Ni dhahiri kabisa kuwa uhai wa Chadema unategemea mbeleko ya Lisu pekee.
Na pia ni jambo lililowazi kuwa Njia pekee ya kumpatia Lisu umaarufu ni uwepo wa mashtaka dhidi yake au kwa yeyote alimradi aende mahakamani.
Bila mahakama Lisu hana hoja wala ushawishi wowote. Nje ya mahakama ni kama samaki nje ya maji; hafurukuti, hana ujanja wala mbinu ya kusurvive.
Hivyo Bila kesi; hakuna lisu wala Chadema.
Chadema imebaki kupata umaarufu wa msimu kwa kutegemea kupanda kwa Lisu mahakamani.
Je? mbeleko hii itaweza kuibeba Chadema mpaka lini? tusubiri na kuona.
Nikiri kuwa mimi ni mmojawapo ambaye ningependa kuona upinzani wenye nguvu kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Maelezo yako yana ukweli ndani yake ingawa inategemea zaidi unaangalia kutokea pembe gani.Kwa mtu wa CCM wa kawaida hii kauli yako ni ya kufurahisha na kutia moyo,"Adui yuko mbendembende" lakini kwa mtu anayetafakari na kuiangalia dunia miaka ishirini ijayo ni lazima awe na wasiwasi.Anakuwa na wasiwasi kwa sababu kwa mwenendo huu atakuwa haoni mwisho mwema kwa jamii yake.Nianze,
Hali halisi ya siasa za vyama vingi imebadilika katika awamu hii kwa kuwa utawala uliopo si wapenzi wa mfumo wa vyama vingi.Hii imedhihirishwa rasmi na matamko mbalimbali ambayo hayana sababu ya kuyarejea hapa.
Jambo la pili ni hulka ya kiongozi mkuu ambayo ndiyo hasa inayo potray utawala uliopo,kufurahia maumivu ya watu wake.Kwa hulka ya namna hii litakuwa jambo la uendawazimu kwa mfano kufanya hata maandamano ya amani kwani ni dhahiri damu itamwagika tu na tunashukuru hilo wapinzani wameliona na wametuepusha nalo.
La tatu ni Chama tawala kumuogopa kiongozi Mkuu kiasi cha kuwa tayari hata kushirikiana naye katika jambo ambalo ni wazi hawaafikiani nalo.
Kwa ufupi ni kuwa si kwamba vyama vya upinzani au mawazo mbadala yamekwisha lakini mawazo hayo utayatoa kwa nani kwa njia ipi wakati tayari kuna viashiria vya wazi (ndani ya bunge na kwingineko)?
Kwa wale wanaoangalia mbali ni kuwa ikiwa vyama vya upinzani vinakuwa kimya mawazo mbadala yatatoka kwa njia gani?
Si jambo la kufurahia kwa vyama vya upinzani kuwa kimya.