.......Mercy/parole to thieves!The best President Tanzanians will never have....
Date::10/6/2008
Profesa Lipumba adai IMF inachochea ufisadi
Na Kizitto Noya
Mwananchi
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amelituhumu Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwamba linachochea na kuendekeza rushwa na ufisadi nchini.
Profesa Lipumba alitoa shutuma hizo nzito upitia barua yake aliyomwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Dominique Strauss-Khan.
Katika barua hiyo ambayo jana aliamua kuigawa kwa vyombo vya habari, Profesa Lipumba alidai amebaini kwmba IMF ambayo imekuwa ikiheshimika kwa miaka mingi, ina mkono katika matukio ya ufisadi yanayoendelea hapa nchini.
Alisema amebaini hilo kutokana na shirika hilo kufumbia macho matukio kadhaa ya ufisadi nchini na kitendo chake cha kumpongeza Rais Jakaya Kikwete kwa hatua ya kuwapa muda wa kurejesha fedha mafisadi wa EPA badala ya kumponda.
Sikusoma popote zaidi kujiridhisha kwamba ulisema, niliamini kwamba taarifa iliyotolewa na gazeti la serikali hapa nchini, The Daily News kuhusu mazungumzo yako na Rais Kikwete ni sahihi. Kauli yako inachochea rushwa na kuendekeza ufisadi Tanzania, alisema Profesa Lipumba katika barua hiyo ya Septemba 26, mwaka huu yenye kumbukumbu namba CUF/AK/ DSM/MKT/001/IMF/2008.
Septemba mosi mwaka huu, gazeti la Daily News lilimkariri Mkurugenzi Mtendaji wa IMF akimsifia rais Jakaya Kikwete kwa hatua alizochukua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wa EPA.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, katika mkutano wao uliofanyika kwenye hoteli ya Omni Shoreham, nchini Marekani, Mkurugenzi huyo wa IMF alisema Tumeridhirika sana na kukupongeza jinsi ulivyoshughulikia suala la EPA. Suala hilo linaweza kutokea popote duniani lakini cha msingi ni jinsi ulivyolishughulikia. Na umelishughulikia vizuri kwa umahiri na utalaam wa hali ya juu. IMF sasa imefunga suala la EPA,
Profesa Lipumba alisema kauli hiyo ya IMF, inachochea rushwa kwani ni ukweli usiofichika kwamba serikali imeshindwa kushughulikia suala hilo kwa umahiri wala utaalam wa hali ya juu kama mkurugenzi huyo anavyodai.
Akifafanua alisema: Serikali haikuwa wazi kuueleza umma jinsi fedha hizo zilivyochotwa, watuhumiwa bado hawajulikani kwa majina na makampuni hayajafikishwa mahakamani,
Kwa mujibu wa Profesa Lipumba kitendo cha Rais Kikwete kutaka watuhumiwa wa ufisadi wa EPA warejeshe fedha, kinaleta shaka kuwa hatawafikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili, kitendo ambacho ni kinyume na utawala bora na sheria.
Alisema rais Kikwete amewasamehe watuhumiwa wa EPA na kauli yake haionyeshi nia thabiti ya serikali kuwafikisha mahakamani hivyo kumsifu kwamba amelishughulikia suala hilo kwa umahiri sio sahihi.
Aliitaka IMF kuongeza umakini katika kupitia hali ya uchumi wa Tanzania katika vikao vyake vijavyo na kuishikiza serikali kusimamia mapendekezo ya ripoti ya awali iliyokagua akaunti ya EPA mwaka 2006 iliyotaka nchi iache kuendelea kulipa madeni hayo kwa kuwa yamepitwa na wakati.
Katika hatua nyingine Profesa Lipumba jana ameeleza kuwa msimamo wa chama chake kuandamana kwa lengo la kuishinikiza serikali itaje majina ya watuhumiwa wa EPA na kuwafikisha mahakamani, uko palepale.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa maandamano hayo yamepangwa kufanyika Oktoba 6 mwaka huu kuanzia Buguruni kupitia barabara ya Uhuru hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambako viongozi wakuu wa CUF watahutubia.
Profesa Lipumba alibainisha kuwa ingawa polisi wameshajulishwa kuhusu maandamano hayo, baadhi ya watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala wameanza kuyawekea mizengwe kwa kuzuia viwanja hivyo.
Alisema baada ya CUF kumwandikia barua mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kumjulisha juu ya maandamano hayo kuishi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, aliwajibu kwa barua kwamba viwanja hivyo haviruhusiwi kwa shughuli za kisiasa.
huyu naye keshaishiwa
angeanza na bilateral agreements kama tulizo nazo na waingereza kupitia dfid ambao wana chochea ufisadi zaidi tanzania kuliko hao imf
mchumi mzima anaboa
Huyu naye keshaishiwa
angeanza na bilateral agreements kama tulizo nazo na waingereza kupitia DFID ambao wana chochea ufisadi zaidi Tanzania kuliko hao IMF
mchumi mzima anaboa
By Beatus KagasheCivic United Front national chairman Ibrahim Lipumba yesterday criticised the International Momentary Fund (IMF) over its approval of Tanzania's war on corruption.
Prof Lipumba said the opposition party had been 'shocked' by reports that the IMF recently praised the Government's handling of the Sh133 billion EPA scandal.
The CUF chairman has written to IMF managing director Dominique Strauss-Kahn to protest the manner in which the institution viewed good governance in Tanzania.
The letter was copied to President Jakaya Kikwete and other development partners. In the letter, Prof Lipumba, who is an economist, said they were not satisfied with measures taken by the Government in dealing with the EPA scandal suspects.
Speaking in Dar es Salaam yesterday, Prof Lipumba said IMF must not support President Kikwete's government because measures taken so far 'are not enough'.
On September 1, the IMF was quoted in the local media as saying that it was satisfied with the way the Government was handling the EPA scandal in which the Bank of Tanzania made dubious payments totalling Sh133 million to 22 shadowy firms.
Mr Strauss-Kahn repeated IMF's position when he recently met President Kikwete in the US.
The IMF director was reported as saying: "We are satisfied and congratulate you for the way you handled the issue. This thing can happen anywhere in the world. What is important is the way it is being handled. And you have handled it very well, with competence and professionalism of highest order. The EPA case is now closed as far as IMF is concerned."
But Prof Lipumba said the Government has not been transparent in informing the public about the looting of public funds through the EPA account.
"It is high time the IMF showed that it is supporting Tanzania to fight grand corruption and not supporting minor steps it must make sure all the money is returned," he said.
President Kikwete told Parliament in August that suspects in the EPA scandals were required to return cash paid to them irregularly by October 31 of face prosecution.
Prof Lipumba said the President's decision to give more time to those implicated to return the money was a sign of failure.
"Giving them more time is treating them like ordinary people who have borrowed money from saccos (savings and credit cooperative societies) these are thieves twho must be prosecuted," he said.
Prof Lipumba warned that moving the EPA account from BoT to a commercial bank would prevent auditors from certifying whether the funds had been recovered or not.
"It's highly suspicious that funds recovered from EPA suspects should be deposited outside BoT, which is supposed to be the custodian of State funds."
Prof Lipumba added that CUF was planning to hold a peaceful demonstration on Thursday to press for the revelation of the names of EPA suspects and their prosecution.
"The aim is to let the President know that his handling of EPA suspects is contrary to the people's wishes these people must be made to face the full force of the law."
Huyu poor profesa amechoka kufikiri..
Huyu poor profesa amechoka kufikiri..
Kikwete ameamua kutokuwachukulia hatua za kisheria watu waliohusika na EPA, skandali ambalo yeye alionyesha bungeni kwamba lilikuwa ni ufisadi. Kwa maneno mengine amewasamehe.
IMF imesema Kikwete ame handle vizuri scandle la EPA.
Profesa Lipumba akasema IMF wanachochea ufisadi kwa kumpongeza Kikwete kwa sababu hizo hatua za Kikwete hazitoshi.
Sasa huyu "poor profesa" amechoka vipi kufikiri hapo ?
unajua kuna mtu aliwahi kuniuliza idadi ya marais duniani wanaoitwa ma professa nikashindwa kuwataja hata mmoja labda OBAMA akiwa rais maana university of Chicago wamesema alikuwa ni professor
Huyu Lipumba kusema ukweli ni disgrace na alizidi kuwa disgrace pale alipokuwa akikampeni nchi za Scandinavia zitukatie misaada in the 90's
saya alot about where his priorities are
ngja tukishamaliza na Mbowe itabidi tuhamie kwa hili kubwa jinga
Kumbe hili lijamaa ni mashoto...
You are missing the point
kagombea urais 1995 kashindwa
kagombea tena 2005 kashindwa
sasa bado anataka kugomea urais
sasa kama kweli angekuwa na akili na alitaka awe taken serious then ilitakiwa akae pembeni awapishe wenzie.
Nimesema angetuletea info jinsi DFID TANZANIA wanavyochochoea ubadhirifu na ufisadi ningemwona wa maana lakini Lupumba comes across as another useless professors tulionao ambaye at most he is good for nothing really
Anhaa, kumbe mlikuwa mnaongelea criticisms za jumla jumla mlizonazo dhidi ya Lipumba. Oh yeah, hata mimi nina misgivings zangu dhidi yake, haswa hilo la kuwa mgombea wa kudumu wa CHADEMA. Nilifikiri mnaongelea hili lililoletwa kwenye mada hapa, ambalo naona Lipumba yuko picture perfectly correct:
Kikwete kasamehe wahusika wa alicholionyesha Bunge kuwa ni ufisadi. IMF ikampongeza Kikwete kwa jinsi alivyo handle skandali la EPA. Profesa Lipumba akasema IMF wanachochea ufisadi kwa kupigia debe hatua ambazo hazitoshi. Exquisite point.
Nyinyi mnasema Profesa kachoka kufikiri. Kumbe mnaongelea yenu mengine. Yes, to the extent that you were just venting unrelated frustrations then I missed the point, you are right.