Inawezekanaje pro Lipumba awe ccm wakati mtu huyu alifikia kupigwa na kuumizwa mkono kwa ajili ya kutetea wanyonge.. NANI ANAKUBALI KUUMIZA MWILI WAKE HALAFU AWE MAMLUKI... haiwezekani. sijaona viongozi wa upinzani walioteswa saana isipokuwa CUF...
-Mdau mmoja humu kaponda kuchaguliwa Lipumba kwa asilimia kubwa,na ati pr Safari kasusa.. Kwanza kuchaguliwa kwa ushindi mkubwa ndani ya cuf ni ushahidi tosha kua wanachama wanamkubali kwa kitendo chake cha kua mkweli na muadilifu.. Amejitahidi saana kukisambaza chama,amehangaika saana,kwa wanaomfatilia wanajua jinsi gani alivopata tabu hata kwenda kwa miguu kwa masafa marefu vijijini huku akikutana na vikwazo vingi vya ccm.. Na kuhusu pr. safari fatilia uzuri ndugu yangu nini kilichomkwamisha,pamoja na kua Lipumba anakubalika lkn ndani ya mkutano wa wanachama kabla ya uchaguzi pr. safari aliulizwa masuala muhimu alishindwa kujibu... hiyo ni miongoni mwa sababu tu...
-Mdau mwengine amechangia humu kwa kusema ati ajenda ya muafaka.pale ndo kafeli.. Ndugu yangu ccm tunaijua na kwa kauli hadharani wanasema serikali haitoki kwa karatasi.. tuliona waznz walivyoteswa,wakati wa uchaguzi jeshi lilikuwa kubwa kuliko hao wananchi,nilikuwepo kwenda kushuhudia,sikuwahi kuona machoni.. Ilifikia wa znz kuzungukwa muda wa siku tatu mtendeni hali ya kuwa wamefunga,hiyo ndio ccm.. kama Lipumba hana kosa bali muafaka ni wa cuf wote na baraza kuu ndilo linaloamua,kwa unafiki wa ccm ndio waliokataa.. Heko kwa cuf na Lipumba waliwavuta ccm mpaka wakakwama wao,na hapo cuf ndio ikajitoa wakati watz wote wanaona ccm ndio iliokataa,na kujua unafiki wao... CUF ni watu wa busara lkn ccm ni wauaji..
-Mdau huyo huyo akasema ati Lipumba kafeli kwa muafaka wakati wenzake kina zito,slaa wameanzisha mada ya ufisadi na kuja juu... Ndugu yangu upo TZ au upo nje?... Siku ya kwanza kujua habari ya ufisadi wa serikali yetu nilikuwa kenya,nikapewa karatasi ambazo zinaelezea ufisadi wa tz... nilivorudi TZ,baada ya miezi kama 6 Nikamsikia Pr Lipumba anazungumzia ufisadi na mafisadi mbele ya waandishi wa habari.. ndo mara ya kwanza tz kutajwa hadharani kuhusu ufisadi,baadae ndipo wakaja mashujaa wetu wengine kina Slaa na Zitto... nitafute kwa wakati wako nitakupa vitu kwa tarehe... Na mpaka sasa hakuna mwengine alietaja moja kwa moja kua Rais Kikwete anahusika na ufisadi isipokua Lipumba pekee... Njoo nikupe kanda..
-Mdau mwengine kasema kaungana na ccm na mkuchika kupinga ufisadi ulotajwa na mengi.. Baba amka!!!!! kwanza Hata viongozi wengine wa upinzani akiwemo mrema walimpinga Mengi... wote hawa hawakupinga ufisadi bali wamepinga njia alizotumia Bw Mengi,pamoja na maneno makali aloyatoa kwa umma.. Kama kapinga ufisadi inakuwaje ameanzisha yeye mada ya ufisadi... kua makini baba,fatilia uzuri...
-Mdau mwengine amesema kumwambia zitto awaambie wananchi wa busanda wasichague ccm,cuf nk kwani hao hawafai.. kwa upande wangu ikichukua chadema au cuf nitafurahi yote sawa lkn sio ccm.. laiti habari za cuf zingekua zinatolewa kama inavotolewa ccm na chadema ungeona jinsi gani cuf ina nguvu mikoani lkn kwa uoga wa ccm dhidi ya Cuf wamefanya kila njia kuhakikisha cuf haitajwi sana habari zake,wapo tayari chadema watajwe kuliko cuf.. Yote hii ni kwa sababu wanaiogopa Cuf...