Lipumba: Ubaguzi kikwazo nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Ubaguzi kikwazo nchini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Dec 27, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba amesema nchi haiwezi kuwa na uzalendo wa kweli endapo ubaguzi utaendelea na matabaka katika utoaji wa elimu.
  Lipumba alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati akiwatakia watanzani heri ya sikukuu ya Krissmas na mwaka mpya huku akitolea mfano tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti wa elimu ikiwemo ya TWAWEZA.

  Alisema pamoja na serikali kufanikiwa kuingiza watoto wengi darasa la kwanza, utafiti huo unaeleza wanafunzi wengi wanamaliza shule za msingi bila kujifunza.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, watoto wengi hawajifunzi kusoma hadithi rahisi hadi wafikie darasa la 5 au 6 na hadi wanamaliza shule ya msingi mwanafunzi mmoja kati ya watano hawawezi kusoma hadithi ya ngazi ya darasa la 2.

  Alisema licha ya kumaliza miaka saba ya elimu ya msingi watoto hao wanabaki kuwa mbumbumbu wasiojua kusoma wala kuandika na wanafika darasa la saba bila kuwa na stadi zozote za Kiingereza.

  Alisema hii ina maana kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaoingia sekondari hawawezi kusoma kwa lugha ya kiingereza ambayo ni lugha ya kufundishia elimu hiyo.

  “Hadi kipindi wanafikia darasa tano, watoto wengi wanaweza kutoa na kujumlisha, lakini wengi bado hawawezi kuzidisha na wengi wao wanapata stadi za hisabati mwishoni mwa shule ya msingi na watoto watatu kati ya kumi wa darasa la saba bado hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za ngazi ya darasa la 2,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema sekondari za kata hazina walimu, vitabu, maktaba na maabara hivyo watoto wengi wanaingia sekondari bila elimu bora ya msingi.

  Alibainisha kuwa elimu wanayopewa watoto wengi haitawawezesha kuwa washindani kwenye soko la ajira katika dunia ya utandawazi.

  “Ubaguzi wa kitabaka katika elimu unazidi kuongezeka, watoto wa wakubwa na wenye kipato cha juu wanaenda ‘English medium primary na secondary schools’ watoto maskini wanaenda shule zisizokuwa na walimu wenye ari na motisha ya kufundisha,” alisema Profesa Lipumba.
   
 2. B

  Bull JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 4, 2008
  Messages: 984
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu kweli ni Prf, sio wakina Slaa na wenzake wanaoendeshwa na jazba na uchu wa madaraka!! Hongera Lipumba kwa adadisi wa kitaalam
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2010
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  lipumba ni mnafiki kama hayo yote anayajua je anautumia vipi u profesor kutatua matatizo hayo?anauzi kweli si angeunganisha nguvu na dr slaa ili wachukue nchi then awe prime minister?anachojua ni kuchongoa domo lake tu. Mstxszsh..
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sasa mnamtumiaje nyie majuha wa CCM? mmempa mwenzie mzanzibar ulaji yeye ni ganda la muwa mmetupa. Mmpo kumsifia wala hamna la maana hata mnaloweza kujifunza toka kwake. Hey nyie majuha kweli. Ndio maana unajiita bull sijui ni bull la P*g?.
   
 5. N

  Nonda JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,Kilimasera

  Unajitahidi kutuwekea habari hapa JF. Asante sana.
  Ushauri: kama habari hujaiandika wewe mwenyewe basi weka source yake mwishoni.
  Hii itaepusha watu kukumwangia upupu, wakifikiria wewe ndiye muandishi.
  Nililiona hilo kwenye thread moja. Ni ushauri tu,mkuu.
   
Loading...