Lipumba, unalipeleka wapi taifa hili?

Lipumba, unalipeleka wapi taifa hili?

Lizaboni

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2013
Posts
33,901
Reaction score
20,410
Kwa siku za karibuni, mwelekeo wa mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba, unazua maswali mengi sana. hali hii inafanya baadhi ya watu waanze kutilia mashaka uzalendo wake hali inayomfanya aonekane kuondokana kabisa na zile siasa zake za kistaarabu. kwamba, wakati Maalim Seif akichochea vurugu kule zanzibar kabla ya yale maridhiano, mzee lipumba alikuwa na mwelekeo tofauti kwa kupinga siasa za vurugu. hali hiyo ilimfanya aheshimike sana kitaifa na kimataifa.

Mashaka yangu yameanza pale alipoanza kuzua kuwa Rais JAKAYA KIKWETE anandaa mazingira ili abaki madarakani hadi mwaka 2017. Kwamba kikwete anataka mchakato wa katiba mpya uchelewe ili aendelee kuongoza nchi mpaka muda huo. Kanusho la Ikulu kuhusiana na taarifa hiyo limemvunjia heshima mzee Lipumba na amejidhalilisha.

Hivi punde kuna taarifa zimeanza kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa kesho tarehe 17/5/2013, shughuli za kijamii zitasimama mjini mtwara ili wananchi wapate fursa ya kusikiliza hotuba ya waziri wa nishati na madini. Sijui taarifa hizo wamezipata wapi maana nijuavyo mie ni kuwa waziri wa nishati anawasilisha hotuba yake Jumatano ijayo na si kesho kama uzushi huo ulivyokuwa. Shauku yao ni kutaka kujua jinsi serikali ilivyoshughulikia madai yao ya kupinga usafirishwaji wa gesi ghafi.

Kilichonishangaza zaidi ni ushiriki wa mzee Lipumba kwenye sakata hilo. kuna baadhi ya wananchi ambao wanajua undani wa sakata hilo, wamedokeza kuwa IBRAHIM LIPUMBA, Mwenyekiti wa CUF amepewa fedha na makampuni ya mafuta na gesi yakiongozwa na kampuni ya AGGRECO, ili ahamasishe wananchi wa mtwara wagomee mpango wa serikali. Pia mzee Lipumba ameandaa watu wake ili hiyo kesho walete fujo na kupora mali za wananchi. inadaiwa kuwa makampuni hayo yanapinga mradi huo ili yaendelee kunufaika na biashara ya mafuta na gesi toka mataifa ya nje. Makampuni hayo ya mafuta inadaiwa kuwa yanatumia fedha nyingi kuwanunua watu wenye ushawishi kwenye jamii ya wana Mtwara ili kuchochea vurugu.

Kutokana na hali hiyo, nimeanza kupata mashaka na kuanza kujiuliza, upo wapi uzalendo wa mzee lipumba, uko wapi usomi wa mzee lipumba ambaye alikuwa anatumia elimu yake kuishauri serikali. kwa hili la kuhamasisha vurugu na uvunjaji wa amani ni wazi kuwa huyu mzee ameanza kufilisika kimawazo. Najua kuwa anatumika na makampuni hayo ya mafuta kama tulivodokezwa, ila cha kujiuliza ni kuwa anafanya hayo kwa faida ya nani? Ona sasa jeshi la polisi limepeleka askari wengi mtwara na silaha za kutosha kudhibiti vurugu hizo, je wananchi wakiuawa, yeye atapata faida gani. hilo likitokea najua kuna watu watageuka. Wale waliokuwa wanasema kuwa serikali ni dhaifu wataanza kusema kuwa serikali ni kandamizi.

Hayo ni maoni yangu tu.

SOURCE: mimi mwenyewe
 
Ikulu imekanusha tu lakini Mpango huo upo kwenye meza za mawaziri, na ni kweli bila shaka kuwa kuna proposal hiyo ya kuiweka serikali iliyopo sasa hadi 2017..
 
JK ni janga la kitaifa. Akifa nitafanya sherehe kubwa kufurahia kifo chake kwani ameliangamiza taifa letu.
 
kama ni kweli sasa lipumba anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe na hili ndilo anguko lake kisiasa.
 
......
kilichonishangaza zaidi ni ushiriki wa mzee lipumba kwenye sakata hilo. kuna baadhi ya wananchi ambao wanajua undani wa sakata hilo, wamedokeza kuwa IBRAHIM LIPUMBA, Mwenyekiti wa CUF amepewa fedha na makampuni ya mafuta yakiongozwa na kampuni ya AGGRECO, ili ahamasishe wananchi wa mtwara wagomee mpango wa serikali. pia mzee lipumba ameandaa watu wake ili hiyo kesho walete fujo na kupora mali za wananchi. inadaiwa kuwa makampuni hayo yanapinga mradi huo ili yaendelee kunufaika na biashara ya mafuta toka mataifa ya nje. makampuni hayo ya mafuta inadaiwa kuwa yanatumia fedha nyingi kuwanunua watu wenye ushawishi kwenye jamii ya wana mtwara ili kuchochea vurugu.
....

SOURCE: mimi mwenyewe

mi hapo kwenye hizo nyekundu ndio umeniacha, Mtwara wamegundua mafuta au gesi?!!, na je hata kama ni mafuta, hayatauzwa nchi nje?!
 
hii ya lipumba kuhusika kwenye hizo vurugu na baadhi ya wanasiasa wengine mimi nazijua ni kweli kabisa na sijui anakwenda wapi.
 
kama ni kweli sasa lipumba anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe na hili ndilo anguko lake kisiasa.

Aanguke mara ya ngapi? Huyu bwana ni mdini sana. Mfuatilie vizuri utaliona hili. He doesnt't behave like a learned person.:kev:
 
JK ni janga la kitaifa. Akifa nitafanya sherehe kubwa kufurahia kifo chake kwani ameliangamiza taifa letu.
mkuu dua la kuku halimpati mwewe unaweza kutangulia ukamwacha jk kwa sabu mungu siyo athumani kaka؛
 
[FONT=century
gothic]mi hapo kwenye hizo nyekundu ndio umeniacha, Mtwara wamegundua
mafuta au gesi?!!, na je hata kama ni mafuta, hayatauzwa nchi
nje?![/FONT]

mkuu, kwa taarifa yako, pale msimbati kwenye visima vya gesi, kumegundulika mafuta pia. pia utambue kuwa nishati ya gesi huambatana na nishati ya mafuta. pia hayo makampuni ya mafuta ndo hufanya biashara ya gesi. hivyo usishangae kuona kampuni kama aggreco wanapinga miradi ya serikali ya gesi kwa vile wanajua kuwa mwisho wa yote ni biashara ya mafuta
 
[FONT=century
gothic]mi hapo kwenye hizo nyekundu ndio umeniacha, Mtwara wamegundua
mafuta au gesi?!!, na je hata kama ni mafuta, hayatauzwa nchi
nje?![/FONT]

mkuu, pia kinachowauma zaidi ni kuona miradi hiyo wanasimamia wachina. upo uwezekano pia hata aggreco wanatumika tu kwa faida ya mataifa ya magharibi
 
''Kilichonishangaza zaidi ni ushiriki wa mzee Lipumba kwenye sakata hilo. kuna baadhi ya wananchi ambao wanajua undani wa sakata hilo, wamedokeza kuwa IBRAHIM LIPUMBA, Mwenyekiti wa CUF amepewa fedha na makampuni ya mafuta yakiongozwa na kampuni ya AGGRECO, ili ahamasishe wananchi wa mtwara wagomee mpango wa serikali. Pia mzee Lipumba ameandaa watu wake ili hiyo kesho walete fujo na kupora mali za wananchi. inadaiwa kuwa makampuni hayo yanapinga mradi huo ili yaendelee kunufaika na biashara ya mafuta toka mataifa ya nje. Makampuni hayo ya mafuta inadaiwa kuwa yanatumia fedha nyingi kuwanunua watu wenye ushawishi kwenye jamii ya wana Mtwara ili kuchochea vurugu. '' by lizabon

UMETUMWA NINI................., Maelezo yamejaa uongo mtupu......
 
hii ya lipumba kuhusika kwenye hizo vurugu na baadhi ya wanasiasa wengine mimi nazijua ni kweli kabisa na sijui anakwenda wapi.

mkuu, inadaiwa kuwa wanamtumia lipumba kwa vile yeye ndiye kiongozi wa chama cha upinzani mwenye ushawishi mkubwa sana kule mtwara
 
Tukubali tukatae lipumba na chama chake ni ndogo sana katika siasa za sasa na kama kaanza siasa za namna hii namtabilia kifo kisiasa hilo liko wazi.
 
wanasiasa siku zote wanapenda kuona shari na vurugu katika nchi badala ya kuhubiri amani
 
watanzania wanatumika kama punda kubeba na kuvusha malengo ya wanasiasa njaa
 
kama kweli lipumbaaaaaaa yupo nyuma ya hili basi amekwisha kisiasa
 
''Kilichonishangaza zaidi ni ushiriki wa mzee Lipumba kwenye sakata hilo. kuna baadhi ya wananchi ambao wanajua undani wa sakata hilo, wamedokeza kuwa IBRAHIM LIPUMBA, Mwenyekiti wa CUF amepewa fedha na makampuni ya mafuta yakiongozwa na kampuni ya AGGRECO, ili ahamasishe wananchi wa mtwara wagomee mpango wa serikali. Pia mzee Lipumba ameandaa watu wake ili hiyo kesho walete fujo na kupora mali za wananchi. inadaiwa kuwa makampuni hayo yanapinga mradi huo ili yaendelee kunufaika na biashara ya mafuta toka mataifa ya nje. Makampuni hayo ya mafuta inadaiwa kuwa yanatumia fedha nyingi kuwanunua watu wenye ushawishi kwenye jamii ya wana Mtwara ili kuchochea vurugu. '' by lizabon

UMETUMWA NINI................., Maelezo yamejaa uongo mtupu......

mkuu, hizo ni taarifa tu nilizopewa na mmoja wa wahusika wa maandalizi ya vurugu hizo. kwa nini hajataja kampuni kama camel oil badala yake kataja aggreco?
 
Back
Top Bottom