Lipumba: Ubaguzi kikwazo nchini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Ubaguzi kikwazo nchini

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  Lipumba: Ubaguzi kikwazo nchini


  na Asha Bani


  [​IMG] MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba amesema nchi haiwezi kuwa na uzalendo wa kweli endapo ubaguzi utaendelea na matabaka katika utoaji wa elimu. Lipumba alisema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam, wakati akiwatakia watanzani heri ya sikukuu ya Krissmas na mwaka mpya huku akitolea mfano tafiti mbalimbali zilizofanywa na watafiti wa elimu ikiwemo ya TWAWEZA.
  Alisema pamoja na serikali kufanikiwa kuingiza watoto wengi darasa la kwanza, utafiti huo unaeleza wanafunzi wengi wanamaliza shule za msingi bila kujifunza.
  Kwa mujibu wa utafiti huo, watoto wengi hawajifunzi kusoma hadithi rahisi hadi wafikie darasa la 5 au 6 na hadi wanamaliza shule ya msingi mwanafunzi mmoja kati ya watano hawawezi kusoma hadithi ya ngazi ya darasa la 2.
  Alisema licha ya kumaliza miaka saba ya elimu ya msingi watoto hao wanabaki kuwa mbumbumbu wasiojua kusoma wala kuandika na wanafika darasa la saba bila kuwa na stadi zozote za Kiingereza.
  Alisema hii ina maana kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaoingia sekondari hawawezi kusoma kwa lugha ya kiingereza ambayo ni lugha ya kufundishia elimu hiyo.
  “Hadi kipindi wanafikia darasa tano, watoto wengi wanaweza kutoa na kujumlisha, lakini wengi bado hawawezi kuzidisha na wengi wao wanapata stadi za hisabati mwishoni mwa shule ya msingi na watoto watatu kati ya kumi wa darasa la saba bado hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za ngazi ya darasa la 2,” alisema Profesa Lipumba.
  Alisema sekondari za kata hazina walimu, vitabu, maktaba na maabara hivyo watoto wengi wanaingia sekondari bila elimu bora ya msingi.
  Alibainisha kuwa elimu wanayopewa watoto wengi haitawawezesha kuwa washindani kwenye soko la ajira katika dunia ya utandawazi.
  “Ubaguzi wa kitabaka katika elimu unazidi kuongezeka, watoto wa wakubwa na wenye kipato cha juu wanaenda ‘English medium primary na secondary schools’ watoto maskini wanaenda shule zisizokuwa na walimu wenye ari na motisha ya kufundisha,” alisema Profesa Lipumba.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,231
  Trophy Points: 280
  Tatizo la profesa Lipumba ni kulalamika bila ya kuwa na majawabu au mikakati ya utatuzi wa matatizo ya elimu yetu ambayo sote tunayaona..........................tuache lipi na tufanye nini.......ndiko tutatua matatizo ya matabaka kwenye jamii...................
   
 3. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  matabaka hayawezi kukosekana katika jamii yeyote hata yeye anaongea tu huku watoto waki si ajabu wakawa hata nje ya nchi . Suluhisho la hili tatizo ni kwanza kuzivunja hizo shule zote zenye gharama za anasa na pilii ni kuziboresha shule zote zinazoonekana kuwa za kawaida ili ziwavutie k watu wote si matajiri au MASIKINI .HAPO NDIPO UTAKAPO ONA HAO VIGOGO WAKIZITHAMINI HIZO SHULE ZA UMMA MAANA WANAJUA WATAWAPELEKA HATA WATOTO WAO ,LASIVYO MMH MLIE TU .
   
Loading...