Lissu amvaa tena zitto.....

Status
Not open for further replies.

jobe ayoub

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
203
99
. Zitto atatimuliwa
MNADHIMU Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tindu Lissu, amesema Mbunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe atakoma kuwa mwanachama mara tu baada ya mahakama itakapolirudisha suala hilo chamani.
Katika mahojiano maalum ndani ya chumba cha habari cha Global Publishers mchana huu, Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chadema, anasema ni vigumu kwa Zitto kuendelea kuwa mwanachama kutokana na mambo aliyoyafanya.
"Zitto alikuwa anataka uenyekiti wa chama chetu, siyo jambo baya, lakini alishiriki kutengeneza waraka wa siri, siri kubwa, ambao haukubaliki. Alimtuhumu mwenyekiti wetu kuwa hana elimu, malaya, mnunuzi mkuu wa mali za chama, fisadi na mambo mengine mengi ya namna hiyo. Huu ni uongo mkubwa, hatuwezi kuukubali.
"Ni vigumu kuzungumzia umalaya wa mwenyekiti wetu lakini nadhani hayo ni mambo ya chumbani ambayo kwa vyovyote huwezi kuyaunganisha na uongozi. Hayo ni mambo binafsi, kama tungekuwa tunalinganisha mambo hayo, sijui tungesema nini kuhusu Rais Nelson Mandela na Bill Clinton wa Marekani ambaye alikumbwa na kashfa katika mojawapo ya vibaraza vya Ikulu ya White House," alisema.
Lissu, alisema Zitto, akiwa Naibu Katibu Mkuu, anafahamu kuwa kila jambo linajadiliwa na Kamati Kuu ambayo yeye ni mjumbe na kwamba tuhuma zote dhidi ya Mwenyekiti na Katibu Mkuu ni uongo.
Kuhusu ukomo wa nafasi ya Uenyekiti wa Chadema Taifa, alisema waraka wa mabadiliko ya katiba ulitolewa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu mwaka 2006, Shaibu Akwilombe aliousambaza kwa wenyeviti wa Wilaya na Mikoa Tanzania nzima uliowataka kuridhia kuondoa kipengele cha ukomo wa nafasi hizo, vinginevyo chama hicho kingekufa kwa vile kusingekuwa na kiongozi halali hadi wakati huo.
"Chama chetu kilitaka kuondoa ukomo huo kwa sababu awali, kilisema kila baada ya miaka kumi viongozi wangetoka, lakini baada ya kulitazama kwa makini, tukagundua kwamba tungekuwa hatuna viongozi kama tungeendelea na utaratibu ule kwa sababu ingefikia baada ya miaka kumi, viongozi wote wanatoka, sijaona chama hicho kama kipo hapa nchini," alisema Lissu.

Yeye ni msumbufu bungeni?
Kuhusu kuonekana kama yeye ni mtu wa vurugu bungeni, Lissu alisema siyo kweli, bali ni mtu mwenye kusimamia kanuni na ndiyo maana anaonekana kuwa hivyo.
Alisema kilichopo hivi sasa ni kuwa ndani ya Bunge la Kumi kuna wabunge wengi wajuaji wameingia (sio wajuaji kama tunavyosema uswahilini, ni wajuaji kwa maana ya wajuaji hasa wa mambo).
Alisema wanajua kutafsiri kanuni na wanazisimamia. "Nadhani ni bunge hili ndilo wananchi wamejua baadhi ya lugha za bunge kama Mwongozo wa Spika na kadhalika, wananiona nina vurugu kwa sababu ninasimamia ukweli.
"Katika Rasimu hii ya Katiba, kumefanyika mabadiliko mara tatu, wanaongea wanakubaliana, lakini baadaye mimi ninasimama na kusema tatizo. Na nikuambie, hoja zote zilizosababisha kufanyiwa kwa marekebisho katika mara zote tatu, zilianza kwenye mkoba wangu, kwenye kalamu yangu, maoni yote kuhusu katiba niliyaanzisha mimi na kuyafanya kuwa ya kambi rasmi ya upinzani bungeni," alisema Lissu.
Alisema Rais Jakaya Kikwete amekuwa akimshambulia kwa kumuita kama mwanasheria msumbufu, lakini kwake ni fahari kwa sababu wakati anamsema hivyo, pia mapendekezo yake yamekuwa yakifanyiwa kazi kila mara.

NB:
1.hivi msemaji wa CHADEMA NI YEYOTE.KATIBU MKUU MSEMAJI,MNYIKA ASEME,MAKENE ASEME,HATA MNADHIMU MKUU NAE ASEME.nani ni msemaji hapa,mwatuchanganya...

2.Mnasema katiba inafuatwa,kamati kuu na baraza kuu ndio watoa mamuzi makuu ktk chama,pale kamati kuu ikitoa hukumu na mtuhumiwa hajaridhika,hukata rufaa baraza kuu ndio chombo cha mwisho kwa hukumu.sasa LISSU anasema Zitto kishatimuliwa wanasubiri mahakama ihamishe majukumu kwa chama.swali kwa LISSU,je ile haki ya mwanachama kukataa rufaa iko wapi,pia mbona unaotoa hukumu ya mwisho wewe wakati katiba inasema baraza kuu ndio chombo cha mwisho kutoa.UNATUCHANGANYA...

3.Mlisema maswala ya zitto yameshaisha na kufugwa mjadala,tena kasema bosi wenu/wako DR slaa.sasa mbona wewe bado upo na zitto tu.Je nawe umekula mrungura unajihami usitajwe km mwenyekiti wako MR. M
 
TL tayari amejidhihirisha ni Mwanasheria kanjanja mpenda sifa na madaraka ndani ya CDM ,hana weledi wa kazi(utamuitaji zzk mbunge wa mahakama?-which means haheshimu maamuzi ya mahakama),ukweli yeye TL ni malaya tu wa vyama so far hana ushawishi ndani ya chama hiwezi kujiringanisha na mwamba ZzK
CDM tumeijenga kwa damu na jasho letu tangia 1993 kipindi hiko hata slaa alikua ni mwanachama mtiifu wa ccm
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom