List ya wasanii 50 wa muziki wa Tanzania ambao "wanalazimisha fani"

C.T.U

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
5,070
3,718
Kwanza kabisa naomba nieleweke kuwa sisi watanzania kwa kipindi hiki tunatafuta icon yetu kwenye mziki ambaye kwa sasa hivi atatuwakilisha kwenye industry nzima ya muziki duniani.

Ifike pahala ukisema Tanzania popote duniani kwenye muziki basi uwe una uwezo wa kutaja majina si chini ya matatu.

Mfano ukitaja Nigeria utasema
Dbanj, 2 Face, Ice Prince na WhizKid

Ukitaja South basi watakutajia ChakaChaka.

Ukitaja Mali watamtaja Keita
Senegar basi watamtaja Yossou Ndour
Congo lazima wakutajie koffi Olomide.

Ila sasa ukija Dar Es Salaam a.k.a Tanzania ni majanga kwani hakuna wasanii ambao wanaoliwakilisha taifa katika industry nchi za nje.

Zamani A.Y nilikuwa namuona kama ana muelekeo fulani lakini na yeye namuona kama amelala fulani hivi.

Kidooogo DIAMOND ndio anakuja juu kwa kasi na akiendelea hivi hivi nasema kabisa kuwa atatutoa Afrika kimaso maso.

Wapo wengine wanaojitahidi watu kama ANAKONDA, Vyonie Mwale, ni aina fulani ya watu ambao wana vision na kuona mbali ambao kimsingi wanaweza kufanya wonders siku fulani bila kumsahau Vanesa Mdee.

Pia kuna MAKANJANJA fulani ambao wamevamia fani na kujiita wao ni wasanii well... ila nikiwaangalia naona kama wanalazimisha fani tu hivyo siwezi kumuona D Banj wa kesho wala Chaka Chaka wa kesho katiika kundi hili ambao naenda kulitaja hapa.

Wengine utakuta wanapendwa saana na watu na huwaambii chochote na wana fan base kubwa tu ila wataendelea kutumbuiza hao hao watu wao na wala hawawezi kuwa wanamuziki wa kimataifa

Mbaya zaidi na wao wanataka walipwe mkwanja mreeefu eti sawa na wanamuziki wa kimarekani kwa kipi?
kwa kuimba sijui NAKOMAA NA JIJI?
thubutuuu.

Watabaki kuwa local artists na kuendelea kulipwa laki saba kwa sababu wao ni wa kiwango hicho cha laki saba ila nawashangaa eti wanataka kulipwa Milioni kumi er show.

Nacheka sana nikisikia hii.

Unless hawatajibrand kimataifa na kutoa muziki wenye ubora plus video watabaki kupiga show za bure za kina airtel na vodacom , kupanga sinza, kuendesha gari zisizozidi mill 10, na kunuka umasikini kila wanakopita.

They need to something ila wakiendelea hivi hivi na wakiwa na ndoto ya kuwa kama kina jay z mie nina ujumbe mmoja tu kwao.

WANALAZIMISHA FANI

WAFUATAO NI WASANII AMBAO MIE KWANGU NAONA KAMA WANALAZIMISHA FANI


1) Young D

2) Shilole

3) Country Boy

4) King Kapita

5) Baba Levo

6) Cyril

7) Jux

8) Mo Racka

9) Young Killa

10) Nyandu Tozi

11) Mr Blue*

12) DuduBaya

13) Kala Pina

14) Masawe mtata

15) Shetta

16) H Baba

17) Chibwa

18) Dogo Mfaume

19) Sam Machozi

20) Queen Darline

21) Kimbunga

22) Bonta

23) Keysha

24) Berry White

25) Berry Black

26) Gerry Wa Rhymes

27) Mansuli

28) Ney Wa Mitego

30) Isha Mashauzi*

31) Omar Tego*

32) Q Chilla*

33) Izzo Bizness

34) Whitness

35) Mataluma*

36) Manzese Crew

37) Mh Temba*

38) KR

39) Bibi Cheka

40) Babuu Wa Kitaa

41) Mbishi Real

42) Timbulo

43) Bonge La Nyau

44) Abdu Kiba

45) Tunda Man

46) Recho

47) Barnaba*

48) Menina

49) Baby Madaha

50) Snura
 
mimi sio mfuatiliaji wa hizi mambo zenu...lakini naona Barnaba(47) hastahili kuwepo katika list yako...
Huwa naona ana vocal nzuri na akiimba anaweza kubadili kule kupanda na kushuka kwa sauti bila kwikwi...
 
Huo ndo mtazamo wako! ngoja tusubiri wajuzi wa mambo ya music na watakao guswa watoe yao.
 
Hujui tz ni sura na kupaka poda ndo usanii ukiwa tu na hela ya kurecord na kuhonga media baaas!eti shilole&hemed wasanii
 
Ukiona chanel zote za maisha zimebana ingia hapa:kuimba,kuigiza,utangazaji hata kama utashusha utu wako.only in tanzania
 
Nakumbuka Steve mshabiki wa Yanga
akiulizwa anasema sina dhiki na hela
mwalimu wako wa muziki anasema ni
CD yangu Chumbani.


Teh teh kwi !
 
Usiwaonee baadhi generalise tu wote kama hawana kitu 0 brain

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
We jamaa umechemka kwa kweli,rudi ukajpange upya,
Jux ana hit songs kama uzuri wako,napata raha,mwambie yeye n.k,
Izzo B (Miss biznes,naongea na riz1,ball player,afu kuna hii aloimba na shaa na barnaba)
Cyril (Nmerud,Nafanya,mtoto wa singida)
Abdu kiba (bingwa viduku,kidera),RUDI KAJPANGE JAMAA AFU NDO UJE TENA NA LIST AKO
 
We jamaa umechemka kwa kweli,rudi ukajpange upya,
Jux ana hit songs kama uzuri wako,napata raha,mwambie yeye n.k,
Izzo B (Miss biznes,naongea na riz1,ball player,afu kuna hii aloimba na shaa na barnaba)
Cyril (Nmerud,Nafanya,mtoto wa singida)
Abdu kiba (bingwa viduku,kidera),RUDI KAJPANGE JAMAA AFU NDO UJE TENA NA LIST AKO

Wewe ndio unayechemka sasa viduku ni muziki tangu lini? Viduku ni starehe ya watoto waliokimbia shule.
 
We jamaa umechemka kwa kweli,rudi ukajpange upya,
Jux ana hit songs kama uzuri wako,napata raha,mwambie yeye n.k,
Izzo B (Miss biznes,naongea na riz1,ball player,afu kuna hii aloimba na shaa na barnaba)
Cyril (Nmerud,Nafanya,mtoto wa singida)
Abdu kiba (bingwa viduku,kidera),RUDI KAJPANGE JAMAA AFU NDO UJE TENA NA LIST AKO

kuwa na hit songs hakukufanye uwe Icon ya Tanzania Mapepe ya Kingwendu ilikuwa ni HIT SONG kipindi kile ila ile nyimbo ulikuwa unaweza kuishindanisha na awards za kimataifa kwa namna yeyote ile? na hit song ni kwa kigezo gani hicho ambacho umesema kuwa ni Hit Song nipe vigezo unavyosema kuwa ni Hit Song

wenzetu marekani wana Billboard sie tunayo ?

au kupigwa sana kwenye vile vipindi vyenu vya saa nane mchana redioni ndio hit song??
 
Duh sikujua kuna wasanii wengi hivi bongo, kuna wengine zaidi ya hao uliowataja au ndio wote humo. Duh kumbe tunajitahidi kuwa na wanamuziki ila sad siwajui wala sijui nyimbo zao.

Diamond eeeh huyo namjua, na nimemsikia ali kiba, ommy dimpoz nae napenda mwimbo mmoja na ray c nyimbo mbili za zamamni, lady jd ana maneno mazuri nyimbo sikumbuki majina za zamani ila simpendi sijui kama anajua kuimba au niseme ana sauti ya kuwa ni mwimbaji, maana anivutiii kabisa nilijaribu hakuniingia kabisa hadi leo.

Vanessa mdee ungemuweka kwenye 50 na kidoti wote na wengine wanajaribu tuuu kwa kutumia u fame wao wa vingine ndio maana mnawasikiliza bali mmmhhh, sauti ya vanessa kwenye ommy dimpoz song tu. Kwingine niliona na video alichemka sana.

Wengi wanasikiliza na kuogopa kumkosoa director au nao hawajui kitakachoendeana na nyimbo etc

Diamond hata apige show ya laki sijui ngapi nitaenda kama kawa.
 
Nasikitika... hata hao uliowataja bado hawatuwakilishi kimataifa..

Show zote wanazofanya nje ya nchi zinaandaliwa na wa-Tanzania wanaoishi nje..Na hapo itategeamea ni birthday,party za kawaida nk..

Tanzania imewakilishwa na

1.Tatunane
2.The kilimanjaro Band(wananjenje)
3.Inafrica Band
4.kilimanjaro connection(wana mkorogo)
5.Mark Band
Hizi zimeweza..
Hao uliowataja "ARE NOT MUSICIAN'S"
 
mimi sio mfuatiliaji wa hizi mambo zenu...lakini naona Barnaba(47) hastahili kuwepo katika list yako...
Huwa naona ana vocal nzuri na akiimba anaweza kubadili kule kupanda na kushuka kwa sauti bila kwikwi...


Mkuu kuwa na Vocal Nzuri sio kigezo cha wewe kuwa msanii wa kimataifa kuna vitu vingi sana ambavyo msanii unatakiwa uwe navyo ili kupenetrate soko la mziki la dunia..

kwa wenzetu kuna watu wana Vocals msala mara mia ya barnaba na still wamekuwa traped underground nenda kwenye reverbnation then search RnB uone mambo
 
Nasikitika... hata hao uliowataja bado hawatuwakilishi kimataifa..

Show zote wanazofanya nje ya nchi zinaandaliwa na wa-Tanzania wanaoishi nje..Na hapo itategeamea ni birthday,party za kawaida nk..

Tanzania imewakilishwa na

1.Tatunane
2.The kilimanjaro Band(wananjenje)
3.Inafrica Band
4.kilimanjaro connection(wana mkorogo)
5.Mark Band
Hizi zimeweza..
Hao uliowataja "ARE NOT MUSICIAN"
mkuu una mawazo kama yangu kabisa.

Shikamoo mkuu
 
kutotambulika kimataifa ndo "kulazimisha fani"??????,(vipi kwenye tasnia nyingine kama bongo movie,soccer,siasa n.k),King Kibaden alikua analazimisha fani enzi zake kwa kua hakujulikana kimataifa??,Juma Kaseja analazimisha fani kwa kua hajulikani kimataifa??...umewakosea heshima wasanii wengi sana,unajua kama KR ndo mwanzilishi wa kundi la GWM (late 1980's & early 1990's) na waasisi wa hicho kinachoitwa "temeke rap style" na inspiration kubwa kwa vijana wa pande zile akiwemo juma nature,gangwe mobb,lwp,n.k

Mbona kuna nchi umetaja msanii mmoja mmoja,kwa hiyo waliobaki wote wanalazimisha fani???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom