JF Member
JF-Expert Member
- Dec 14, 2014
- 7,391
- 9,665
Andika vizuri. Unachokiwaza umishia kuandika robo yake na hata hakieleweki bado.Hakika Tundu Lissu ana maono. Utawala wa awamu ya tano amefanya nao kazi ndani ya bunge na nje kwa muda wa mwaka mmoja na miezi 10 tuu, lakini yale yote aliyokuwa anayasema kuhusu utawala huu na kiongozi mkuu sasa baada ya miaka minne kupita tumegundua hakuna hata moja alilokuwa anawasingizia na yametokea na kutokea.
Kuanzia udikteta uchwara, utawala bora, matumizi mabaya ya polisi, kuminya Uhuru wa bunge na mahakama na hata upendeleo wa kikanda.
Kulikuwa na kusudio la kumuua Lissu September 7, 2017 na sababu zinahisiwa kuwa za kisiasa kutokana na kusemea ukweli.
Je, kiongozi mwenye maono kiasi hiki na asiye na rekodi ya ufisadi huku akiheshimu sana sheria na kuitetea katiba hatutakuwa tunapoteza tumaini la taifa kama 2020 tutaacha fursa ya kumtumia kuirudisha nchi kwenye matumaini na furaha?