Lipumba: Spika anafanya Upendeleo Bungeni.

sokoinei

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Posts
1,832
Reaction score
566
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba, amesema kwamba yanayotokea Bungeni ni matokeo ya KITI cha Spika kufanya upendeleo waziwazi, kwa kuwakandamiza Wabunge wa Upinzani!!

Alisema ni Vigumu sana Bungeni kuwepo utulivu kama kiti cha Spika kitaendelea kuwaonea Wabunge wa Upinzani!!

Source: Gazeti la Nipashe
 
Profesa naye awe mkweli; asitake kuzunguka mbali bila sababu. Badala ya neno wapinzani aweke neno sahihi. Nadhani hakusikia mbunge wa chama chake Habib Mnyaa alivyokuwa anamwaga pumba kwenye media baada ya lile tukio la aibu la kiti cha Spika.
 
Ni kweli kabisa, spika anachezea kiti
 
Ni ukweli ambao uko wazi, na spika siyo kwamba anafanya hivyo kwa bahati mbaya, ni mpango wa kupunguza kasi ya UPINZANI bungeni, na hayo na maelezo ya wakuu wake wa chama, ndiyo maana wabunge wa ccm badala ya kuchangia mijadala ya bajeti, wamekuwa watu wa kuipinga CHADEMA bila ya sababu za msingi, huku wakianalyze matatizo kibao kwenye majimbo yao na kisha kuinga mkono bajeti kwa asili mia zote!!! Huu ni unafiki ambao waliowachagua inabid waufahamu na wachukue hatua stahiki 2015. Vinginevyo tutakuwa na wabunge wanaoitetea serikali, yaani tunashindwa kabisa kutofautisha wabunge na mawaziri wa serikali!!!!
 
Wabunge wa Magamba woote ukiwatoa watatu, ni Mawaziri. Huenda hawajui majukumu yao kama wabunge.
 
Profesa naye awe mkweli; asitake kuzunguka mbali bila sababu. Badala ya neno wapinzani aweke neno sahihi. Nadhani hakusikia mbunge wa chama chake Habib Mnyaa alivyokuwa anamwaga pumba kwenye media baada ya lile tukio la aibu la kiti cha Spika.

Yale yalikuwa ni maoni ya huyo mbunge lakini haya ni maoni ya mwenyekiti wa CUF Prof. Haruna Lipumba.
Kwa hiyo maoni ya mwenyekiti yanasound sana.
 
Kumbe Profesa Lipumba hawachukii chadema ila wao chadema wanamchukia Profesa lipumba.

Kumbe sio profesa uchwara.

Sasa nauliza swali: Maprofesa kama hawa Tanzania tunao wangapi? Tunawaenzi vipi??
 
Sidhani nikikuomba ushahidi kuwa CHADEMA wanamchukia Prof. Lipumba unaweza kunipatia! Naomba nifanye hivyo bila kusita nipatie ushahidi kwa mifano thabiti. Kwa habari ya idadi ya Maprofesa nchini Tanzania tunao mamia na zaidi ya Prof. Lipumba wapo wengi mfano ni mchumi Prof. Lambilo anayefanya kazi STATE UNIVERSITY U.S.A. na mchumi Prof. Ndalikulumuye Harare University Zimbabwe.

Unamjua na kumuaminia zaidi Lipumba kwa kuwa ni mwanasiasa ambaye anasukumwa na karaktaristiks za kisiasa kupanda majukwaani na kwenye media ambapo ni rahisi kujinadi ukaingilika kuwa kama yeye ni adimu kumbe wapo kibao kimya kimya wanaendelea na mapambano ukombozi ukipatikana wanapanda Ikulu utawajua tu.
 
...Nadhani hakusikia mbunge wa chama chake Habib Mnyaa alivyokuwa anamwaga pumba kwenye media baada ya lile tukio la aibu la kiti cha Spika.
CUF ni vipande vipande, msimamo wa Mwenyekiti sio msimamo wa viongozi wengine, na kila mtu anaongea yake kwenye media
 
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba, amesema kwamba yanayotokea Bungeni ni matokeo ya KITI cha Spika kufanya upendeleo waziwazi, kwa kuwakandamiza Wabunge wa Upinzani!!

Alisema ni Vigumu sana Bungeni kuwepo utulivu kama kiti cha Spika kitaendelea kuwaonea Wabunge wa Upinzani!!

Source: Gazeti la Nipashe

Sawa. Lakini mimi sielewi huyu prof anafanya nini akiwa bungeni. kama anaona huyo spika anafanya hayo mambo yeye mbona aombi mwongozo ili tujue usomi wake una maana katika kuleta mabadiriko ktk nchi yetu! Sasa mimi ninazidi kuchoka na usomi katika siasa zetu!!!
baba wa taifa mwalimu Nyerere hakuwa prof na dr za kupewa alizikataa. Ndugu yetu mpendwa Sokoine hakuwa na hizo dr. zenu lkn kazi ilitendeka!!!
 
Wabunge wanatakiwa kuikosoa/ kuirekebisha serikali pale inapokwenda ndivyo sivyo , tofauti na sasa wabunge wa CCM wamekuwa wao ndo serikali
 
kuna siku alisikika pr.Lipumba akisema na kuapa kwenye mikutano yake kuwa, kamwe CHADEMA hawatingia ikulu. Sijui alimaanisha nini!!!
 
Kwa mtu mwenye akili timamu hatutegemei kusikia akishabikia kiti cha SPIKA hata kidogo
 
swala la upinzani wa tanzania kuonewa na kiti cha spika hata mtoto wangu wa darasa la pili A analitambua hilo
 
Sawa. Lakini mimi sielewi huyu prof anafanya nini akiwa bungeni. kama anaona huyo spika anafanya hayo mambo yeye mbona aombi mwongozo ili tujue usomi wake una maana katika kuleta mabadiriko ktk nchi yetu! Sasa mimi ninazidi kuchoka na usomi katika siasa zetu!!!
baba wa taifa mwalimu Nyerere hakuwa prof na dr za kupewa alizikataa. Ndugu yetu mpendwa Sokoine hakuwa na hizo dr. zenu lkn kazi ilitendeka!!!

Mkuu uko usingizini nn au ww siyo Mtz? Pr.Lipumba hayuko bungeni
 
Sawa. Lakini mimi sielewi huyu prof anafanya nini akiwa bungeni. kama anaona huyo spika anafanya hayo mambo yeye mbona aombi mwongozo ili tujue usomi wake una maana katika kuleta mabadiriko ktk nchi yetu! Sasa mimi ninazidi kuchoka na usomi katika siasa zetu!!!
baba wa taifa mwalimu Nyerere hakuwa prof na dr za kupewa alizikataa. Ndugu yetu mpendwa Sokoine hakuwa na hizo dr. zenu lkn kazi ilitendeka!!!

Duh hii kali! Lipumba mbunge tokea lini? talk about "kukurupuka"
 
Mwenyekiti wa CUF Prof Ibrahim Lipumba, amesema kwamba yanayotokea Bungeni ni matokeo ya KITI cha Spika kufanya upendeleo waziwazi, kwa kuwakandamiza Wabunge wa Upinzani!!

Alisema ni Vigumu sana Bungeni kuwepo utulivu kama kiti cha Spika kitaendelea kuwaonea Wabunge wa Upinzani!!

Source: Gazeti la Nipashe

Lipumba hapo atuweke sawa, spika na magamba hawana tatizo na vyama vya upinzani, wanatatizo na chadema, ye anaongea kwenye media wakat wabunge wake wameridhika na kinachoendelea mjengoni
 
Back
Top Bottom