Lipumba: CUF haiwezi kufa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lipumba: CUF haiwezi kufa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bangoo, Mar 23, 2012.

 1. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Leo asubui alikuwa tbc akizungumzia mambo mbalimbali kuhusu uchumi na ya chama chake cha cuf. Kati ya meengi aliyozungumza ni hili alisema kwamba Mwalim Julius K Nyerere alitabiri kwamba chama cha cuf hakitakaa kife. Je? wazee wa kale maneno haya ya profesa no 1 duniani kwa uchumi ni ya kweli?.

  Nawasilisha.
   
 2. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,876
  Trophy Points: 280
  Alimaanisha haiwezi kufa Pemba
   
 3. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,459
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Hata mgonjwa wa UKIMWI anashauriwa aishi kwa matumaini! Kifo chake hakitakuwa ghafla ila slowly but sure! Ameshasoma alama akashtuka, ndo maana anakuja na matumaini. CUF anataka ife mara ngapi zaidi ya hapo!
   
 4. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hakiwezi kufa tena coz tayari kimeshakufa kitambo.
   
 5. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumbe wafu nao wanaongeaga!!! Duh! Hii ni hatari.:lock1:
   
 6. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Ni kweli haiwezi kufa mbona hata TLP haijafa!
   
 7. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  dah! Hapo umenena mkuu na mm sina la kuongezea.
   
 8. kanta

  kanta JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 343
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  CUF ife mara ngapi? Ilishakufa na mazishi yake yalikuwa uchaguzi wa UZINI walikoambulia kura 20, Uchaguzi wa Almeru wameshindwa hata kusimamisha mgombea cause wanajua aibu ambayo ingewakuta ni ghalika.
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Kwani iliwahi kuwa hai lini ?
   
 10. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Na hakiwezi kufufuka pia
   
 11. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mtamaliza maneno, midomo itapanuka kwa kusema CUF itakufa, cuf itakufa, mtaiona Cuf hivyo hivyo kama uchi wa mtoto mdogo.
   
 12. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kumbe roho zinawaumaga........CUF sio ita.....ishakufaga Siku mingi kisiasa.....sasahv iko dormant haiwezi ku'erupt tena.....imebaki story
   
 13. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watawala daima huwa ni wabishi! hapo anafahamu fika chama kimemfia mikononi mwake lakini hataki kukiri!
   
 14. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Wakati yeye anafanya uprofesa wa Ki-Sindbad katiak uchumi chama kilanza kuugua

  Chama kimeshakufa anashauriwa akaomboleze kule Zenj kilikofia.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  [h=1]Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba Awashukuru Wananchi na Kuwataka Kujipanga Vyema Kutoa Maoni Katiba Mpya[/h]


  [​IMG]
  Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akiwahutubia maelefu ya wanachama na wapenzi wa Chama hicho katika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako kulifanyika mkutano wa hadhara.
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akimkaribisha Mwenyekiti wa Chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba katika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam ambako kulifanyika mkutano wa hadhara wa Chama hicho. Katikati ni Makamu Mwenyekiti Mhe. Machano Khamis Ali.
  [​IMG]
  Wafuasi wa CUF waliopata ajali siku ya mapokezi ya Prof. Lipumba tarehe 11/03/2012, wakiwasili katika viwanja vya Muembe Yanga Temeke Dar es Salaam kwa ajili ya kumuona na kumsikiliza Mwenyekiti huyo wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
  ---

  Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba amewataka watanzania kusimama imara na kujipanga katika kutoa maoni ya katiba mpya, ili kuhakikisha kuwa katiba inaweka wazi suala la maliasili kuwa rasilimali za Watanzania.

  Amesema Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi zikiwemo dhahabu, almasi, Tanzanite, copper na madini mengine kadhaa, lakini bado rasilimali hizo hazijawanufaisha wananchi kutokana na kutokuwepo utaratibu unaoeleweka juu ya mgawano wa rasilimali hizo.
  Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa Chama hicho wenye lengo la kuwashukuru wananchama na wakaazi wa Dar es Salaam pamoja na Mikoa jirani kutokana na kujitokeza kwa wingi kwenye mapokezi yake tarehe 11/03/2012 Prof. Lipumba amesema iwapo kutawekwa utaratibu maalum kikatiba, maliasili hizo zinaweza kuwanufaisha Watanzania wote.
  Katika mkutano huo uliofanyika viwanja vya Muembe Yanga Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amewapongeza wanachama na wananchi waliojitokeza kwenye mapokezi hayo, na kutaka moyo waliounyesha kwake siku hiyo uendelezwe katika kukijenga chama hicho na kuwa dira ya uchaguzi mkuu ujao.

  Prof. Lipumba amefahamisha kuwa kutokana na kutokuwepo kwa mipango imara ya kiuchumi nchini, kumepelekea kuwepo kwa mfumko mkubwa wa bei kwa zaidia ya asilimia 50, jambo ambalo linadumaza maendeleo ya Watanzania waliopata uhuru miaka 50 iliyopita.
  Amesema kipindi cha miaka 50 ni kikubwa kuweza kuleta mapinduzi ya kweli yw kiuchumi na maendeleo endelevu, na kwamba nchi nyingi tayari zimefanikiwa zikiwemo Singapore, Malaysia na Korea ya Kusini.


  "Tunahitaji uongozi wenye dira ya kuikomboa Tanzania kiuchumi, nchi yetu ina utajiri mkubwa lakini hakuna mipango imara kutokana na ombwe ya uongozi uliopo", alisema Prof. Lipumba ambaye alirejea nchini mapema mwezi huu kutoka Marekani alikokuwa alifanya utafiti kuhusu mambo ya demokrasia na maendeleo ya kiuchumi.


  Amewaeleza maelfu ya wanachama na wapenzi wa Chama hicho kuwa tayari amepata mwaliko mwengine wa kwenda nchini Barcelona mwishoni mwa mwezi huu, ambako atakutana na wataalamu wawili wa kuchumi kutoa nchi za Urusi na Ubelgiji kwa lengo la kujadili matatizo ya kisiasa ya nchi za kiarabu na athari za kiuchumi na kisiasa zinazoweza kujitokeza kwa nchi nyengine.


  Mapema Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amepongeza mapokezi makubwa aliyopewa Prof. Lipumba ambayo amesema yanathibitisha kuwa CUF kweli ni Chama Cha Wananchi, sambamba na wanachama kuwa na uchungu na Chama chao.
  Maalim Seif amekebehi kwa wale wanaodai kuwa CUF ni CCM ‘B' kwamba wana wivu wa kisiasa, na kutoa wito kwa wanachama kutokubali kuyumbishwa katika kukiendeleza chama hicho.


  Katika hatua nyengine mjumbe wa baraza kuu la uongozi la Chama hicho aliyepewa onyo kali wakati Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Mhe. Hamad Rashid Mohd pamoja na wenzake walipofukuzwa uanachama Bw. Yassir Mrotwa, ameibuka na kuomba radhi kutokana kukifikisha Chama hicho mahakamani.


  Amesema atafuatilia mwenendo wa kesi hiyo ili kufuta saini yake isitumike kwenye mwendelezo wa kesi hiyo.


  Wakati huo aliyekuwa naibu mkurugenzi wa uchaguzi wa CUF taifa Bw. Khamis Katuga ambaye alikihama chama hicho na kuhamia CCM, amerejea tena CUF ambapo amerejesha kadi ya CCM na kukabidhiwa kadi ya CUF.


  Ametahadharisha kuwa tatizo kubwa linalorejesha nyuma maendeleo ya chama hicho ni kutokanyika kwa vikao katika ngazi ngazi mbali mbali, huku akieleza sababu zilizomrejesha tena CUF kuwa ni uimara na sera zinazotekelezeka za chama hicho, huku akifunga maelezo yake kwa usemi "asiyejua kufa achungulie kaburi".

  Na
  Hassan Hamad
  Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kwa iyo hii ni taarifa ya kiserikali that y inatolewa kutoka ktk ofisi ya makamu wa kwanza zenji??
   
 17. T

  Topical JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0

  Kumbe hujui kama CUF iko katika serikali Zanzibar?

  Tunakuja kwa kasi kuingia katika serikali Tanganyika..

  Jiulize cdm lini mtakuwa serikalini Zanzibar au hata bara?? mtakesha JF ikulu (zote) kwenu ni ndoto
   
Loading...