Lissu ama Zitto 2020: Magufuli atapata tabu sana

Lissu ama Zitto 2020: Magufuli atapata tabu sana

Tang Zhou

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2018
Posts
1,206
Reaction score
2,591
Wataje viongozi wa Kiafrika dizaini ya Rais Magufuli....Mnangagwa wa Zimbabwe, Yoweri Museveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Al Sisi wa Egypt nk. Viongozi wote hawa ni Wakora kwelikweli....lakini wana jambo moja ambalo rafiki yao hapa nchini hana...maarifa na werevu wa kisomi na wa ki-stateman...wenzake ni wajuzi wa Uchumi, Ulinzi, Intelligencia na ni career soldiers/army officers wakiishi miaka mingi msituni kupigana vita kuzikomboa nchi zao.

Sasa tunaye Magufuli, anatumia maguvu tu bila background yoyote ya kutukuka academically, intellectually na katika medani za kivita na siasa japo anajitutumua kufit in...mtu wa namna hii ni rahisi sana kuachwa APAMBANE NA HALI YAKE ikifika mahali vyombo vya Ulinzi na Usalama vikahisi anakoipeleka nchi siko.

Jambo moja la dhahiri ni kuwa kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za ukinzani nchini CCM itaingia kwenye uchaguzi wa Rais mwaka 2020 ikiwa na mgombea asiye na maarifa ya kujibu hoja za washindani wake kutoka vyama pinzani kuhusu masuala mbalimbali ya siasa, ulinzi na uchumi nchini...na fikiria atakutana na hoja za vijana wasomi Tundu Lissu ama Zitto Kabwe

2015 aliachwa aongee mwenyewe lakini 2020 hakika atapata tabu sana...atajibuje hoja za Zitto ama Lissu? Zile fiksi za Saddam alikuwa Rais wa Kuwait ndo zitazidi hakika.

Vizuri CCM muanze kufikiri tangu sasa, huyu mtu wenu ATAWAPA TABU sana 2020...nimewapa ushauri wa bure ufanyieni kazi ama upuuzeni tutakutana 2020...

Magu vs Zitto....Zitto hawezi kukubali kuibiwa kura kifala, kule Kigoma kuna mapori mengi ikibidi!
 
Lissu vs Magu, hakika huyu mzee jiwe atapitia wakati mgumu zaidi kuliko wakati wowote katika maisha yake ya siasa.

NB; kabla ya yooote hayo tuanze na katiba mpya, tukifanikisha 2020 jiwe ataondoka saa 3 asubuhi kuelekea chato kuendelea na maisha mengine.
 
1. Lissu (Tz)
2. Fat Karume (Zanzibar)

Campaign managers: Tz
1. Zitto Kabwe
2.Prof Baregu

Campaign managers: Zanzibar
1. Seif
2. Mwalimu

MAGU hachomoki hata kwa dawa
Hoja zenu zitakuwa sheria na haki. Mwenzenu ana tangible results.
Mtakwaa kisiki kushinda 2015
 
Kama Tume ni hii hii na waTZ ni hawahawa, hakuna jipya hapo.
 
Kumbuka mwenyekiti wa tume amemteua yeye, jaji Wa mahakama kuu amemteua yeye, mkuu Wa majeshi amemteua yeye, mkuu wa jeshi la polisi amemteua yeye, na mwisho wasimamizi wa uchaguzi yaani wakurugenzi wa halmashauri amewateua yeye
 
Mkuu,CCM huwa hawategemei kura za wananchi kuingia madarakani wao wanategemea police na vyombo vya usalama!
 
Back
Top Bottom