Lipumba anafaa kuwa waziri mkuu!

Lipumba anafaa kuwa waziri mkuu!

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
11,842
Reaction score
18,100
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inahitaji waziri mkuu imara katika serikali ijayo! Mtu ambaye anaweza kusimamia nidhamu ya watendaji wa serikali na uchumi wa nchi! Mtu ambaye atapandisha heshima ya serikali kitaifa na kimataifa!

Hivyo kwa hitaji hili muhimu, UKAWA wana kila sababu ya kumshawishi Mhe. Lipumba agombee ubunge ili Rais ajaye kutoka UKAWA aweze kumteua kuwa waziri mkuu wa Tanzania!

Mungu ibariki Tanzania!
 
Anafaa kuwa waziri wa fedha ili uprofessor wake utumike kurekebisha uchumi ulioharibika. Elimu apewe Mh. Mbatia, kama Dr. Saa hatogombea apewe u waziri mkuu ili ainyoshe nchi na AG atakuwa Mh. Lissu.
 
Mnapotoa mapendekezo pia muwe mnafahamu katiba ya JMT inasemaje, Vinginevyo hili litakuwa sio jukwaa la GTs.

**** mtu mwingine aliwahi ku propose kwamba Lipumba awe mgombea mwenza wa Dr. Slaa or vice versa. This is a wishful thinking. Under our constituttion this CAN NOT HAPPEN. Ni sawa na kuomba mbingu na dunia zishikamane.

Turudi kwenye topic yetu ya Lipumba kuwa WM. Katiba ya JMT ya mwaka 1977 inaelekeza jinsi ya kumpata WM (Waziri Mkuu)

Ibara 51 (1) - (2). Rais Mteule atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la uchaguzi kutokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi kuwa WM wa JMT. Naye hatashika madaraka hayo mpaka uteuzi wake uwe umethibitishwa na bunge.

Nini maana yake
  1. Ili Lipumba awe WM, kwanza lazima awe mbunge wa kuchaguliwa
  2. Ili Lipumba awe WM, lazima CUF iwe na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vingine vya siasa

Baada ya kufahamu hayo naomba sasa uje tujadiliane!
 
Hiyo inajulikana si kila kitu lazima kiandikwe. Aliye sema awe PM ana maana kuwa kama ukawa watakubaliana mgombea wa urais basi Lipumba akagombee ubunge ili ukawa ikishinda ateuliwe kuwa PM kwenye serikali ya ukawa.

Na mimi pia ni hivyo kuwa akagombee ubunge ili ateuliwe kuwa waziri wa fedha kama ukawa itashinda.
 
Uwezo wako wa kufikiri ndo umeishia hapo??!
 
Shukrani kwa kutoa hoja kwa msingi wa katiba iliyopo!
 
Kwani kuna tatizo gani Lipumba kuwa PM hata kama siyo Mbunge. Si Rais Slaa atamteua kuwa Mbunge kisha PM?
 
Kwa mujibu wa katiba iliyopo waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pia atokane na wabunge walio wengi bungeni!
 
Hiyo inajulikana si kila kitu lazima kiandikwe. Aliye sema awe PM ana maana kuwa kama ukawa watakubaliana mgombea wa urais basi Lipumba akagombee ubunge ili ukawa ikishinda ateuliwe kuwa PM kwenye serikali ya ukawa.

Na mimi pia ni hivyo kuwa akagombee ubunge ili ateuliwe kuwa waziri wa fedha kama ukawa itashinda.

Kumbuka ukawa sio chama cha siasa vyama vinavyotambulika ni hivyo vilivyoungana!Na katiba iko wazi kuwa waziri mkuu atatoka katika chama chenye wabunge wengi bungeni...je cuf wanaweza kuwa na wabunge wengi bungeni kuliko vyama vyote???
 
Asante mtoatoa mada umeelewa baada ya kupewa ufafanuz lakn bado kuna watu wanahoj kama hawaielew katba. Pole zao,lakn tusisahau CUF wenye anataka Lipumba awe rais.
 
kuwa professa na uwaziri wa fedha kuna uhusiano gani? Lipumba ni professor wa uchumi sio fedha au biashara. Finance inataka mtu mwenye uzoefu wa kuongoza sio kusoma bali kuongozi kitengo cha finance kama Bank, investment company au Central bank kama BOT. Ukiweka wasomi ambao hawajawahi kufanya kazi tutaona pumba tu kwani watu si vitabu
 
Wenzako cuf washasema anafaa kuwa Rais halafu wewe unazua zogo lako naona unataka ugomvi na watu wa cuf tu.
 
kuwa professa na uwaziri wa fedha kuna uhusiano gani? Lipumba ni professor wa uchumi sio fedha au biashara. Finance inataka mtu mwenye uzoefu wa kuongoza sio kusoma bali kuongozi kitengo cha finance kama Bank, investment company au Central bank kama BOT. Ukiweka wasomi ambao hawajawahi kufanya kazi tutaona pumba tu kwani watu si vitabu
Cuf wakiona post yako hii wanaweza kukutwanga na mawe hujui kuwa lipumba kule cuf ndiyo mungu wao.
 
Kwa mujibu wa katiba iliyopo waziri mkuu lazima awe mbunge wa kuchaguliwa na pia atokane na wabunge walio wengi bungeni!

Maandamano yatafanyika na Lipumba atateuliwa kuwa Waziri Mkuu,UKAWA hawa angalii hilo!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inahitaji waziri mkuu imara katika serikali ijayo! Mtu ambaye anaweza kusimamia nidhamu ya watendaji wa serikali na uchumi wa nchi! Mtu ambaye atapandisha heshima ya serikali kitaifa na kimataifa!

Hivyo kwa hitaji hili muhimu, UKAWA wana kila sababu ya kumshawishi Mhe. Lipumba agombee ubunge ili Rais ajaye kutoka UKAWA aweze kumteua kuwa waziri mkuu wa Tanzania!

Mungu ibariki Tanzania!

Haha,mwaka huu tutaona wazimu wa kila namna!
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Tanzania inahitaji waziri mkuu imara katika serikali ijayo! Mtu ambaye anaweza kusimamia nidhamu ya watendaji wa serikali na uchumi wa nchi! Mtu ambaye atapandisha heshima ya serikali kitaifa na kimataifa!

Hivyo kwa hitaji hili muhimu, UKAWA wana kila sababu ya kumshawishi Mhe. Lipumba agombee ubunge ili Rais ajaye kutoka UKAWA aweze kumteua kuwa waziri mkuu wa Tanzania!

Mungu ibariki Tanzania!

Haha,mwaka huu tutaona wazimu wa kila namna;watu wanalala wakiamka wanazoza tuuu!
 
Kwani kuna tatizo gani Lipumba kuwa PM hata kama siyo Mbunge. Si Rais Slaa atamteua kuwa Mbunge kisha PM?

PM anatokana na mbunge wa kuchaguliwa, jamani someni muelewe na sikukurupuka kujaza server
 
Back
Top Bottom