhaa za nje, hivyo basi mwathirika mkuu wa mfumuko wa bei ni end user (mtumiaji wa bidhaa) ambapo kimsingi ni mtanzania. Madhara mengine kwa ufupi ni pamoja na kushuka thamani ya pesa yetu, wafanyakazi kuhaha na kutokidhi mahitaji yao kwa kuwa inflation haiendani na nyongeza katika mishahara yao na hii ni indication kwamba uchumi wetu ni wa hovyo.
Nini kifanyike? Tuandae sera mahsusi na maalum kwa ajili ya tatizo hili na ifanyike control ya kila wiki 6 kufanya tathmini kuona kama sera imefanikiwa au lah!. Rais anaweza kuteau tume maalum kushughulikia zoezo hili na uzuri ni kwamba tunao wasomi wengi ambao wanaufahamu uchumi. Hapa akina Lipumba wana maoni ya kuliokoa taifa letu na matatizo haya. Vinginevyo tutaendelea na inflation itapanda na mwishowe tutakuwa na taifa kama lile la Zaire wakati wa Mobutu au uchumi kama wa zimbambwe, mimi nadhani keshokutwa tutachapisha noti mpya za elfu 20 na elfu 50 kupunguza circulation ya fedha mikononi mwa wananchi. Ni hayo niliyonayo ila naomba wana JF tuchangie maada hii kwa kina...