lipumba na hamu ya kupendwa uzeeni

lipumba na hamu ya kupendwa uzeeni

2013

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2011
Posts
11,365
Reaction score
6,085
lipumba ametawala vichwa vya habari kwa kauli zake. kiukweli aliutamani urais wa tanzania na kwa bahati mbaya ama nzuri hakuweza kuwa rahisi, namfahamu kama profesa mchumi lakini asiye na mvuto katika maneno na alipokuwa akiongoza chama sikumwona kama mwenye sauti zaidi ya kuona mshiriki mwenzake wa zanzibar kama mwenye sauti zaidi katika chama chake chenye kupewa alama za sii(C), yuuu, ef(F). umri umemtupa mkono mzee huyu amesha-ahidi kutogombea urais 2015, lakini anatamani kupendwa na anahisi elimu yake haijasaidia imani yake labda ndio maana amegeukia dini ili kupata ushawishi na kurudisha mvuto wake wa zamani. akiwa kama mtanzania yoyote yule ameanza kuonyesha ngozi yake ya ndani, kwa matamshi yake. japo sijajua kwanini ccm inaitwa chama chenye udini pengine ndoa yake na cuf ilipelekea hili kujitokeza na wangekuwa wao pekeyao wasingekuwa na matatizo hayo.pia si ajabu hata haya ayasemayo profu huyu yanatokana na presha ndani ya chama chake ndio maana kayasema, manake hata kama yana ukweli kwa elimu yake nadhani hakustahili kuyasema hata kama anayajua. nahisi amegeuka mwanaharakati mzee zaidi akitaka bado kukubalika miongoni mwa watu wake wa karibu na chama chake ambacho nahisi kimemchoka sasa na kingetaka mabadiliko kama ya chadema na ccm. inashangaza sana kudai amemsaidia kikwete wakati yeye mwenyewe aligombea urais, siwezi kukataa kwasababu amesema. nadhani watanzania wa sasa tunaamini wasomi na hatutegemei kuwa na wasomi wanaozeeka katika hali mbaya kama hii. upigwaji marufuku udini na serikali unatakiwa uchukue hatua na uswahiba uwekwe kando kama anakosa amelifanya kwa kauli zake na sio kusubiri upande mwingine wa dini ndipo hatua zichukuliwa kwa urari. mungu ibariki tanzania.
 
Back
Top Bottom