Lissu: Serikali ya wala rushwa haiwezi kukusanya kodi!

Lissu: Serikali ya wala rushwa haiwezi kukusanya kodi!

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
Mhe Tundu Lissu akiwa ana changia kwenye muswaada wa sheria ya fedha (Finance Bill) amesema, serikali ya wala rushwa haiwezi kukusanya kodi. Maneno haya amenukuu kutoka kwa baba wa taifa miaka 20 iliyopita, wakati baba wa taifa akiwa anaongea na wana habari mwaka 1993.

Katika maelezo yake hayo hayo ya serikali kuwa na udhaifu mkubwa wa kukusanya kodi, akaishauri serikali ijikite zaidi kwenye kukusanya kodi kwenye makampuni hasa ya madini na gesi,badala ya kuangaika na "wapaka wanja mitaani".

Aidha, mhe Lissu amegusia na suala la mauaji yaliyo fanywa Soweto Arusha na yale ya Mtwara kwa kusema, kuelekea kwenye ukombozi damu itamwagika tu, lakini ukombozi utapatikana. Hapa alinukuu maneno ya mzee Mandela miaka 60 iliyopita.

Kwa kumalizia mhe Lissu ameeleza masikitiko yake kwa wabunge kuendelea na shughuli za bunge huku mauaji kwa watanzania yakiwa yamefanyika, hapa mhe Lissu aliongea kwa uzuni na masikitiko makubwa sana.

Akichangia hoja bungeni jioni ya leo kwa masikitiko makubwa,watu wanauawa serikali imenyamaza,mlipoko wa bomu arusha bunge linaendelea na shughuli lkn siku moja tutapata uhuru wa kweli kwasababu nchi ya tanzania inapita ktk bonde la uvuli wa mauti lkn damu hizo hazitaenda bure zitaleta chachu ya mabadiliko na uhuru wa kweli zidi ya wakoloni weusi maccm

chanzo
bungeni
 
Lisu anawazungumzia watoto wawili wa Africa yaani
Nyerere : Amezungumzia kauli yake kuwa serikali corrupt haikusanyi kodi
na Mandela: Amezungumzia kauli ya njia ya kwenda kwenye uhuru na namna watu wengi wanaoteswa kwa ajili ya uhuru wa waTanzania.
Amerudi kwa ari mpya na nguvu mpya.
 
Serikali dhaifu, corrupt inahangaika kumgandamiza mlalahoi tatizo kubwa sana hawa watawala wetu tulionao
 
Tulishapata uhuru toka mwaka1961 na tulisaidia nchi nyingine kupata uhuru . sasa uhuru anaosema mh lissu ni upi? Hata marekeni na kwingine kote watu wanaovunja sheria hufikishwa mahakamani na wanaokaidi amri halali hukumbana.na kipigo tuu, sasa wewe kama ni sehemu ya mambo yote haya lazima ukutane na mkono wa sheria. Huu ndio ukweli halisi.
 
Wezi hawawezi kukusanya kodi olesendeka kasema ikiundwa tume wengi wataondoka so lissu yupo sahihi
 
Mhe Tundu Lissu akiwa ana changia kwenye muswaada wa sheria ya fedha (Finance Bill) amesema, serikali ya wala rushwa haiwezi kukusanya kodh.

Pia ameongelea swala la wabunge kuendelea na vikao huku watanzania wakiwa wamepoteza maisha.

huyu jamaa si wa kawaida,namkubali na bi kiroboto alikuwa anataka kulia wakati Lisu ananukuu wana wa afrika na matamshi yao. Aisee ilikuwa speech tamu.
 
Mimi sioni kama kuna mada ya kujadili hapa. Unataka tujadili nini? Kauli ya Lissu kum Quote Mandela kuhusu long walk to freedom ambayo amei google leo kwakuwa mzee mgonjwa mahututi?
 
Na amenukuu maneno ya Mandela..."njia ya kuelekea kwenye uhuru ni ngumu, na wengine itabidi wapitie kwenye mabonde ya vifo ili waweze fika kwenye kilele cha mafanikio". Huyu jamaa ni noma, haya maneno nadhani yapo kwenye kitabu cha Mandela "LONG WAY TO FREEDOM".
 
Tulishapata uhuru toka mwaka1961 na tulisaidia nchi nyingine kupata uhuru . sasa uhuru anaosema mh lissu ni upi? Hata marekeni na kwingine kote watu wanaovunja sheria hufikishwa mahakamani na wanaokaidi amri halali hukumbana.na kipigo tuu, sasa wewe kama ni sehemu ya mambo yote haya lazima ukutane na mkono wa sheria. Huu ndio ukweli halisi.

Hata Makaburu walikuwa wanasema hivyo kwamba South Africa ipo huru. Mandela alicho kuwa anafanya ni uhaini. Mwisho wa siku mambo yakawa hadharani.

Hata Tanganyika pia. Wachache wanao faidi keki ya Tanganyika, lazima waseme Tanganyika ilipata Uhuru 1961. Siku ikifika waTanganyika tukafaidi wote kwa ujumla wetu, ndio utauona uheru na ukombozi wa kweli wa Tanganyika.
 
Mimi sioni kama kuna mada ya kujadili hapa. Unataka tujadili nini? Kauli ya Lissu kum Quote Mandela kuhusu long walk to freedom ambayo amei google leo kwakuwa mzee mgonjwa mahututi?

Suala la kujadili hapa ni: Je ni kweli kuwa serikali hii ni dhaifu na kwamba haikusanyi kodi?
 
serekali corrupt itakua ina kimbizana na wafanya bishara wadogo ikiwaacha wafanyabiashra wakubwa tena ikiwasaidia kukwepa kulipa kodi.
mfano mzuri ni makampuni ya simu,hayalipi kodi na hata umeme pia hawalipi,wanatumia umeme wa wizi hawalip bili,huku mtaani watu wanasumbuliwa kila siku kuhusu kulipa bili kubwa ya umeme kumbe wanaenda kubalance mambo.
 
Tunawashukuru sana wanasingida vijijini kwa kutuletea Tundu lisu bungeni
 
Lisu anawazungumzia watoto wawili wa Africa yaani
Nyerere : Amezungumzia kauli yake kuwa serikali corrupt haikusanyi kodi
na Mandela: Amezungumzia kauli ya njia ya kwenda kwenye uhuru na namna watu wengi wanaoteswa kwa ajili ya uhuru wa waTanzania.
Amerudi kwa ari mpya na nguvu mpya.

Huyu hana lolote bali alikuwa anagenye ya kutoa matusi tu kama kawa.
 
Tulishapata uhuru toka mwaka1961 na tulisaidia nchi nyingine kupata uhuru . sasa uhuru anaosema mh lissu ni upi? Hata marekeni na kwingine kote watu wanaovunja sheria hufikishwa mahakamani na wanaokaidi amri halali hukumbana.na kipigo tuu, sasa wewe kama ni sehemu ya mambo yote haya lazima ukutane na mkono wa sheria. Huu ndio ukweli halisi.
Usijifanye unaijua marekani kutokana na Ujio wa Obama, Nimesona sheria Marekani, hakuna hata kifungu kimoja kinachompa ruhusa police apige mtu. Je unajua kuna kesi ngapi za police brutality huko marekani? Je unajua police wangapi wanafungwa kutokana na kupiga watu? Nenda kasome acha kuwa mshabiki
 
Suala la kujadili hapa ni: Je ni kweli kuwa serikali hii ni dhaifu na kwamba haikusanyi kodi?
kukumbushana ni muhim sana na mtu ambaye hana kumbukumbu duniani ni mwendawazim so kukumbusha siyo vibaya!!
Watanzania tunaogojwa wa kusahau sana tukipata watu wa kutukumbusha ni vizuri sana.ndio maana kwenye tasisi zote kuna vikao na mikutano ya mara kwa mara yote ni kukumbushana juu ya malengo na wapi tuna toka na wapi tuna kwenda na pia maneno ya wahenga ni dawa wakati mwingi na utu uzima ni dawa pia.kutukumbusha manene ya nyerere ni vizuri itasaidia ambao hawakuyasikia
 
Back
Top Bottom