Ndumbayeye
JF-Expert Member
- Jan 31, 2009
- 7,420
- 4,032
hajawahi kuwa hata katibu kata
Jamaa anafaa sana kuwa gavana BOT
Hilo neno nililoliweka rangi nyekundu halistahili kuwepo hapo!Mnapotoa mapendekezo pia muwe mnafahamu katiba ya JMT inasemaje, Vinginevyo hili litakuwa sio jukwaa la GTs.
**** mtu mwingine aliwahi ku propose kwamba Lipumba awe mgombea mwenza wa Dr. Slaa or vice versa. This is a wishful thinking. Under our constituttion this CAN NOT HAPPEN. Ni sawa na kuomba mbingu na dunia zishikamane.
Turudi kwenye topic yetu ya Lipumba kuwa WM. Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inaelekeza jinsi ya kumpata WM (Waziri Mkuu)
Ibara 51 (1) - (2). Rais Mteule atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la uchaguzi kutokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi kuwa WM wa JMT. Naye hatashika madaraka hayo mpaka uteuzi wake uwe umethibitishwa na bunge.
Nini maana yake
- Ili Lipumba awe WM, kwanza lazima awe mbunge wa kuchaguliwa
- Ili Lipumba awe WM, lazima CUF iwe na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vingine vya siasa
Baada ya kufahamu hayo naomba sasa uje tujadiliane!