Lissu amtega JK

Lissu amtega JK

ndiyomkuusana

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
668
Reaction score
426
Julius Magodi, Dodoma
SUALA la kuwapo kwa majaji wasiokuwa na sifa nchini limeingia katika sura mpya baada ya Mnadhimu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu kusema atawasilisha hoja ya kumshtaki Rais Jakaya Kikwete kama atashindwa kuwaondoa kazini ifikapo Kikao cha Bunge lijalo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Bunge jana, Lissu alisema amechukua uamuzi huo baada ya kuona Bunge limeikalia ripoti ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomhoji kuhusu kauli yake ya kuwatuhumu majaji kuwa baadhi yao hawana sifa.

Alisema ameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Rais Kikwete ambaye ana mamlaka ya kuteua majaji, ameshindwa kuwaondoa kazini majaji hao wasiokuwa na sifa. Lissu alisema atawasilisha hoja yake hiyo kwa kutumia Kanuni ya Bunge sehemu ya 11, Ibara ya 121, 122, 123, 124, 125 na 126 na pia kwa kutumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ibara ya 146 A.
Sehemu ya 11 ya Kanuni ya Bunge, Ibara ya 121 inaeleza kuwa mbunge yeyote anaweza kuwasilisha kwa Spika taarifa ya hoja ya kumshtaki Rais kwa madhumuni ya kumwondoa Rais madarakani kupitia azimio la Bunge kwa mujibu wa Ibara ya 46 A ya Katiba ikiwa inadaiwa kwamba Rais; ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinavunja katiba au sheria ya maadili ya viongozi wa umma.
Lissu alisema atakusanya saini za wabunge kuunga mkono hoja yake ambayo ni asilimia 20 kwa mujibu wa Kanuni za Bunge. Wabunge wote kikatiba ni 357.

Julai 13, mwaka huu wakati akitoa maoni ya Kambi ya Upinzani katika Wizara ya Katiba na Sheria bungeni, Lissu alisema uteuzi wa majaji umegubikwa na ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano. Alisema baadhi ya majaji walioteuliwa hawana sifa, uwezo na kwamba hawakufaa kufanya kazi hiyo.

Kauli hiyo ilisababisha Bunge kuiagiza Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo (CCM), Hassan Ngwilizi kumhoji ili athibitishe kauli yake. Alisema wakati akihojiwa na kamati hiyo, pamoja na nyaraka nyingine, aliwasilisha nakala ya ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa mwaka 2008 na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo kuchunguza uteuzi wa majaji nchini. Alisema ripoti ya kikosi kazi hicho kilibaini kuwapo majaji ambao hawana sifa ya kufanya kazi hiyo, lakini Rais Kikwete ameshindwa kuwaondoa kazini.

Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA alisema hali ya mahakama ni mbaya, kwani kuna majaji wawili ambao waliwahi kukamatwa kwa rushwa wakiwa mawakili, lakini wakateuliwa kufanya kazi hiyo. Alisema baadhi ya majaji hawana uwezo hata wa kuandika hukumu kutokana na kutojua vyema lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo inayotumika katika Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani. Mbunge huyo alimtaja Jaji mmoja wa Mahakama ya Rufani ambaye ameteuliwa akisema hana hata shahada ya kwanza ya sheria kinyume cha taratibu. "Kwa mfano, yupo Jaji wa Mahakama ya Rufani (jina tunalo), ambaye hana hata shahada ya sheria anaweza vipi kuwa jaji?," alihoji Lissu.

Alisema jaji huyo hivi sasa anasoma shahada ya sheria katika chuo kikuu kimoja hapa nchini.

Lissu alisema ili mtu aweze kuchaguliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lazima awe na elimu ya shahada ya kwanza ya sheria, awe ametumikia miaka 10 mahakamani na anayechaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Rufani lazima awe ametumikia miaka 15 mahakamani. Mbali ya kueleza hayo, Lissu alisema kwamba alitoa pia katika kamati hiyo, ushahidi unaoonyesha kuwa kuna jaji mmoja wa Mahakama Kuu ambaye hawezi hata kuandika sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka... "Kama jaji hawezi kuandika hata sentensi moja ya Kiingereza iliyonyooka, tunaweza vipi kuwa na mahakama inayotenda haki?"

Alisema kuna jaji mwingine ambaye ameongezewa mkataba wa kufanya kazi mara ya tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria. Alisema kwa mujibu wa Tume ya Mahakama, hakuna jaji ambaye anaweza kufanya kazi kwa mkataba kwa vipindi vitatu.
Mbunge huyo alisema mbali ya madudu hayo katika sekta ya mahakama, hivi sasa kuna jaji maarufu ambaye ameghushi umri wa kuzaliwa ili aweze kuendelea kufanya kazi hiyo. Alisema jaji huyo amezaliwa Septemba 4, 1949 lakini amebadilisha umri wake kuwa amezaliwa Septemba 4, 1952 ili aweze kufanya kazi hiyo hadi mwaka 2017. Mbunge huyo alisema kazi hiyo ya kughushi umri wa jaji huyo imefanywa kwa kunyofoa nyaraka za kumbukumbu zake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Alimtaka jaji huyo kuzirejesha mara moja nyaraka hizo vinginevyo katika Bunge lijalo atamtaja kwa jina hadharani.
Alipotakiwa kueleza kwa nini asimtaje sasa alisema akifanya hivyo anaweza kutingisha nchi. Kama Lissu atachukua hatua hiyo, itakuwa ni mara ya pili kwa mbunge kuwasilisha bungeni hoja ya kutaka kumwajibisha kiongozi wa juu serikalini. Mara ya kwanza alikuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe katika Bunge lililopita alipokusanya saini za wabunge kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitaka awajibishe baadhi ya mawaziri waliokuwa wametajwa kuhusika katika matumizi mabaya ya madaraka katika Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Hata hivyo, Rais Kikwete alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza lake la Mawaziri hivyo kuzima hoja hiyo ya Zitto.

source: mwananchi 17.12.12
 
Usirudi nyuma kaka.Mh. Tundu Lissu ninakubari,kwani unafanya kile ki2 nilichoku2ma. Big up bro. Ikibidi kumuondo madarakani kabisa huyu msafiri rais wetu mchakachuaji ambaye alihisi kazi ya urais ni raisi na sasa anajuta kwani nafasi kwa sasa inampwaya
 
hivi mnamjua Jk au mnamfananisha sana sana atawajibu huo ni upepo tu utapita
 
CCM na Jk wameweka nta nzito maskini hata uwapigie kelele vipi bure kikubwa kuimarisha chama zaidi mikoani na vijijini ili 2015 tuwang'oe kirahisi hakuna njia nyingine maana huwa mswada ukienda bungeni wabunge wa CCM hawataupitisha kwa kuwa matokeo ya kumtoa raisi kwa azimio la bunge ina maanisha pia bunge linavunjwa na uchaguzi mpya kuitishwa, sasa hofu ni hapo kwenye uchaguzi mpya ccm hakuna kitu wanahofia kwa sasa kama uchaguzi!
 
CCM na Jk wameweka nta nzito maskini hata uwapigie kelele vipi bure kikubwa kuimarisha chama zaidi mikoani na vijijini ili 2015 tuwang'oe kirahisi hakuna njia nyingine maana huwa mswada ukienda bungeni wabunge wa ccm hawataupitisha kwa kuwa matokeo ya kumtoa raisi kwa azimio la bunge ina maanisha pia bunge linavunjwa na uchaguzi mpya kuitishwa, sasa hofu ni hapo kwenye uchaguzi mpya ccm hakuna kitu wanahofia kwa sasa kama uchaguzi!
Mkuu usiwe na wasiwasi hii ni hatua tu, CHADEMA kumejaa watu wenye akili sana.

Siku zote siasa za kisayansi kama hizi anazofanya Tundu Lissu zina hatua Nne, hii anayotaka kufanya Tundu Lissu ni hatua ya tatu.
Hatua hizo ni UTAFITI, HOJA, MJADALA, HARAKATI
 
Eti Jaji Mkuu wa Kenya hana hata Shahada?
Are you sure?
I dont think so.

Kwani sheria za kenya zinasemaje kuhusu sifa za muhimu za mtu kuwa jaji?

Kwa jinsi uteuzi wa jaji mkuu Kenya ulivyo wazi na makini sana, sidhani kama mtu asiyekuwa na elimu ya kutosha angepita kuwa jaji mkuu?
 
hivi mnamjua Jk au mnamfananisha sana sana atawajibu huo ni upepo tu utapita
Kwani tuhuma za ufisadi ilikuwaje pale zilipoanza kutangazwa mwaka 2007 Mwembeyanga-Temeke, Dr.Slaa na Tundu Lissu walivyotikisa nchi?
Mpaka leo zinaitesa Serikali na CCM na hawana majibu wa suluhisho wamebaki kunyosheana vidole.
 
Eti Jaji Mkuu wa Kenya hana hata Shahada?

hii ina uhusiano gani na hoja inayojadiliwa hapa ?? sheria, kanuni na taratibu za kenya ni tofauti na Tanzania.
kuhusu hoja ya Lissu ila nina wasiwasi CCM huenda bila kuzingatia hoja wakaendelea na zoezi lao la ku abuse majority power yao ambayo inalipotezea bunge hadhi yake kama chombo huru na kugeuka kuwa rubber stamp ya jk.
 
Acha waseme watakavyo sema lakini ukweli utabaki palepale kwani watu makini hawakurupuki wakati wanapotoa taarifa zao. Kwahiyo hata taarifa ya Mh. Lissu inawatesa na itaendelea kuwatesa mpaka hapo watakapochukua hatua.
 
Eti Jaji Mkuu wa Kenya hana hata Shahada?

Kwa minajili ya kuweka kumbukumbu sawa,Jaji Mkuu wa Kenya ni Willy Mutunga(PhD).
Ungewewa ku google na ukapata taarifa sahihi badala ya kuweka taarifa zisizo sahihi.
 
Eti jaji mkuu wa Tz., ndio aliyeongeza muda wa kuzaliwa..... kama kweli ni hatari sana. @ 2015 tutasikia na kuona mengi sanaaaa

V
SENGEREMA
 
Serikali ya ccm ni kawaida yake kuvunja katiba ya nchi,si suala la majaji tu,hata mambo ya kule ilemela na arusha kuhusu mameya ni mlolongo uleule wa kuvunja katiba na sheria za nchi! Ccm ni zaidi ya uijuavyo!
 
Eti Jaji Mkuu wa Kenya hana hata Shahada?

Mkuu nakushauri usiwe unakurupuka, fanya hata tafiti ndogo kabla haujaingiza taarifa humu jamvini, kwa taarifa yako Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga ana shahada mbili za sheria, moja LLB Nairobi Univ., Kenya, LLM Univ. of DSM Tz., kule jamaa hawateuani kishemeji shemeji kama hapa kwetu.
 
Mkuu nakushauri usiwe unakurupuka, fanya hata tafiti ndogo kabla haujaingiza taarifa humu jamvini, kwa taarifa yako Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga ana shahada mbili za sheria, moja LLB Nairobi Univ., Kenya, LLM Univ. of DSM Tz., kule jamaa hawateuani kishemeji shemeji kama hapa kwetu.
mkuu mbavu zangu mie,kishemeji shemeji. Daa"
 
Mkuu nakushauri usiwe unakurupuka, fanya hata tafiti ndogo kabla haujaingiza taarifa humu jamvini, kwa taarifa yako Jaji Mkuu wa Kenya Willy Mutunga ana shahada mbili za sheria, moja LLB Nairobi Univ., Kenya, LLM Univ. of DSM Tz., kule jamaa hawateuani kishemeji shemeji kama hapa kwetu.

na hajajiongezea umri. Makavu live
 
Kumbe lile suala la cj lilimfikia lissu! Pamoja na kutuma jamaa zake wamtetee humu lakini imefahamika alizaliwa 1949! Loh! Mi nilishangaa hawa jamaa mbona wanazunguka tu bila kutupa umri? Wengine kabisa wanasema tulilala chumba kimoja ila umri hawajui?
 
Eti Jaji Mkuu wa Kenya hana hata Shahada?

Profile of the Chief Justice Willy Mutunga - Kenya

Home » Office of The Chief Justice » Profile of the Chief Justice
Dr. Willy Mutunga is senior counsel and an Advocate of the High Court in Kenya. He has a Bachelors of Law Degree from the University of Nairobi, Masters Degree from the University of Dar es Salaam, and a PhD from York University (Osgoode Hall Law School) in Toronto, Canada.
A committed activist in the pro-democracy movement in Kenya since the 1970s, Dr. Mutunga has worked in a number of prominent human rights organizations throughout the country, and has also been an active member of the university staff trade unions. His work in the pro-democracy movement, notably with the pro-democracy Twelfth of December Movement, made him a target of Moi’s Kenyan African National Union (KANU) party, and he was imprisoned from 1982-83. He has since spoken out enthusiastically on behalf of political prisoners.
Dr. Mutunga was Chair of the Law Society of Kenya from 1993-95. He is also the author of a number of widely published articles on the rights of detainees, the role of NGOs and civil society in democratization, the constitutional rights of Kenya’s nomad pastoralists, and the rights of tenants.
He is a former Board Member of the International Centre for Human Rights and Democratic Development in Montreal. He has also been a consultant, and has written for or edited numerous human rights and civil society publications.
Until his appointment as the Chief Justice, Dr. Mutunga was the representative for the Ford Foundation in Nairobi, overseeing all grant making in the Eastern Africa region, mainly focusing on human rights and social justice and protection of women’s rights. Source: Profile of the Chief Justice :: Republic of Kenya - The Judiciary
 
Wa TZ hasa serikali ya CCM, watu wanapenda kupeana vyeo pasipokuwa na sifa stahiki, hii ni dhambi mbaya sana.
 
Back
Top Bottom