Lissu amlima barua Shibuda

cdm kuchukua nchi ni ndoto ya alinacha, sioni walichonacho kipya zaidi ya kutaka baadhi ya watu wawe na sauti zaidi ya wengine, kwa nini kila mtu anaehoji cdm anagombana na mbowe?mbowe hutakiwi kuwa rais pole kaka

Hivi unajua Hatamtu mzima akiwa Hana Meno mdomoni ukimwambia aongee, utaishia kucheka tu, sasa ndugu yangu kama huna point si unyamaze badala ya kutapika pumba? unajua maana ya kusimamia makubaliano, na jinsi ya kutofautisha na uongozi wa kibepari kama wa magamba?
 
Huyu shibuda afukuzwe ubunge na spika wa bunge kwa sababu amekiuka taratibu,kanuni na sheria za bunge.Bunge linawatambua wabunge wanaowakilisha wananchi kupitia vyama vyao vya siasa walivyopitia kuwa wabunge.Sasa hamuoni shibuda amekiuka hilo?Yeye ni aina mpya ya ubunge ambayo bado haijapitishwa na bunge.MBUNGE ASIYEWAKILISHA KUPITIA CHAMA ALICHOPITIA KUWA MBUNGE.MBUNGE BINAFSI,si bado haijapitishwa wakuu?
 
Kwa mustakabali na maendeleo ya chama Shibuda hafai kuwa ndani ya chadema hata kidogo. Kunako mfaa ni huko alikotoka kwenye watu waliovimbiwa kwa kutojali maslahi ya wengi.

Chadema isipo chukua maamuzi magumu ya kumfukuza itakuwa haina mfano na ule msemo wa wahenga wa mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, kwa maana hiyo atakuja kuleta madhara makubwa baadae na dalili hizo zote tayari zimesha jionyesha kwa kupingana na maazimio na sera za chama dhahiri.

Naiomba kamati imfukuze hata kama tutakosa jimbo. Afadhari kuwa na wabunge wachache watii kuliko utitiri wa aina ya shibuda.
Dr Slaa, Mbowe, Zitto, Lissu na kamati nzima fukuzeni huyo jamaa hatufai sasa na hata tufuata hata baadae.
 
huyu shibuda bado ana ka element za kimagamba,mimi tokea mwanzo sikumuamini kabisa.alishazoea mambo ya kifisadi,kaja chadema kakuta watu wameridhika na njaa zao,ndio maana anapaona pachungu.let him go.hafai
 

Inategemea na sababu yenyewe ya umfukuzia. Kwani wakimfukuza nae akaenda mahakamani na kuwashinda basi atabakia kuwa mbunge kwa amri ya mahakama mpaka bunge litakapo vunjwa 2015. Kwani yeye atadai kuwa anayoyafanywa ameelezwa na wapiga kura wake na sio chama chake. Ukizingatia Wananchi ndio waliomchagua na wanachokitaka atakitenda.

Mfano mzuri ni Mama Naila Jidawi.
 
Uroho wa madaraka ndo unamsumbua alihamia CHADEMA ili apate Ubunge baada ya kuangushwa vibaya na CCM sasa anaona Magambani kwake ni kuzuri anatamani kurudi wajameni kha!! Vyeo hivi balaa tupu
 
Uroho wa madaraka ndo unamsumbua alihamia CHADEMA ili apate Ubunge baada ya kuangushwa vibaya na CCM sasa anaona Magambani kwake ni kuzuri anatamani kurudi wajameni kha!! Vyeo hivi balaa tupu timulia mbali kabisa huyo mtu
 

Kama mtajichanganya kumfukuza hiyo itakuwa ni golden chance kwa ccm. they will make sure jimbo linarudi kwao,kwani wananchi waliompa kura wataudhika na kuwatosa cdm.
shibuda ni kada wa chama kongwe,nawashangaa leo eti ndio mnajifanya hamumtaki. Kuchemka kachemka ila kumfukuza nalo itakuwa ni uchemfu mwingine. mkimaliza kumfukuza huyo afatie Lema, kwani alijifanya kutotambua naibu meya nawakati mpango mzima alihusishwa.
 
chama cha wakiristo kwani yy mwislaam. john Magale Shibuda
 
Kuna mengi ambayo Shibuda amevumiliwa tangu ajiunge na Chadema kwa miezi kadhaa, na hajaonyesha umoja na wenzake iwe katika mikutano ya bunge au mikutano ya hadhara. Wabunge wenzake wanapowajibika pamoja kuitangaza Chadema yeye anajua anakojificha na kusubiri tu kurudi bungeni kwa ajili ya posho. Huu si uwajibikaji. Bora kuwa na watu wachache wawajibikaji kama Lisu, Mnyika, Lema nk na kumwondoa huyu samaki aliyeoza harufu yake chafu isije ambukiza samaki wazuri wakaonekana wote wameoza.
 
Toa hayo magamba kabla hayajagandamana mwilini ili ccm wajifunze jinsi gani wanaume walivyo na maamuzi magumu maana nina uhakika kijana yeyote kutoka chadema anaweza kusisimama pale coz wananchi washapata tuition ya kutosha kutoka cdm

Kijana unamawazo mazuri sana, ila jamaa hawakujua kuwa mwenzao ni kinyonga. Kwa hiyo magamba yake yanabadilika ili kujihami.
 
Kwa hiyo ametumwa na wapiga kura wake kwenda bungeni kutetea wabunge waongezewe posho kufikia laki tano kwa siku?! haya ni matusi kwa wapiga kura ambao wanahangaika huku na huko kupata mlo mmoja wa siku.
 
Vijembe na misuto, lakini hujajibu swali. Nawasilisha tena:

Chadema wametishia kumfukuza Shibuda kwa msimamo wake wa kutaka posho ya Wabunge iendelee.

Katiba ya CHADEMA inaseme mwanachama analazimika akubaliane na
Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA.

Ni wapi ilipoandikwa kwamba kupinga posho inatoka kwenye Katiba, Sera, Kanuni, Maadili ya Chama, Itikadi au Falsafa ya CHADEMA?

Kama papo mahala pameandikwa kwenye Katiba au Sera au Kanuni au Maadili ya Chama au Itikadi au Falsafa ya CHADEMA, kwamba CHADEMA inapinga posho ya Wabunge, mbona Tundu Lissu leo hii amekula posho, afukuzwe CHADEMA?
 


Kama Shibuka hakubaliani na haya basi aondoke tu aache watu wapambane .Aje upande wa MS .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…