Lipumba: Nilidhani ni zamu yangu kuanguaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: Nilidhani ni zamu yangu kuanguaka

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Quinine, Aug 26, 2010.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,936
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba, jana aliuacha hoi umati wa wanachama wake waliokuwa wamefurika katika mkutano wa kampeni wa chama hicho baada ya Mgombea Udiwani wa Vingunguti, Ally Omary, kutikisa jukwaa lake na kuliyumbisha.

  Lipumba alipigwa na butwaa na kuuchekesha umati wa watu akidai kuwa alidhani naye zamu yake ya kuanguka imefika, hali ambayo iliwafanya wananchi waliokuwa wamefurika katika viwanja vya Buguruni Kisiwani kuangua vicheko.

  “Enh, ndugu yangu umenishtua sana baada ya kunyanyuka na kupanda jukwaani kwani niliona linayumba nikapata hofu sana nikasema leo nadhani nami zamu yangu imefika,” alisema Lipumba.

  Lipumba aliyasema hayo bila kutaja nani mwingine aliyeanguka wakati akiendelea na utambulisho wa wagombea wa nafasi ya Ubunge na Udiwani kwa tiketi ya chama hicho ambapo mkutano huo uliandaliwa na mgombea Ubunge Jimbo la Segerea, Ayoub Kimangale.
   
 2. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  .
  Duh!! 90 + 15 +5 sawa sawa na asilimia ngapi ya nini?
   
Loading...