Lissu anamwaga cheche Kibaha

Lissu anamwaga cheche Kibaha

Mpaka raha, jana kamgaragaza vibaya Job Ndugai, leo amegeuza makali Kibaha na anatoa elimu ya uraia.
Nazidi kuona ni kwanini JK alikuwa anamwogopa sana Lissu.
 
ndg wanabodi jf.niliahidi kuja hapa tena mara baada ya mkutano kwisha nami naleta kile tu nilichokisikia toka kwa kamanda lisu.

mara baada ya kukaribishwa alitoa shukrani zake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza huku wakiwa na kiu kuu sana.

'kuhusu mabaya ya ccm sita yasema kwa kuwa kila raia anayafahamu,kuhusu maisha bora kwa kila mtanzania hilo sita sema kwa kuwa tunajua sote kuwa tunaishi kwenye umasikini uliotopea.Bali nitaongelea mambo yahusuyo Tanzania ya sasa na kule tunakotaka kuipeleka na wala si ccm wanakotaka iende bali sisi.

nini wajibu wetu,kama raia kuhusu nchi yetu

KUHUSU MFUMO WA ELIMU/AFYA
Elimu imeharibiwa tangu chekechea hadi chuo kikuu,hakuna elimu bora kwa vijana wetu.Afya nayo hospitali za Tanzania zimekuwa sehemu za kufia kwa ndugu zetu.serikali ya chama cha mapinduzi imegombana na walimu,imegombana na madaktari wakidai kuongezewa mkate wa siku kwa kuwa haukidhi mahitaji ya kila siku

KUHUSU HASA NCHI ILIPO NA NINI KIFANYIKE.

Kuhusu wizi wa mali ya uma,pesa zilizoibwa mimi sitazizungumzia kwa maana tunajua yote haya yamefanywa ndani ya miaka 50 ya utawala wa ccm.ila leo nitaongelea kusoma alama za nyakati.ukiweza kuzitambua utaelewa ninacho maanisha.

1.nitaongelea kuhusu kusoma alama za nyakati na
2.katiba

la kwanza ,unaweza ukawa na macho lakini usione,unaweza ukawa na masikio lakini usisikie,aliufananisha utawala ndani ya ccm na mchezo wa mpira wa miguu ya kwamba huwa ni dakika 90 zinazo amua mchezo nani mshindi kwa dakika hizo hata pengine dakika hizo huongezwa na kuwa 120.
sasa utawala huu tayari umesha maliza dakika 85 bila ya ukombozi wa kweli wa mtanzania zimebaki dakika tano(5)
zamani watanzania walikuwa wamekubali ukiwapiga kofi la kushoto wanakupa la kulia ,lakini mambo si yalivyo leo,wao wanarudishia tazama mapambano ya raia na polisi,kule mtwara,songea arusha mbeya dar,dumila morogoro,mtwara,na kwingineko.ukiona raia wanaanza kuchoma vituo vya polisi na woga ukitoweka miongoni mwa raia ujue zimebaki dakika 5,utawala kuvunjika na mapambazuko mapya kuingia.watanzania wanaishiwa uvumilivu wa kuonewa na watawala,
wanadai haki zao.

katika historia ya nchi yetu hakuna hata wakati mmoja ambapo raia walitokwa na woga na kuamua kupambana na polisi.

MIGOMO
Serikali ya ccm,imepuuza haki za watumishi wake na badala yake imekandamiza raia wake,madaktari,walimu,wanachuo,wanafunzi wa shule za sekondari na msingi wote wamegombana na selikali ya ccm,na walimu siku zote ndio inayo simamia upigaji wa kura nao wamenyimwa haki zao.nao wamekata tamaa ya kufanya kazi.

ccm imekosa hoja za kuwaambia tena watanzania.
mf,walifungia gazeti mwanahalisi kuwa ni kinara wa uchochezi na kusababisha wananchi kuichukia serikali yao.hilo halikuwezekana,wakasema ni hawa wapinzani tuwafungie.halikufua dafu,hofu ya nini wao wapo bungeni 300(wabunge wa ccm).na upinzani hasa chadema kama 50 hivi ,hapo hoja si wingi wao ni hoja zinazotazamwa wingi si hoja hoja ni hoja tu.nao wanaogopa na kuamuru bunge lisioneshwe kwa wananchi kwa kuwa ni sehemu ya kusababisha ccm ichukiwe na wananchi .hilo nalo limeshindikana.ukiona serikali ina haha namna hiyo ujue utawala wao uko dakika 5 kwisha.

serikali ilidai ina wapa polisi posho sh100,000.tulipo hoji uhalali kama kweli wanalipwa polisi wakalalamika kuwa magereza wanapata posho sh50000 elfu tu na polisi wa kawaida huku jeshi wakipewa sh.100,000.kama posho,ukiona serikali ina chakachua hadi walinda usalama ujue zimebaki dakika 5 mchezo kwisha.

tazama rais alipata kura 6 tu kambini lugalo,je huwa wanampigia saluti kw unafiki tu ili wapate mkate wao wa kila siku?.angalia hadi ikulu ipo kawe,masaki ipo kawe,na wafanya biashara wakuu wanaishi jimboni kwa halima mdee,mbona ccm ilishindwa huko,ukiona hata walinzi wa nchi wana ipa kisogo ccm ujue dakika 5 zimebaki.

kuhusu kubadilishwa kwa mawaziri wakuu ndani ya miaka 7 ya utawala wake jk.na makatibu wa chama hicho kikongwe kilicho zeeka na kukosa muono wa mbali nayo ilikuwa dalili ya nyakati mbaya kwa ccm.

aliwataka wanakibaha kuanzisha haraka matawi ya cdm kwa kuwa hakuna tena mtetezi wao bila ya matusi na kudai kuwa upinzani umekua kwa kasi ya ajbu kwa miaka ya hivi karibuni.alitolea mfano mkoa wa shinyanga na kutoa wabunge wa upinzani 5,ambao ndi uliokuwa mkoa unaotoa kura nono kwa ccm ukifuatiwa na singida mwaka 2005,nayo singida imeanza kuikacha ccm kwa kuwa walimchagua .saa ya ukombozi ni sasa.
mwisho aliwaasa wana kibaha na watanzania kwa ujumla huyu aliyeko madarakani hata waacha salama,kukabidhi madaraka,huenda kukawa na umwagikaji mkuu wa damu na kuuliwa hovyo kwa kuwa si rahisi yeye kukabidhi nchi kwa urahisi,aliwaasa kwa maneno mengine kuwa ukombozi wao ni sasa,wasiogope.lazima waiunge mkono cdm kwa ukombozi wao kwa kuwa taya ri ccm imekwishakupoteza mwelekeo na kuwa telekeza wananchi na matatizo yao.

KUHUSU KATIBA
nawaomba mshiriki kikamilifu kutoa maoni yenu kuhusu tanzania muitakayo




ni mimi mwanakidagu niliyekuwepo kwenye mkutano wa tundu lisu kibaha.mood,nisaidieni muifufue ile thread ya mchana niliyoahidi kuwajuza walio mbali na kibaha.
 
watu wa pwani wana takiwa kufufuliwa watoke kwenye makaburi.wawe hai tena kiakili na kifkra.wafanye maamuzi.sahii.2015.wasiwe misukule ya ccm.
 
Huyu Tundu Lissu ni mtu hatari sana, yaani wiki iliyopita 'kamkunja' vibaya sana Makinda na magamba wengine bungeni, jana usiku 'kamvua nguo' hadharani Ndugai kwenye kipima joto ITV, leo tena yuko kibaya anatoa dose nzito ya Elimu ya uraia.
 
Lisu,kwa kweli jana ulifunguka nikakuelewa.Ndugai si saizi yako.Sioni mtu wa kusimama na wewe.F.Werema aibu tupu.
 
Kamanda Lissu anatakiwa aanze kusherehekea ushindi huu popote pale anapokuwa jukwaani hata kudansi ni sawa tu ili kuhamasisha wananchi kweli zimebaki dakika tano na wao waanze kudansi. Hii ni lugha ambayo wanachi wengi wanaielewa zaidi ya kutumia maneno mengi sana kwani ubongo wetu sisi wengine huchukua machache tu

Cheza na jukwaa kamanda kwa furaha na wanachi nao watacheza kwa mafanikio unayowaambia.
 
Bado dakika 5 mchezo uishe! Amandla!! Asubuhi njema ya ukombozi inakaribia!!
 
Kamanda Lissu Furaha ionekani kwa vitendo ukiwa jukwaani!
 
Kamanda Lissu Furaha ionekani kwa vitendo ukiwa jukwaani!

Hii inafurahisha strategy sasa ni kuwafanya wananchi wachukue hatuwa hakuna kuhubiri kila siku ujinga wa CCM sasa hivi ni kuwapa wananchi skills za kuhakikisha CCM haiendelei kuharibu nchi na kuwasimamisha kujifanya wako juu ya katiba bravo Lissu
 
Ahsante mkuu kwa taarifa, lkn bado kuna wana jf ambao wapo kwenye blanjet zito ama macho yao yana ukungu mf SUMU, hawa 2waombee uzima washudie msiba wa ccm, bado dk 5.
 
Back
Top Bottom