Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo

Lissu tembelea Rusahunga - Rusumo haraka iwezekanavyo

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Mtia nia kipenzi cha wengi yapo mengi yanayoashiria wazi kuwa "ni wewe 2020" kama hapatakuwa na zengwe.

Kuna wale wanaoijitanabaisha kuwa wamefanya mengi hasa kwenye miundo mbinu hali ni janja janja tu za kutafutia kura mijini.

Katika picha ni hali halisi ya barabara kuelekea rusumo kutokea rusahunga kama ambavyo iko kwa miaka mingi sasa. Inafahamika wazi kuwa bila ya ufanisi wa barabara kama hii bandari ya Dar ni kama mfu. Yaani marehemu kaburini.

Kodi lukuki serikali inachukua kupitia barabara hii na hata ingeweza kupata mapato zaidi, achilia mbali maafa wanayo wasababishia watumia barabara hii.

Waathirika wa barabara hii wakiwamo wakazi wa maeneo hayo, wenye magari, wasafiri na hasa wote wenye uelewa wa kuwapo kwa bandari Dar na umuhimu wake kiuchumi si kundi la kubeza.

Ziara ya mapema huko itakupa picha zaidi ya janja janja zao za kisiasa ndumila kuwili hawa.

Ikumbukwe hali imekuwa hivi hivi bila kushughulikiwa tangia miaka ya 2014 na hata kabla sana ya hapo.

IMG_20200808_073721_332.jpg


IMG_20200808_072932_015.jpg


IMG_20200808_113420_115.jpg

IMG_20200808_093123_136.jpg

IMG_20200808_093123_136.jpg
IMG_20200808_094250_673.jpg


IMG_20200808_090622_003.jpg


Haya yakiendelea huko, makwetu kulikotukuka kwenye hata international airports pako hivi:

Chato kupo hivi. Je, hii ngozi haivutwi mno?

Wanasema Tanzania itakuwa kama ulaya. Lini kama hata kabla ya 2014 hauonekani umuhimu wa kuitumia bandari ya Dar kikamilifu kwa maslahi ya nchi? Labda ni kama kwa ule mwujiza uliomsabaratisha Corona virus.

Hali ya mbaya mno ya barabara Nyakanazi Rusumo vipaumbele vyetu ni nini?

Madhila ya Barabara Rusahunga -Rusumo

Ukiwahi huko baadhi ya magari yaliyoanguka utayakuta kama yalivyo katika picha.

Hivi ni baadhi tu ya vishindo vya awamu ya tano.
 
Hiyo njia haina wapiga kura wengi watumiaji wakubwa wa hiyo njia Ni madereva wa malori wa kutoka nje ya Nchi na maeneo ya Dar es salaam Sio wapiga kura wa huko
 
Si mnasema barabara hata wakoloni walijenga?

Kwani Lisu na Chadema mnahitaji barabara? Kwani mtakula hizo barabara?

Akili za vijana wa chadema ni takataka kabisa!

Utasikia hoo sisi hatuna shida na reli, bwawa, barabara wala flyover.
Lakini hapa unajibinuabinua kuomba ujengewe barabara.? Shwain.
 
Kwa iyo mnajenga barabara kwa kuangalia Kama Kuna wapiga kura wenu au kwa maslahi mapana ya uchumi wa Taifa?
Kama nlimsikia vizuri Lisu alisema nchi hii haina shida na barabara maana hata wakoloni walijenga.

Kwa maneno mengine anasema barabara siyo sehemu ya maendeleo.
Kama unabisha muulize nyumbu mwenzio anaitwa SIJIJUI.
 
Kama nlimsikia vizuri Lisu alisema nchi hii haina shida na barabara maana hata wakoloni walijenga.

Kwa maneno mengine anasema barabara siyo sehemu ya maendeleo.
Kama unabisha muulize nyumbu mwenzio anaitwa SIJIJUI.
Umepaniki wewe mbogamboga
 
Hiyo njia haina wapiga kura wengi watumiaji wakubwa wa hiyo njia Ni madereva wa malori wa kutoka nje ya Nchi na maeneo ya Dar es salaam Sio wapiga kura wa huko
Mkuu achana na hizi taktaka za humu!

Kila siku wanasema humu barabara siyo sehemu ya maendeleo.
.
Si umeona mgombea wao anasema Magufuli atapigiwa kura na flyover na ndege?

Maana yake kwao hivyo vitu si maendeleo
 
Kwani kitoka Nyakanazi hadi Lusahunga bado haijaisha?

Lusahunga Benaco nilisikia kuna mkandarasi, bado hajaanza kujenga?

Hiyo barabara ni mbovu sijawahi kuona. Malori yanaanguka na kuharibika kila kukicha.

Kutoka Lusahunga hadi Mizani, Mizani hadi Rusomo Border ni balaa.
 
Twende taratibu acha kupaniki!
Kwani hata chadema mnahitaji barabara? Mtakula hizo barabara?

Kwani hata chadema wanaona barabara ni maendeleo? Hayo si maendeleo ya vitu hayo?
 
Kwani hata chadema mnahitaji barabara? Mtakula hizo barabara?

Kwani hata chadema wanaona barabara ni maendeleo? Hayo si maendeleo ya vitu hayo?
Hahahaha unajitekenya kucheka mwenyewe
 
Back
Top Bottom