Lipumba na Maendeleo ya CUF... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba na Maendeleo ya CUF...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Topical, Feb 12, 2012.

 1. T

  Topical JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Prof. Lipumba yuko nchini merakani kwa mwaliko wa taasisi ya National for Democracy endowment, ameombwa kutoa mada juu ujenzi ya taasisi ya kidemokrasia nchini Tanzania; mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 500 kutoka nchi mbalimbali duniani. Amekuwepo huko Tangu october 2011 akitoa mada mbalimbali..

  Akiongelea maendeleo ya CUF amesema chama Tawala kinahujumu matokea halali ya kidemokrasia Tanzania kwasababu hakuna tume huru, wala hakuna tofauti kati ya chama Tawala na vyombo vya dola. Hata hivyo amesema CUF imepata mafanikio makubwa kwa upande wa Zanzibar kwa kuweza kushiriki katika serikali ya kitaifa na kupunguza uhasama wa kisiasa na mauaji wa raia unaofanywa kila baada ya uchaguzi. Kwa ujumla anasema CUF kina wabunge 24 wa kuchaguliwa na wananchi 22 kutoka Zanzibar na 2 kutoka Tanzania Bara, amesisitiza kuwa tume ingekuwa huru wangepata zaidi ya hao wabunge....

  Akiongolea issue HR amesema, HR ana nia mbaya ya kuhujumu na kudhoofisha chama, kwakuwa HR ni kiongozi na anajua taratibu za kujaza nafasi za uongozi, alishiriki kuzitunga, akasisitiza kuwa chama imara ni kile ambacho viongozi wake hawayumbishwi na mwanachama yeyote na wanasimamia NIDHAMU kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama... Aliyataja makosa ya HR kuwa ni pamoja na a. Kufanya mikutano ya ndani ya chama bila kufuata taratibu b. kutuhumu viongozi wa chama kwa mambo ambayo si ya kweli c. kupinga mambo yaliyokubaliwa katika vikao halali vya chama hivyo kudhoofisha collectively responsibility ili kujenga chama d. kukataa kuhudhuria katika vikao halali vya chama; hivyo yeye anasema anaafiki kuondolewa katika chama kwani hana nia njema kwani alioongea naye kabla ya kuondoka wakakubaliana kuwa atafuata taratibu zote za chama bila kudhoofisha na kuwachanganya wanachama kugombea uongozi...

  Akiongelea changamoto zinazoikabili CUF kwa sasa alisema; kwanza ni TUME huru ya uchaguzi na pili MEDIA BOYCCOT; amesema chama chake mainstream media wamekuwa hawaongolei kazi za chama chake japo wamejitahidi kuelimisha wananchi, hata hivyo wanampango wa kubadilisha mbinu ili kuweza kuhakikisha wanawafikia wananchi..

  mahojiano kamili -michuzi blog...(source)..
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Topical,
  Ni National Endowment for Democracy.
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  "Nchi hii muachie Mnyamwezi"
   
 4. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wapo kwenye coalition kwa nini wasishauri ndani kwa ndani au terms and conditions za ushirikiano ni zipi sasa?
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa mfano kwenye issue gani?
   
Loading...