Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,156
- 31,049
Kwa wale waliowahi kutazama series ya Jumong hii ni sound track number 7, ni moja ya soundtrack kali wabongo wameicopy na kuitumia kwenye movie nyingi sana
Kwa waliotazama series ya Spartacus nadhani mtakuwa mnaikumbuka hii theme nadhani inaiwa Sura theme ni bonge la theme.
Hii utaikuta kwenye movie ya Gladiator hii inajulikana kama Now we are free, Kaiandika na kuiproduce Hans Zimmer ila kaimba Richard Gerrad. Lugha iliyomo humu ni ya kubuni kama ambavyo Anya aliimba lugha ya kubuni kwenye May it be ya Lord of the ring kwa kutumia lugha ya kubuni
Hii utaipata kwenye Mini series ya THe Lord of the rings, kaimba mwanamama Anya yule ambaye nyimbo zake zinasikika kwenye kipindi cha Bango. Huyu mwanamama anaimba balaa japo inasemekana ni muabudu shetani na nyimbo zake zinadaka balaa.
Hii utaipata kwenye Game of thrones season ya 8 epsode nadhani ya 9 wakati wakisubiri kupambana na the Night King. Ni one of the best soundtracks za GOT na hiyo ilikuwa among the best epsode ya wapenzi wa GOT maana hakuna aliyejua kama atapona kwenye battle na the night walkers.
Hii ni soundtrack yenyewe ya GOT wakati show inafunguliwa na kufungwa.
Hii emotion theme inajulikana kama Latika theme, iko kwenye slam dog millionare ni humming theme
James Hormer ndiye mtengenezaji mkuu wa themes nyingi za Titanic na katisha.
Katika utengenezaji wa movie, themes zinacost sana yani mtengeneza theme za movie naye anashiriki kama director wa movie inabidi wakae na direct watazame movie waamue nini la kuweka siyo kama bongo wanachukua theme yoyote wanatupia hata kama ya movie nyingine, au wanaweka kinanda hakiedani na moment. Unakuta theme ni ya mapenzi inapigwa theme over movie la kivita.