Lipumba: JK atamaliza urais vibaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: JK atamaliza urais vibaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fangfangjt, Mar 21, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Lipumba: JK atamaliza urais vibaya

  Burhani Yakub,Tanga

  CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema Rais Jakaya Kikwete atamaliza muda wake akiwa ameshindwa vibaya kusimamia shughuli za Taifa la Tanzania.

  Alisema endapo Rais Kikwete anataka kukumbukwa katika historia, atumie muda uliobaki katika kuhakikisha katiba inafanyiwa marekebisho na tume ya uchaguzi inakuwa huru.

  Ushauri huo ulitolewa jana na Mwenyekiti wa CUF,Profesa Ibrahimu Lipumba wakati akizindua kitaifa oparesheni Zinduka katika viwanja vya Tangamano jijini Tanga.

  Alisema kati ya marais waliomtangulia kuongoza Tanzania kuanzia awamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere hakuna rais aliyeshindwa vibaya kusimamia masuala ya kitaifa kama Rais Jakaya Kikwete, tofauti na matarajio ya wananchi ambao walikuwa na imani kubwa wakati wakimchagua mwaka 2005.

  “Kikwete ameshindwa kusimamia elimu ameweka rekodi ya kufelisha wanafunzi wa kidato cha nne ambayo haijawahi kutokea tangu tupate uhuru,kwenye afya mambo ni magumu katika uchumi, huko hakusemeki
  ameshindwa kuzuia mfumuko wa bei, mpaka sasa umeme ni ngonjera tu miaka 50 ya uhuru Tanzania iko gizani,”alisema Lipumba.

  Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mchumi alisema chanzo cha kuanguka kwa uchumi wa Tanzania ni baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwadhibiti mapapa wa rushwa na ufisadi nchini akiwaogopa na kuwaacha wafanye wanachotaka jambo ambalo limewakatisha tama wananchi.

  “Utawala wa Kikwete unakabiliwa na ombwe la uongozi, na hii inatokana na mfumo wa CCM ambao ameshindwa kila kitu,lakini kwa ushauri wangu ni kuwa kama anataka akumbukwe na historia basi ajikite zaidi katika kusimamia
  marekebisho ya katiba na tume ya uchaguzi”alisema Lipumba.

  Alisema jambo pekee ambalo Rais Kikwete ameanza kulisimamia ni kulivalia njuga suala la marekebisho ya katiba kwa kuhakikisha inabalishwa kulingana na matakwa ya Watanzania na si vinginevyo.

  Lipumba alisema mchakato wa katiba unatakiwa uanze haraka ili kutoa fursa kwa Watanzania kuchangia maoni yao, lakini alisisitiza kuwa inatakiwa kwenda sambamba na kuunda tume ya uchaguzi ili huru na siyo kuwa na katiba ya sasa ambayo inafanya kazi ya kuchakachua kura na matokeo.

  “Tume iliyopo haifai, hata kwenye tovuti yake haiandiki idadi halisi ya wapiga kura, imechakachua hadi daftari la wapiga kura, tunataka tume isiyowatumia watendaji wa Halmashauri wakiwamo wakurugenzi watendaji
  na maofisa watendaji,”alisema Lipumba ambaye aaliambatana na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad Rashid Mohamed.

  Aliwata wananchi kutumia fursa hiyo kwa kujitokeza kutoa maoni ya marekebisho ya katiba kwa kuwa ni haki yao na kwamba wahakikishe wanapendekeza masuala muhimu yenye kuligusa Taifa.

  Kuhusu suala la kufanya maandamano na mikutano ya hadhara,Lipumba alisema ni haki ya vyama vya siasa na wananchi kuandamana kudai marekebisho ya katiba na kulalamikia mambo ambayo haendi sawa kutokana na uzembe wa viongozi wa Serikali ya CCM.

  Aliwaasa wananchi kujihadhari na kauli zinazotolewa na baadhi ya viongozi wanaosema Tanzania haitatawalika na kwamba kinachotakiwa ni kufuata taratibu kwani Serikali iliyopo itang’olewa madarakani kwa kura na siyo vurugu.

  “Msikubali kushabikia kauli zenye kuashiria vurugu,kama tusipoangalia tutasababisha CCM iendelee kushika dola,napenda kuwaeleza kuwa CCM imeshafikia mwisho tutaing’oa kwa kufuata taratibu”alisema Lipumba.
   
 2. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Naomba aliyemwelewa Prof Lipumba anisaidie:
  1. Anadai tume haifai kwa sababu inachakachua hadi daftari la wapiga kura lakini bado anaamini serikali iliyopo itang'olewa kwa kutumia kufuata taratibu za kura.
  2. Anasema maandamo ni sawa ila vurugu na kauli za kuashiria vurugu hapana. Maandamano pekee ambayo yamekuwa gumzo kwa taifa hili ni yale ya CDM. Sasa ni kauli zipi zilizotolewa zenye kuashiria vurugu? CCM hawajaweza kuziorodhesha! Na polisi hawajaweza kusema lolote maana walikuwepo kwenye maandamano. Ni vurugu zipi zilizotokea kwenye maandamano isipokuwa zile za Arusha ambazo sote tunajua aliyezianzisha. Kama si jeshi la polisi kunsingekuwa na yote yaliyotokea. Uthibitisho upo. Siku ya maziko ya wahanga wa Arusha, polisi walisusia kazi yao lakini hakukuwa na vurugu yoyote. Maandamano ya kanda ya ziwa kwa siku zote yamekuwa ya amani kabisa. Sasa ni vurugu zipi?
  3. Je, anauma na kupuliza kwa sababu alikuwa na Hamad Rashid mwenye uchu wa madaraka? Ambaye yuko tayari kupindisha kanuni kwa maslahi yake binafsi. Alifanya hivyo 1995 kwa kuongeza neno 'Kambi rasmi' ili kuitoa nje NCCR; na amefanya hivyo mwaka huu kwa kuongeza tafsiri ya Kambi rasmi.
  Naomba nisaidiwe kumwelewa Prof. Lipumba
   
 3. JUST

  JUST JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 554
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  NIMEPOTEZA:
  mimi ni pro. pumba, naongea zote pumba,
  kama vile muuza mitumba, mawazo yangu hayawezi kuumba,
  nimeshapoteza ile yangu rumba, naomba zake kudra muumba,
  nimepoteza nasema nimepoteza, uongozi wa nchi kwangu mwiko.

  mimi naanzia kunani, labda dira chamani yaweza rudi,
  nafuatani na wangu makuhani, japo najua ni wazandiki na wakurdi,
  napenda yangu maisha mazuri kibandani, hivyo nakiri kuwa mnafiki zaidi na zaidi,
  nimepoteza nasema nimepoteza, uongozi wa nchi kwangu mwiko.

  naumia sana roho, wenzangu wakishangiliwa,
  nibora niwakabe koo, japokuwa hwana la kulaumiwa,
  acha nitafute ukoo, angalau nipate japo ganda la muwa,
  nimepoteza nasema nimepoteza, uongozi wa nchi kwangu mwisho.
   
 4. s

  shujaa Member

  #4
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Watanzania hawahitaji marekebisho ya katiba, wanahitaji katiba mpya.
   
 5. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Inaelekea siku hizi mheshimiwa Lipumba ana tafuta pa kutokea hapati. Ana tafuta kwa bidii ujumbe uta kao uza chama chake na yeye mwenyewe. Tatizo ana ongea sana mpaka hatujui what he stands for and who he stands by. Yani siku hizi kawa Mr. Contradiction.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kauli ya Lipumba inaonyesha wazi ya kuwa ukweli anaujua, lakini kwakuwa nguvu ya CUF iko visiwani, na visiwa hivyo vimekwishaamua kuwa kitu kimoja na CCM, Lipumba anajikuta analazimika kuuma na kupuliza mara zote anapozungumzia hali ya kisisa nchini. Kwa hali hiyo, kama alivyomtabiria JK na yeye uenda akamaliza vibaya.
   
 7. domo bwakubwaku

  domo bwakubwaku Member

  #7
  Mar 21, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  harity should begin at home men wanyamwezi wenzake hawataki hata kumsikia sasa sijui nyie mnatakaje
   
 8. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  ukifatilia cables za WikiLeaks (ya HOSEA na USULUHISHO wa ZNZ) utaona Rais maamuzi yake mengi ni ya kisiasa zaidi, kila mara anawalinda na kujaribu kutokasirisha watu wakaribu na kuweka maslahi ya taifa pembeni, kama ni njia yakujitengenezea maisha mazuri akimaliza muda wake sijui, lakini ni bora afanye maamuzi magumu kwa maslahi ya taifa ambayo atayatetea hata miaka 50 ijayo , kama Nyerere, hata kama ameharibu , bado anaweza kuelezea bila woga na watu wakaelewa na kuheshimu! lakini hii ya kubeba watu ambao hawabebebki ni kama kukopesha mtu asiye kopesheka, utajitetea nini pale haupo madarakani na watu wamekubana ?
   
 9. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yaonekana mtunga mashairi mzuri weyye yakhe, khabari za umchicha mwiba vipi ?
   
 10. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nimekusoma na nimekupiga thanx. Ni vile tu ngonjera/ ushairi ulinipitia pembeni, ningekupiga ubeti wa shukurani
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,638
  Likes Received: 1,427
  Trophy Points: 280
  kwani huyo JK alianza urais vizuri lini mpaka waseme atamaliza vibaya? sorry am not gettin the point here
   
 12. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,330
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nimebaki na maswali mengi kuliko majibu! Huu ni mtazamo wake au ni wa chama chake? Kama ni wa chama, inamaana cuf wanataka marekebisho ya katiba na sio katiba mpya? Jk anatakiwa kutimiza ahadi/wajibu wake au afanye "mambo" ya kukumbukwa? Mi naamini kwamba JKatakumbukwa sana na watz. Ni rais aliyeshindwa vibaya sana kuongoza taifa hili. Ni rais aliyepata uongozi licha ya kushinwa uchaguzi. Ni rais anayeondoka madarakani na chama chake. Ni rais wa kwanza atakayekabidhi upinzani madaraka kwa nguvu ya umma. Ana mengi tu ya kukumbukwa wala haitaji kufanya "mambo" mengine!
   
 13. S

  Shkh Yahya Senior Member

  #13
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  With due respect..Lipumba is the most capale,competent and a very influentital Politicia. Anamvuto mkubwa akiongea..hatumii jazba kufikisha ujumbe wala uzushi na data za mitandao ya jamii. Nyote mtakumbuka hamasa ya CUF mwaka 2005 na kibano walichukowa wakikipata..

  kwa kuwa mahusiano yao na anahabari hayakuwa mazuri hawakupewa airtime yakotosha, magazeti hayakuwa yakiandika habari zao..mpaka wakawa wanatumia mikanda ya video kuonyesha harakato zao za kisiasa na mikanda hiyo kusafirishwa kutoka mkoa hadi mkoa,wilaya hadi wilaya..n.k.

  Kasoro yake na ni moja tu, jina lake la kwanza na chama anachikiongoza. CCM wote..wale CCM asili ( wa piga ua) na hawa walio defect na kuingia CDM temporarily... walishiriki kuihusisha CUF na udini. Mwaka 2000 na 2005 ambapo hii hoja inayozungumzwa leo ya eti ndoa ya CCM na CUF kama njia ya kuibeza CUF na kuiita CCMB ikiwa bado...watu hawa hawa ambao leo wana kauli hizi walikataa kuiunga mkono CUF simply kwa sababu ya jina la mgombea wao.

  Leo wamepata sababu ya maridhiano ya CUF na CCM tena kule Zanzibar na wanataka watu waamini kuwa eti CUF sio wapinzani. Shida hapa ni udini tu..na ndio maana kuna watu wanaandika na kushangaa kwa nini Julius (Mtatiro) akawa yuko CUF... wakiamini kama Julius yeye kwake ni CDM tu..kama ilivyo kwa John(Mnyika), Wilbroad (Slaa), Freeman (Mbowe),n.k.,n.k

  The botomline hapa ni udini tu...mimi nasema if ana only if CCM mambo yakibadilika..safu ya uongozi ikikaa vizuri..then no one will bother kwenda CDM. CCM itarudi kama mwanzo na hata kina baba Askofu wataanza kusifia tena.

  Shkh Yahya.
   
 14. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Hili ndiyo tatizo la kusoma kwa kukariri hence short memory.

  Lakini hatutachoka kukuelimisha/kukumbusha. FYI Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 CDM haikusimamisha mgombea wa kiti cha urais wa JMT. CDM walimuunga mkono mgombea wa CUF Prof. Ibrahimu Haruna Lipumba. (ask CUF zealots will tell the same). Lakini wale ambao hawaani redio IMANI

  Waliokibatiza CUF = Chama cha Udini na Fujo si CDM ni CCM muulize hata Maalimu Seif atakwambia.

  Taking that FACTS into accounts WADINI hapa ni CCM no wonder sasa hivi wamekibatiza CDM= Chama Cha Wakatoliki.

  The sad story of this ni kwamba hata wewe umekuwa manipulated na brainwashed with CCM cheap politics of DIVIDE AND RULE
   
 15. S

  Shkh Yahya Senior Member

  #15
  Mar 21, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 100
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0

  I talked of the whole system na the political wave ya nchi yetu..ni udini tu. The reason kama CDM hawakusimamisha mgombea kuiunga mkono CUF ni debetable...,they may simply have decided not to have Presidential candidate as they didnot have one.

  Simply haiwezekani..Lipumba ashindwe na Peter Mziray in more than half a century of consituencies...ah!!! hapa simply hii nchi imejaa udini tu....

  Nak nikisema udini najua unamaanisha nini !!!
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  yahya una ukweli ndani yako,la kusema cdm wameiita cuf kwa udini ni uongo usiohitajika. Mwaka 2005 aliyekwenda Tbc by then TvT kusema kuwa cuf ni wadini,wajaidina na magaidi ni Mkurugenzi ktk sekta ya utalii ndg.OMAR MAHITA,pia jk na nazir karamagi akisaidiwa na na akina Daniel Yona na Ibrahimu Msabaha,walikamata visu vyenye nembo ya cuf bandia na kuihusisha cuf na kuingiza silaha za vita,je hapa udini ni nini?kwamba mtu akiipinga cuf au mtu kuwa dini tofauti akampinga aliye chama cha cuf?je baada ya hapo walimchagua rais wa dini ipi kama walikuwa wadini? Ujue mnachukua maneno ya watawala mafisadi na kuyakumbatia bila kureason hapa ndo tatzo linapoanzia. TZ kuna udini kwa maana kuwa kila mtz ana dini yake ila HAMNA UBAGUZI WA KIDINI. Njoo mitaani uone majirani wanavokaa pamoja wakienjoy,wanacheka,wanapiga soga,wanabishana mambo ya Loliondo,nyie mnaimba udini,mtakesha!
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Mengi ya haya aliyoyasema kuhusu JK na serikali yake ni yaleyale ambayo kina Slaa walikuwa wanasema majukwaani. Tusubiri iwapo CCM watasema Lipumba na CUF nao wanatishia amani na kutaka kuleta machafukao!!!!!!
   
 18. amanibaraka

  amanibaraka JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 258
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kichwa chako sawa kweli wewe?

   
Loading...